
Warning Guys!
That's known as pyramid scheme. Very few people get rich, the ones who run this idiotic scheme. It has made a lot of people more poor. It operated in South Africa, Zimbabwe, Germany and UK. In actual fact its a criminal offence in UK and if caught you end up in Jail.
Unaweza google au nenda wikipedia na search Pyramid scheme. Mchongo wenyewe wa kuingizana mjini inakuwa kama ilivyoelezwa hapo chini
--------------------------------------------------
1: Kijiji kina watu 10000
2. Watu wa 10 wa kwanza wasio na fedha wanaanzisha mradi wa DECI. Wanasema kujiunga nao ni Shs. 200,000Watu 1000 wanajiunga kwa kutoa Tsh200,000 kila mmoja. (Kijiji kinabakia na watu 8990. Kwa kiyo Mtaji wa kwanza ni: Tsh. 200,000,000 (za wale watu 10)Hawa wanaambiwa wasubiri miezi minne ili “wavune” faida.
3. Wanatangaza na watu wengine 1500 wanajiunga kijiji kinabakiwa na watu 7490Watu wale 1500 wanaleta mtaji mpya wa milioni 300,000,000 Miezi minne inapopita wale 1000 wa kwanza wanalipwa fedha yao milioni 200, na kila mmoja anapata “faida” ya laki moja moja hivyo kila aliyeingia na laki mbili miezi minne anatoka na laki tatu!
4. Wanaingia watu wengi zaidi sasa nao wanafikia 2000 nao wanataka haya mavuno! Kijiji kinabakiwa na watu 5490 ambao sio wanachama.
5. Wale watu 2000 wanaingia na mtaji wa 400,000,000. Sasa hapa ndipo kuna kitu cha kuangalia vizuria. kuna watu 1500 ambao wanatakiwa kulipwa laki mbili zao (kwa jumla ya milioni 300 za mbegu). Lakini pia wanatajia kupata kila mmoja laki moja zaidi kama faida.b. Hivyo pamoja na kiasi hicho unatakiwa mradi wa milioni 150 zaidi kama faida ya kundi lile la pili.c. Kiasi hicho kinatolewa kwa wale waliokuwa na milioni 400 na hivyo kufanya wale wanaoingia na milioni mia nne kimsingi kuwa wamekingia na milioni 250! (hilo si tatizo kwa sasa). d. So wale wa kundi la pili wanaondoka na wao na laki tatu tatu kwa furaha ya “mvunaji”
6. Hivyo kampuni yetu inaanzisha recruitment drive nyingine na watu wengine 3000 wanajiunga na kampuni yetu hii ya mavuno. Kijiji kinabakiwa na 2490 ambao wengi wao wanaonekana kuwa ni wanachama wa JF!! Hao nao wanaingia na mtaji wa 600,000,000!
7. Hivyo muda umefika wa kuwalipa walioingia na milioni 400! So wale milioni mia nne kwanza wanalipwa “seed money yao) ambayo ni kiasi hicho hicho. Lakini wanataka faida yao ya laki moja moja kila mmoja. - Hivyo zinahitajika milioni 200 nyingine na hivyo kuchukua kabisa mtaji wa wale wa milioni 600, kuwalipa wao na hivyo wale wa milioni 600. So wale wa milioni mia nne wanaondoka kwa furaha kwani wamepata fedha yao.
8 Wale wa milioni mia sita (ambao ni wengi zaidi – 3000) na wenyewe wanaambiwa wasubiri fedha zao hadi mwisho wa miezi minna. 9. Sasa recruitment inaenda na kuwashawishi wale 2490 waliosalia kijijini kujiunga ili “wavune. Nao wanaingia na mtaji wa 498000! (mara moja tunaona kuwa wanaingia na kiasi pungufu. Kampuni yetu ifanye nini basi; 10. Kampuni inawashawishi wale waliokwisha pewa mavuno yao kuzizungusha fedha hizo hizo tena kwenye mfumo huo. Kwa hiyo wale wa 1000, na wale 1500 na wanatakiwa kuzungusha fedha zao humo kwa humo.
NOW THIS HOW THE SYSTEM COLLAPSES
SCENARIO ONE:
a. Baada ya wale 2490 kuingia na kulipa milioni 498 wale wa milioni 600 watajikuta wanapungukiwa Sh 102! Bila ya fedha kuzungushwa tena kundi la milioni 600 wataanza kulalamika.
b. Wakati hao wanaanza kulalamika kundi lile la 2490 linasubiri kiasi walichoingia nacho (kwa maana angalau waliokwishalipwa awali idadi kama yao wawe wamzungusha tena fedha). Na pia wanasubiri milioni 249 kama faida! (kwa maana ya kwamba wanahitajika watu wengine kama 50 hivi kujiunga kuweza kuzalisha hiyo faida.
SCENARIO TWO:
a. Hii inategemea idadi ya watu ambao wako tayari kuzungusha fedha zao ndani kwa ndani. Kinachofanyika hapa ni saikolojia ya fedha. Wakikupa laki moja faida na wakakuambia uziingize tena kwenye system itabadi urudishe laki mbili kwao tena, na wewe unabakiwa na laki moja! Katika mfano halisi wa DECI ni kwamba wanakulipa laki tatu, na unaweza kuzirudisha kwa mafungu laki mbili mbili, hivyo utarudisha kwao zile za kwako (laki mbili) za kwao (laki mbili) na wewe unabakia na laki moja! Ulichofurahia kimsingi ni wewe kuwa na “laki tatu” kwa muda fulani, siyo kuzitumia.
b. Hili hata hivyo linatabia ya kuchosha huwezi kuwa na fedha usiyoitumia! Hivyo collapse ya pili itatokea pale watu ambao wamekuwa wakizungusha fedha zao huko kwenye kampuni watakapoamua kuziondoa kwenye mzunguko! Kwa maneno mengine wale 1000, na wale 2000 na wale wa 3000 watakapoamua kuondoka na fedha zao wale wa mwisho 2490 watajikuta wameliwa karibu milioni 500!
Hahahahaaa, Hapo wadau mkilizwa kwa kuingia mkenge huu kicha kichwa msianze oooohh hamkutustua mapema, mara ooooohh JK mbaya kuruhusu haya, mara oooooohhh kwa nini serikali isipige marufuku kama ilivyokuwa Kenya. Eh Kalagheni baho, ila mnaambiwa hii ni kanyaboya mwenye macho asikie na mwenye masikio na aone!
Source
KUHUSU DECI, HIZO THEORY AU EXAMPLES ULIZOTUMIA KATIKA HII DECI YA TANZANIA HAZITUMIKI, KWA SABABU ILI MTU AVUNE HAITAKIWI MTU MWINGINE AINGIE ILI YEYE AVUNE... NA PIA MTU AKIPANDA MARA MOJA... HAKUNA KITU KINACHOMLAZIMISHA APANDE TENA.... ILI AWEZE VUNA.... AKIPANDA NI KWAMBA ANAONGEZA MBEGU ZA KUVUNA.
ReplyDeleteNACHOONA HAPA WATU WANATAKA KUJUA DECI INAPATA PESA WAPI.... LAKINI HAIFANYI PONZI SCHEME HATA KIDOGO.
KUNA WATU WALIANZA TOKA 2006... MPAKA LEO ZILE PESA ZA KWANZA WANAVUNA.... SASA HIYO PONZI ISIYO COLLAPSE NI IPI... NINAVYOJUA PONZI MTU AKIMALIZA CIRCLE ANATOKA AKITAKA ANAANZA UPYA... LAKINI DECI ILIKUWA UKIINGIA UMEINGIA....
USHAURI WANGU AU MAONI... KAMA KITU UKIJUI USIPENDE KUKIONGELEA... NI HATARI... UTALISHA WATU SUMU.
KUMUAMBIA MTU AMBAYE AMEFAIDIKA MARA MOJA, KUWA HAKUNA SHORCUT KWENYE MAISHA, INAKUWA NGUMU.
ReplyDeleteYANI HAWA DECI WAKIHAMA HAPO WALIPO SASA HIVI, SAY WANACHAMA WAKIENDA KESHO WAKAKUTA OFISI IMEFUNGWA, HAWANA PA KUENDA KABISA!!
MIMI NIMEULIZA KADHAA, WALICHONACHO NI RISITI MOJA TU, AMBAYO INA TIN NUMBER ETI NDIO KITHIBITISHO!!
SERIKALI INABIDI ISEME JAMBO LA MSIMAMO MARA MOJA. SIYO KUWATAHADHARISHA TU.
MBONA SCHEMES ZA PESA KAMA M PESA ZINASIMAMIWA KOONI?
JE HAKUNA SHERIA?
JE SHERIA INAHITAJIKA?
Kila mtu anakuja na hii story ya pyramid scheme.
ReplyDeleteCha ajabu hao DECI wapo, kwanini wasipewe nafasi wakahojiwa ili wadau wajue wanaendeshaje biashara yao na wanawezaje kulipa hayo mafao kwa watejea wao.
Hapo tutaweza jua kama hii ni pyramid scheme au la, vinginevyo itakuwa ni kuongea out of emotions kwa vile story kama hii ishatokea sehemu zingine duniani.
Naamini kama kungekuwa na ukweli tosha juu ya uendashwaji wa hii DECI ingeshafungwa au kusimamishwa maramoja, cha ajabu kila mamlaka inajaribu kujikinga isionekane kuhusika. Nazungumzia BOT na CMSA. Hapa kila mtu anaepusha bawa lake. Na hii si suluhu, kwa vile hawa jamaa wa DECI bado wapo na hawajafunga ofisi, ni wakati muafaka wakahojiwa na kujua nini kinacho endelea, masula ya tume ni ujinga tuliouzoea. Hii kitu iko more than simple kwa mtu aliye makini.
Kama hawajamaa wapo zaidi ya miaka mitatu wanasubiri nini?
Wangesha sepa longtime nionavyo mimi,maana so far watakuwa na hela ya kutosha na sijui hizo scheme zingine zilikaa muda gani mpaka kusitukiwa.
Msimamo wangu: Mpaka sasa sioni tatizo la DECI kwa kuwa naona hizi story ni za upande moja tu. Hawajamaa watoe mchakato wao wa kuweza walipa hao wadau wao hayo mafao baada ya kupanda
Pili: Kama serikali inasema hao jamaa wako kinyume na sheria pamoja na wateja,wafungiwe na wateja wao washitakiwe mara moja.
Tatu: Kinyume cha hapo basi serikali na jamii yake BOT na CMSA hawana wanachojua kuhusu DECI na biashara yake na hawajui limitation ya kibali amabacho DECI ilipewa, wawe wawazi katika hilo.
Wadau wote wawili yaani mchambuaji na mtoa maoni wa kwanza wapo sahii. mchambuaji kajalibu kuwaasa watu kutokimbilia mambo hovyo kwa kuwa kuna baadhi ya nchi wamepata adhari kubwa na sasa baadhi ya watu wanalia. pia naungana na mtoa maoni kuwa kama una uhakika na jambo si vizuri kulizungumzia.
ReplyDeleteIla mimi napenda kumuunga zaidi mkono mchambuzi kuwa tahadhari ya hari ya juu inatakiwa. maana kuwa nchini kwa miaka mitatu si kigezo kuwa jambo kama lililiookea kenya haliwezi kutokea hapa.
hawa ni watu waliojipanga kiakili sana na wanachukua kila aina ya tahadhali.
Hivyo si vibaya kwa wanachama kuwa makini, inaweza kutokea ya kutokea mkaanza kuinyooshea vibaya serikali wakati mlijiunga wenyewe kwa matakwa yenu.
Kwa maelezo haya, ina maana waendeshaji wa hiyo DECI hawapati chochote? maana fedha yote wanapewa wawekezaji kama faida. La pili, Hawana utaratibu wowote wa kuziwekeza hizo fedha? Kwa mfano kununua hisa, kufanyia biashara fulani nk.
ReplyDeleteKwa upande wangu naona haya maelezo hayajitoshelezi, kwa maana hayaonyeshi waendeshaji wa DECI wananufaika vipi na huo mradi!
This is arrogant explaination, am sorry i call it that way...
ReplyDeletewakati wazazi wetu pesa zao zipo in jeorpady nyinyi mnaleta michezo ya kipuuzi hapa. Bank Kuu didn't use the smart way kuzuia hii ponzi schem. Kilichakuwa kinatakiwa ni smart move ya kurecover pesa za watu...
Some time i feel kutapika nikiwaza mambo yanafanyika nyumbani.
Mchumi wa Texas
Kweli wajinga ndio waliwao!!!!!!!!!!
ReplyDeleteNO MATTER THE COUNTRY USHALIWA HIVYO....SASA JIPANGE TENA
DECI ni Madoff, Ponzi Scheme. Ushauri mmepewa,kukubali au kukataa ni juu yenu. Ni suala la muda tu.
ReplyDeleteKibaya zaidi wanaoshiriki kwenye huu mchezo, sidhani kama wana upeo na DECI inavyofanya kazi.
Mfano mzuri ni Long Term Capital Management. Hii kampuni ilifilisika. Ilikuwa na battallion ya mathematicians, computer scientists, nobel prize economists professors. Ingawa case yao ni tofauti na DECI,lakini ndio wale wale.
Kazi kwenu!
maelezo yako ni magumu sana kufuatilia...lakini ni ya ukweli. sasa kama watanzania wanaendelea na ubishi, wee waache tu. Tutumie common sense
ReplyDeletejamani ndugu zangu Watanzania.
ReplyDeletehakuna utajiri wa haraka kihivyo. hao DECI hawafai.
uzoefu unaonesha wameliza watu huko Kenya cha ajabu jina ni hili hili la deci na shughuri ni hizi hizi na pia deci ya kenya ilikuwa chini ya Taasisi ya Kidini kama ilivyo hiyo.
ukiwa chunguza kwa makini utagundua jamaa hata kodi hawalipi wanalipa TIN ya 95,000 kwa mwaka hebu jiulize iweje Taasisi inayohozi mamilioni ya watu harafu inaishia kuripa kodi ambayo anastahili kulipa mmiliki wa kiosk?
Watanzania tuache ubishi DECI haifai naiunga mkono serikari na ikiwezekana waipige marufuku
Nikutumia akili tu, kuwa hawa hawazalishi, hawana mkopo, nini hatima yake, kwani kwa namna nyingine ni kuwa mnachangiana wenyewe kwa wenyewe, na wa mwanzo watavuna,kwa vyovyote wa mwisho watalia kilio cha sintosahau!
ReplyDeleteM3
Mtoa mada ulichosema ni kweli,na thanks kwa tahadhari. Ila ukiangalia kwa jicho la tatu ni bonge la opportunity, manake kabla ya kucollapse kuna watu wanafaidika..hivo anayeingia mapema anapeta, hivyo mimi naenda kujiunga DECI sasa hivi, nishaona opportunity hyo, DECI itakuwa itakufa, lakini sio siku za karibuni, huu ni wakati muafaka. Wacha 'wajinga' tule , nyie wasomi mtabaki hivo hivo na hesabu zenu za kwenye makaratasi.
ReplyDeleteBongo Blogger
Mchumi wa Texas, unaongelea recovery ya pesa zipi? Unaambiwa kwa muda mrefu watu wamekuwa wakivuna fedha DECI, sasa unapokuja kuwaambia hii Ponzi Scheme, lazima uwe na maelezo ya kuwaridhisha hao wanaopanda fedha zao. Kuna watu wanadhani kuna njama za kuiua DECI kwa sababu wateja wamepungua kule kwenye mradi wa nanihii. Nadhani cha msingi, hao DECI wapewe nafasi ya kuelezea mradi wao unafanyaje kazi, kma hizo pesa wanawekeza na faida ndio wapanadaji wanapewa kama mavuno, au bw. Yesu anakuja kujazia hicho kiwango kinachotolewa kama faida.
ReplyDeleteMchuuzi Dar.
Naona ni mchezo mzuri hasa pale unapopata referee kama serikali (BOT). Acheni watu waendelee kuchangiana "to infinite". Hao waliokumbwa na dhahama hilo tunawapeni pole sana kwani wao hawakupata bahati walionayo hawa wa sasa. BOT tafadhali simamieni mchezo huu tuone mwisho wake. wamiliki hao wa DECI watoe dhamana kadri mapato ya yanavyoendelea.
ReplyDeleteNa pia inasemekana si DECI tu kuna wengine wameibuka huko kwa mgongo wa dini kusaidia wajane, watu wasio na kipato n.k.
Jambo hili ni imani, likisimamiwa vizuri wengi wataneemeka, ukizingatia wengi hawana elimu ya ujasiriamali. Najua kilicho na mwanzo lazima kiwe na mwisho, hata makampuni makubwa yaliyosajiliwa Ulaya hata America yamekuwa yakisambaratika kila kukicha sembuse DECI.... Ujanja kuwahi na kupata.. The Higher the risk the higher the return, msisitizo huo.
Msiniroge.
kekundu kekundu kekundu................
ReplyDeleteMpaka watu walizwe,ndio watajua kumbe ni PONZI SCHEME!
ReplyDeleteNa hao BOT wanachunguza nini! Unaweza ukawa na PHD 3 lakini uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo ukawa mdogo.
Tatizo letu kila kitu ni dili!
Watanzania wenzangu, hapo DECI hakuna kitu. Wanaosubiri kuvuna mbegu subirini, ambao hamjapanda tafuteni mashamba mengine. Hutavuna kama DECI lakini usalama upo.
People, hebu toeni theory zenu hapa.
ReplyDeleteDECI iko bomba. Mi nishavuna milioni tatu mpaka sasa kwa investment ndogo tu.
Game ya DECI ni:
1. Wekeza kiasi ambacho hata kikipotea hutaumia sana. Mfano kama una 500,000 wekeza 50,000 tu. Sio una laki tano halafu unawekeza 400,000 hapo utalia na kusaga meno mambo yakienda mrama.
2. Usiishi mjini kwa kutegemea DECI tu. Piga deal zingine kwa pesa utakayovuna DECI, then rudi kuwekeza tena kiasi kidogo tu.
This is Bongo bwana... akili mkichwa. Na hii longo longo ya BoT sijui CMSA ndio inazidi kuipandisha DECI chati.
Kuna vita baridi kati ya maskini na walionacho...huyu mwandishi ni maskini tu kwa muono wangu, sasa amejawa emotions na anaonekana anaandika kwa jazba na haraka ndio maana hata makosa ya maneno ni mengi, haraka ya nini ungetulia uje na kitu cha kueleweka. Hebu fikiria mimi ambaye nimeambulia patupu suala lako la deci (na umewataja deci deci deci sijui kwa ruhusa ya mahakama gani kuhukumu) je yule unayemwita mjinga si ndio atazidi kuendelea, tulia, tafuta mifano halisi na uje na maelezo mazuri
ReplyDeleteWalau ungesisitiza kuwa hakuna uwezekano wa kupata pesa kirahisi namna hiyo ila kuwahi kuchukua michoro ya wikiP na kuileta huku wala husaidii! Pia ukija uje na maelezo ya upande wa pili wa shilingi, je DECI wanasemaje, BOT na wengine sio kuja kujidai ni Pyramid Scheme! Kisha mfano wako unasema kijiji cha watu elfu kumi, unadhani deci hawapokei wazungu, so ungeleta hesabu za kila mtu dunia nzima uone deci inakuja kufa mwaka gani!
Bongo!!!! Forums kibao ni za kuponda tu wakati wote ni tiamajitiamaji!
Hivi mbona upatu zote huwa haziendi muda mrefu. Lazima kuna kitu kitatokea na watu wata-loose tu. Wajinga wataendelea kuliwa kila siku, especily wanaopenda shortcut ya maisha........
ReplyDeletepyramid scheme hii inafanyika sana hapa sauz hasa ktk location za watu weusi na watu wanakula bingo kichizi na mwisho wake inakuwa story na kesi zisizoisha na pesa za wengine zinapotea na wengine wamelamba wale wa mwanzo tu na mwenye scheme tu alafu wanakimbia nchi
ReplyDelete1. Namshukuru alieanza thread hii maana taarifa zake ni za muhimu mno na ni muhimu zienee haraka oili watu wengi zaidi wasije wakatapeliwa. Natamani TEKNOHAMA ingekuwa imeenea kote Tanzania ili watu wajue haraka.
ReplyDelete2.Nasikitika na kushangaa kwamba DECi imeweza kuendesha utapeli kwa miaka 3. BOT iko wapi inafanya nini? Huu ni ushahidi dgahiriwa finacial regulatory system yetu. Na bila shaka huko kwenye mabenki ya nje tunaoigwa bao zaidi kwenye forex mnarkets na capital is flying out like no one's business. Tatizo ni kwamaba hata Governor aliyepita nae alikuwa busy na utapeli, sasa regulation itatoka wapi. Hata kasi ya sasa hivi ya kuzima huu utapeli ni taratibu mno na ukweli wa mambo inaelekea kuna wateja amabao wana imani kubwa zaidi na matapeli DECI kuliko na BOT. BOT ina mkazi kubwa sana ya kuridisha confidence ya watu wa Tanzania.
3. Kazi amabayo bdugu yetu ameianzisha hapa ya kuuelimishs umma ndiyop hasa kazi ambayo BOT ilipoaswa kufanya na siyo leo lakini siku nyingi tu; maana this is not the first Ponzi scheme in Tanzania, alafu zilizotangulia ni mbaya zaidi maana zilihusisha wake za wakubwa. Kweli kweli watanzania tunahitaji viongozi wanaofanya kazi kwa principle. Hii ni sura nyingine ya ufisadi jamani. Wake up jamani nyie mnao bisha.Someni jamani kwenye internet na encyclopaedia na vitabu vya historia: Ponzi/Pyramid schemes zina historia ndefu tu na zimepigwa marufuku nchini kwingine ambako tayari utapeli huo umeonekana.
4. DECI haifanyi investment yoyote. Haiwekezi popote.Inawalipa waliotangulia kuweka kutokana na pesa zinazoweka wanaofuata kuweka pesa. This is a hallmark of a Ponzi sceme.
5. DECI haina account popote, pesa zinawekwa kwenye account binafsi za waanzilishi wa DECI.Fikiria kama ni FDR ya mabilioni ya miezi mitatu sita na kadhalika- hiyo interest ni ya wenyewe siyo ya wanaotapeliwa.
5.Kwenye Pyramid/Ponzi schemes zote waliotangulia ndiyo wanapata na wanapopata wanaeneza 'injili' ya ponzi scheme na kuwavuta watu zaidi kuweka pesa.Hii ni Hallmark nyingine ya Ponzi schemes- ukiwa mwanzoni utapata tu. lakini ukae ukijua ulichopata ni jasho la waanaofuata ambao watalizwa tu.
6. Mwanzo wa mwisho wa ponzi schemes zote ni watu waliyoweka pesa kuelimika. Wanaposhtuka watataka kutoa pesa zao. Mwanzoni huenda ikawa rahisi kutoa, lakini baadae masharti ya kutoa pesa yanakuwa magumu na hatimae kuna kuwa hakuna pesa na mwishoni walioanzisha hiyo scheme wanapotea au wanakamatwa.Historia ya naman hii iko sehemu nyingi tu duniani hasa marekani na ulkaya ambako vitu kama DECI ni marufuku toka karne zilizopita!!!!
7. Nilisiskitika kuona kwenye Gazeti la Mtanzania Jumapili ya 5 Aprili 2009 ikitetea DECI ambao ni ufisadi na utapeli. Eti makala inahoji DECi ina ubaya gani?Eti makala inasema DECI ni mkombozi wa wanyonge. Eti ukurasa wa kwanza unasema Mzee Iddi Simba maeitilia fitna DECI Benki Kuu ndiyo maana BOT imeanza kutoa tahadhari kwa wateja wa DECI. Eti ukurasa wa kwanza wa Mtanzania unasema Iddi Simab na wasiwasi kwa sababau yeye ni kiongozi wa PRIDE (microfinance institution inayotoa mikopo kwa wawekezaji wadogo na wa kati)na DECI inaonyesha ushindani mkubwa. This is the most ignorant crap I have read in any paper in my life. Ni hatari kwa kweli kwa taifa kuruhusu uandishi wa aina hii unaoweza kuwapa imani katika kitu cha kitapeli kama DECI. Sijui Mtanzania litakuwa wapi watu watakapoanza kuambiwa pesa zako hazipo? Hivi sheria ya ownership ya magazeti ya nchi hii inasemaje? Na je mtu yoyote anaweza kuandika chochote tu. Mtanzania is leading people to the slaughter house.Aliyeandika ile makala si mjinga tu bali hakufanya researd=ch ya aina yoyote- eti ansema mbona watu wanapanda na kuvuna pesa vizuri tu?
8. Hakuna short cut ndugu zangu bali kuchapa kazi kwa maarifa. Msije mkapotea na ushauri wa Magazeti kama Mtanzania. Gazeti limeoza tangu Ulimwengu amuuzie mtu mmoja hivi. Gazeti linapotosha watu, linachafua watu. Iddi Simba is an finacial expert of long standing na aliwajibu Mtanzania vizuri na labda kigentleman mno kwamba PRIDE haiwezi kuwa na wasi wasi na watu wanaoendesha kamali- lakini ukweli Mze Simba ni vizuri kuwa very direct na kuwaambia wananchi moja kwa moja kwamba DECI ni utapeli na ufisadi ili kuepusha madhara zaidi.Alafu Mtanzania utalinganishaje microfinance institution yenye track record ya miaka mingi tu, zaidi ya 20, hapa nchini inayoendelea kukua mwaka hadi mwaka hapa nchini, yenye loan repayment rate ya karibu ya 90%, ambayo inakaribia sasa kuweza kutimiza masharti ya kuw a benki kamili.Hivi Gazeti la Mtanzania linajua linafanya nini kweli?
9. Na hivi BOT mlikuwa wapi kwa miaka 3 bila kuichukulia DECI hatua. Aidhahii si Ponzi scheme ya kwanza hapa nchini. Zinaanzishwa zinaliza watu na matapeli wananufaika na kuondoka. Mnafanya nini? What the hell are you doing?
10. hata kama ni Mzee Iddoi Simba aliyewatonya kuhusu DECI alikuwa na kila haki. Ponzi scheme zinaweza kutorosh pesa kwenye nzunfunguko wa kawaida wa uchumi na sekta ya benki/fedha mkajikuta mashindwa kuilinda finacial system na watu wamepoteza life savings zao. Na hii ikitokea wakati wa recession basi this can only deepen the recession. Wake up BOT wake up.You should never have allowed DECI to get this far. This is the major conclusion of this scandal kwamba hakuna usimaizi wa sekta ya fedha.
1: Kijiji kina watu 10000
ReplyDelete2. Watu 10 wa kwanza wasio na fedha wanaanzisha mradi wa DECI. Wanasema kujiunga nao ni Shs. 200,000 Watu 1000 wanajiunga kwa kutoa Tsh 200,000 kila mmoja. (Kijiji kinabakia na watu 8990 this is WRONG for this Case 9990). Kwa kiyo Mtaji wa kwanza ni: Tsh. 200,000,000 (za wale watu 10)Hawa wanaambiwa wasubiri miezi minne ili “wavune” faida.
Proof Read Your Propaganda Next Time, Au Ulifeli Hesabu Darasa La NNE?
BOoSt3D.
Waliopo ktk mchezo huu kwa sasa wanahitaji kujua namna ya kurudishiwa fedha zao, maelezo mengine hayawasaidii maana mchezo umefungwa na wamekwisha weka fedha zao. Ilitakiwa aliyefunga isimamie kuhakikisha fedha zinarudishwa.
ReplyDeleteAnon wa Tarehe April 08, 2009 7:16 PM
ReplyDeleteUmesoma shule kweli?
Kijiji kina watu 10,000
Waanzilishi wa DECI 10
Watu 1,000 wanajiunga
Kwa hiyo 10,000(Wanakijiji wote)-10(Waanzilishi)-1,000(Waliojiunga)
=8,990
Best of luck!
Anon wa April 08, 2009 7:22 PM
ReplyDeleteFedha haziwezi kurudishwa! Kwa sababu mbegu za mtu mmoja ndo mavuno ya mtu mwengine, hakuna njia ya huu mchezo kuisha bila watu juingia hasara, labda serikali iwafidie, kitu ambacho bongo hakiwezi kutokea.
wadini na wenye busara tusicheze.
ReplyDeleteIla KAMALI ni sehemu ya maisha
weka kidogo vuna na ukiuawa BADILAKI
Woga tuu, busara tuu, sheria tuu
Business with more risk has more profit
Maskini wanavuta na wako powa
Akili mkichwaaaaaaaaaa
Risk ama acha
Ila ushauri pia muhimu
This is also known as Multi-Level Marketing Scams. I have seen friends here in the US and even relatives so much into these kinds of businesses and warned them, but because they were too smart in their own eyes to listen to anyone...ended up losing lot's of money. In the 1990's this came to Tanzania and was known as UPATU; if some of you can still remember...there is no making money without production of goods or services....that's all...anything beyond that, is a gambling game...!! Don't participate in these kind of business schemes....!! Wanna read more? http://www.fraudguides.com/home-business-multilevel-marketing.asp You can also google Multi-Level marketing and learn more to just become your own judge..!!! Mdau-USA
ReplyDelete