Home
Unlabelled
mwenge wa olimpiki wamulika dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Unaitwa mwenge sio mwenye. Angalia usijesema mwanya... hiiiiiiiii
ReplyDeleteThe whole world is in protest about human rights violation in China. The tourch should sent the same massage to Tanzania on violating the peoples constitutional rights in Zanzibar.
ReplyDeleteThe single massage should be Tanzania is not just for CCM.
Sio massage ni message. sio lazima kutema ngeli hapa, tumia lugha ya Taifa
ReplyDeleteThe whole world is standing against invasion of China in Tibet. Tanzania need to stand against mauaji ya China kwa wananchi wa Tibet na kutia chachu mauji ya Dafur
ReplyDeleteUchina inakiuka haki za binadamu sio kwa Tibet tu, hata kwa raia wake. Wananchi wengi wa kichina hawana sauti kwani wanauawa. Tanzania tuna freedom of speech.
ReplyDeleteUnafiki mtupu! Olympic imeaandaliwa kwenye nchi ngapi zenye utata juu ya haki za binadamu? Australia haina utata juu ya haki za binadamu? Au Aboriginals siyo watu? Marekani tena Atlanta hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu? Ushenzi wanaofanyiwa Roman (Gypses), wakimbizi wa Kialbania na wahamiaji wengine toka nchi za dunia ya tatu nchini Ugiriki siyo ukiukwaji wa haki za binadamu? Spain hakuna jamaa wanaotaka kujitenga? Tofauti ya madai ya Bask/ETA na Wacorsica kule Ufaransa na waTibet wa China ni nini? Spain, USA, Greece, Australia zote hizi zimeandaa Olimpiki mbona hakuna aliyejitokeza kuwatia shinikizo la haki za binadamu? Mnakumbuka Catherine Freeman alipokimbia na bendera ya Aboriginal kukumbushia ukiukwaji wa haki za binadamu (Aboriginals) jinsi vyombo vya habari vya kimagharibi vilivyomshupalia kama mtovu wa nidhamu? Jamani wakati mwingine tusiwe wepesi sana kughilibiwa.
ReplyDeleteHaki za binadamu zinaonekana kuvunjwa na wengine tu! Mugabe anaweza kuwekea vikwazo vya uchumi, kijamii, mpaka kisiasa na anafanyiwa njama zinazomfanya achukiwe na hata wasiojua kuchukia. Njama hizi hazijaanza leo. Kaangalie historia ya Ghana (Nkrumah), Congo(Lumumba), Chile (Allende)na tukio la hivi karibuni Iraq ndiyo utajua nini kinachoendelea. Ikiwa kama Mugabe kakaa madarakani muda mrefu je amekaa muda mrefu kuliko Gadhafi au Omar Bongo? Vipi Hosni Mubarak na Paul Biya wamekaa muda mfupi? Kama ni hali mbaya ya kiuchumi, udikteta na kukaa madarakani muda mrefu mbona hawakwenda kumchomoa Fidel Castro ambaye katawala Cuba takribani nusu karne? Tena kishawahi kuwaelekezea makombora Marekani!
ann wa 10:32 nakuunga mkono na mguu kwa hali na mali.
ReplyDeleteChina inapigwa vita sana na nchi za magharibi US/Uk na nyingine kwani maendeleo iliyonao na kasi inayoibuka nayo ni kubwa mno.
Kiuchumi nchi za West hawaiwezi China na wanaonea wivu Olimpiki yao itakuwa kali kuliko zote. Wachina kwa mapamba utazimia.
Ndiyo jamaa ni "wavutaji" lakini angalau hawa wanavuta na kupulizia kama panya kuliko Us na Uk wanaotumia nguvu, mabavu na mtutu wa bunduki kama wafanyavyo huko Iraq, Afghanstan, Sierra Leone na kwengineko.
Watu wengi hawaelewi na ndiyo maana wanashindwa kuivamia Zimbabwe kwa sababu hakuna kitu kule. Wanadai Mugabe mbabe kwa wazungu...mbona Nyerere alifanya Azimio la Arusha?
Hivi kidampa gani atoke Afrika na kuishi UK au US na kudai anamiliki ardhi akakubaliwa? LETS OPEN OUR EYES WADAU.
Maendeleo ya CHINA ni kiboko na ndiyo maana hata bidhaa zao zinakamatwa na kuchomwa moto nchi ngeni ili kuua UCHUMI wao na kuona bidhaa zao feki!KUMBE WIVUUUU TU
Wewe anonym wa apr 14,10:32 umemshupalia Mugabe tadhani unachokisema cha maana.Kama huko nyuma watu walifanya makosa kuyafumbia macho maovu hayo basi waendelee kuyafumbia macho hata hivi sasa?Dunia inabadilika kwa kasi kubwa sana,na vijana wasio ogopa kusema ukweli tofauti na wazee wao waliotawaliwa katika mazingira ya UOGA WA KIJINGA wanazidi kuongezeka siku hadi siku.Hebu kasome historia ya Tibet kabla hujaanza kuropoka utumbo katika blogu hii.Yaliyotokea DARFUR bila shaka hujayasahau,je watu waendelee kukaa kimya eti?Mugabe mwenye umri wa miaka 85 hivi sasa na kesha kaa katika Urais kwa miaka 28 sasa anachokitafuta katika Urais wa Zimbabwe hivi sasa ni kitu gani?Basi katika Chama chake mwenyewe cha ZANU PF hakuna Mzimbabwe mwengine wa kuongoza nchi isipokuwa yeye pekee?Alipoingia msituni ili kumng'oa Ian Smith alichokuwa akikipiga vita ni Utawala wa Watu Wachache katika misingi ya Kidikteta,siyo?Iweje yeye kaingia madarakani asahau kile alichokipiga vita na yeye mwenyewe kukiuka misingi ileile ya utawala wa kidemokrasia alyoitetea miaka yake yote?Pale alipo Mugabe ana akili gani na nguvu gani tena za kuiongoza Zimbabwe mpya au MRADI KUROPOKA TU BILA YA MSINGI WOWOTE?Hao kina Gadhafi,Mubarak,Biya,Museveni,Santos na wengine pia watambue kwamba wakati wao wa kuongoza umekwisha,kama kweli wanaitakia Afrika mema basi kwa hiari yao wenyewe wakabidhi madaraka yao katika chaguzi za kidemokrasia katika nchi zao,wasisubiri ghadhabu ya wananchi katika nchi zao.China ikikiuka haki za binadamu isikemewe eti kwa sababu wengine hawakukemewa?Hatwendi hivyo Mzee,samahani sana mtatuharibia nchi?Ukiulizwa,amani na utulivu?Bila ya haki amani itakuwepo kweli?Au watu wenyewe ndiyo wastaarabu tu,vinginevyo pasinge tosha hapa nakuambia!
ReplyDelete