Balozi wa Marekani kujibu maswali moja kwa moja kupitia mtandao

Balozi Mark Green atajibu maswali kutoka kwa Watanzania kupitia mjadala wa moja kwa moja, kwa njia ya mtandao wa komputa, ambao umepangwa kufanyika Jumatatu Oktoba 29, 2007 kuanzia saa tisa mchana.
Katika kipindi hicho cha majibu na maswali, Balozi Green atajadili kuhusu msaada wa dola milioni 698 utakaosaidia kupunguza umaskini nchini Tanzania, ambao uliidhinishwa hivi karibuni.

Balozi Green amesema kuwa huenda maneno “MCC” na “sheria ya Millennium Challenge” yakawachanganya baadhi ya watu hapo mwanzoni, lakini baada ya muda kidogo, Watanzania watajifunza jinsi mpango huo unavyoweza kuleta tofauti kubwa kwatika maisha yao. “Pindi mkataba mpya wa MCC utakapotiwa saini na Serikali ya Tanzania, utajenga ushirikiano wa karibu zaidi kati ya mataifa yetu mawili.”

Mpango huo wa MCC uliotolewa na wananchi wa Marekani, ni mpango wa miaka mitano ambao lengo lake ni kupunguza umaskini, kuchochea kukua kwa uchumi, na kuongeza kipato cha wananchi kupitia uwekezaji maalum katika miundombinu ya sekta za usafiri, nishati na maji nchini kote Tanzania.

Ili uweze kujiandikisha kushiriki kwenye mjadala huu wa mtandao, tumia anuani yako ya barua pepe kuingia kwenye ukurasa wa tovuti ya
http://webchat.state.gov.
Unaweza pia kuingia kwenye mjadala huo wa mtandao kupitia ukurasa wa tovuti yetu - http://tanzania.usembassy.gov.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...