mdau hadji katuletea grupu letu katika kuwania tiketi ya kwenda kucheza kombe la dunia 2010

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Watanzania hapa ndo pakutafutia sifa. Wao kwani walianzaje, si kama sisi tu na kwenye mashindano hakuna mkubwa wala mdogo cha msingi ni timu na wachezaji wetu kujiandaa kwa moyo mmoja ili kupigania soka ya bongo. Hapa lazima tuwe ngangari ama sivyo tutapigwa mabao mpaka tukiona cha mtemakuni. Naomba kuwasilisha hoja.

    ReplyDelete
  2. Ndugu Wadau. "Amini Usiamini Katika Nchi hizo zote nchi amabayo Kutokana na Taarifa za FIFA za hivi karibuni Nchi amabayo soka lake linakua kwa haraka na kwa hivyo inaogopewa na nchi nyingine zote Africa ni Tanzania. Na kama ingekuwa Nchi yenye Historia ndiyo itakayo shinda bila shaka kusinge pangwa mechi yeyote ile. Tusubili Majibu...."

    ReplyDelete
  3. HILI KUNDI NI ZURI NA BILA YA WASI

    TUNAWEZA KUONESHA MAAJABU


    MTANZANIA KUTOKA MASOMONI INDIA

    ReplyDelete
  4. hivi hawa cameroon wana tafauti gani na senegal au bukina si tushakula nao sasa nini wale woote wenye mawazo ya kizamani kuwa hatuwezi wasichangie hapa nazani ni furaha kuwafahamu maadui zatu mapema ili tupange mikakati kama sisi kama wao

    stars wamekuja hao wenyewe mmoja mmoja tutamchinja

    ReplyDelete
  5. Ghana ilinuka lakini Sauzi kulaleki lazima twende mwanangu.... Maximo jitume na vijana..... Kwenye kundi hapo ni Cameroon tu ndio naona kidogo mchosho lakini wengine hao wallahi ni bwerere kinomaaaa...
    Mungu Ibariki Tanzania na watu wake...

    ReplyDelete
  6. daah wangetutolea hao cameroon

    ReplyDelete
  7. Mshindi wa kwannza kwenye kundi anaenda world cup.
    Mshindi wa pili kwenye kundi anaenda Africa Cup of Nations 2010 Angola.

    Sasa Wa-TZ wenzangu safari ya Angola tunaiona kabisa ipo hapo 2010. (Huyo Cape na Mauritius tunachakaza tu)

    Senegal tulitoa naye draw pale kirumba. Hivyo Cameroon asiogopwe.

    Go go go Tanzania AFCON 2010 and World Cup.

    ReplyDelete
  8. Hilo kundi tushindwe sisi tu. Cameroon maji marefu ingawa tunaweza kuambulia draw nyumbani after all walifungwa na equatorial Guinea ugenini na wakaifunga Rwanda kwa tabu 2-1 mechi ya pili nyumbani. Cape Verde kwenye Fifa rankings ni ya 112, Mauritius ya 161 sisi wa 103. Kwenye qualifying ya Ghana timu hizo mbili zilishika mkia kwenye group zao ila Cape Verde inaonekana ngumu kidogo ikiwa nyumbani maana haikufungwa hata mechi moja hapo ila ilifungwa mechi zote ugenini. Kundi hili lilikuwa na Guinea, Algeria na Gambia pia. Mauritius ilipata sare mbili tu nyingine zote ikafungwa na ilikuwa kundi moja na Sudan, Tunisia na Seychelles. Nafasi ya kuingia second round tunayo kubwa kama moja ya timu nane bora zitakazoshika nafasi ya pili kwenye makundi labda tuchemshe wenyewe.Uwezo tunao, sababu tunayo na nia tunayo...

    ReplyDelete
  9. WADAU HII SASA INAKERA,ALIYEPOST HII KWA NINI BENDERA YETU KAIWEKA KICHWA CHINI MIGUU JUU?NA WEWE ISSA HUKUNOTICE HILO?

    ReplyDelete
  10. astagafulahi,,msalie mtume tumekwisha......
    kasera
    kansas city

    ReplyDelete
  11. Mshindi wa kwanza ktk kundi haendi World Cup moja kwa moja jamaa anachanganya watu hapo juu!! Mshindi wa kwanza wa kundi kwenye makundi 12 na mabest runner 8 kutoka makundi, wote wataingia raundi ya pili ambayo kutakuwa na timu 20 ambazo zitakuwa kwenye makundi matano ya timu nne kila moja, mshindi wa kundi anakwenda Sauzi.Safari hii tumepewa nafasi 6 jumlisha na Host South Africa!!

    ReplyDelete
  12. haki ya mungu tena siamini km tumeenda SOUTH...manake hili kundi ni mchekea ni hakuna mfano!!! huyo cameroon kwao draw kwetu mbili kavu atake asitake!!!

    ReplyDelete
  13. Hili kundi ni gumu, kwenye mpira wa miguu hakuna kundi jepesi unless kama unapanga timu kwenye karatasi ila uwanjani kila timu ni ngumu. Tuandae timu mapema tuache hadithi nyingi yasije yakatokea ya Ticotico tena!

    ReplyDelete
  14. KAMA WAO WAMEWEZA WANA NINI?
    NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI?
    LET'S THINK BIG

    MAMA F

    ReplyDelete
  15. Mama F, sisi tunashindwa kwa sababu HATUWEZI na HATUTAKI KUWEZA, tumebakia hadithi nyingi na porojo.

    ReplyDelete
  16. LA...HAULA..LAKWATA..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...