jarida la Bang! ambalo ni kama Ebony ya bongo toleo la June-July lina Hasheem Thabeet, nyota wa mpira wa kikapu ambaye majuzi kapata ulaji wa NBA na Memphis Grizzlies. Pongezi kwa timu ya jarida hili chini ya da' Imelda Mwamanga ambayo imeweza kuitoa bongo kimasomaso kwa jarida maridhawa ambalo hivi sasa linakubalika afrika mashariki na kati kwa makala safi na taswira zilizoenda shule
mambo yote ya Hasheem uyajuayo na usiyoyajua yamo humo
limeonesha pia kwamba Hasheem naye kwa pamba hajambo
kwa wapenzi wa basketball hili si toleo la kulikosa kwani limetoka wakati muafaka katika historia ya mpira wa kikapu nchini

BANG HADI MAMTONI TUNALIKUBALI,EMELDA ENDELEZA LIBENEKE USICHOKE!!
ReplyDeleteMbona website yao haiwi updated?
ReplyDeletehi Michuzi mambo. Pongezi kwa uongozi wa Bang sasa suali langu ni kwamba je hili toleo la Hasheem ni baada la lile lenye sura ya Imelda kama ndivyo basi tunaomba Bang wahakikishe linafika Moshi tuna kiu sana na Bang tafadhali sana uongozi wa Bang mkisoma hii comment send copies
ReplyDeletebwana Michuzi hivi gazeti la exel limekufa???
ReplyDeletekaka michuzi, sio kwa ubaya... huyu jamaa namwona sana kwenye blog yako ila naishi marekani na niko sana kwenye michezo yao (shabiki) lakini sijaona akitangazwa kokote sio kwenye vipindi wala kwenye habari za hapa na pale, hivi ni kweli jamaa anachezea kikapu au maneno tu? nahisi bado ni hajulikani sana huyu.
ReplyDeleteBravoo! hasheem anarepresent. huyo mdau aliyesema hamjui hasheem,anatakiwa kuwa updated.Majuzi wakati wa NBA pick walitangaza kwa masaa hapa USA kuwa Thabeet mtanzania wa kwanza ktk NBA,alikuwa the second pick of all NBA new stars,wamemsifia kwa hali zote.Let us be positive kwa kumsupport and praise him for the hard work.He deserves it!way to go!
ReplyDelete