Ni yule yule muigizaji machachali wa Movie inayokuja kwa kasi “Baby Powder” itakayozinduliwa jijini Atlanta, Ga mnamo Nov 14 2009 na ambaye imekubalika ni mkamuaji anayetambaa katika matawi ya juu ametoka na video ya single yake iliyotoka hivi karibuni ya Barua kwa Mama ambayo imegeuka kuwa gumzo hapa duniani kwa njia ya mtandao…


yesss si mwingine bali ni Albino Fulani (AF) ambaye siku chache zilizopita aliweka mistari ya singo yake mpya “NAFASI” akishirikiana na Mwana FA aka Binamu na Mr II aka Sugu atakayoizindua BONGO siku ya Xmas. Inasemekana walifanikiwa kurekodi video ya singo hii ambayo nayo itazinduliwa Xmas vilevile.

Kwa wale msiomfahamu AF ni albino anayeishi nchini marekani ambaye anatumia music kuhamasisha dunia haswa nchi za Africa kuwa maalbnio pia ni watu kama wewe na mimi.ili kuondoa mauaji yanayoendelea.....

ENJOY!!!!
Bofya hapa

,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Big Up Babu and everybody who got the video together...I'm impressed!

    Sam.

    ReplyDelete
  2. Wazz up Babu...do ya thang hommie...the whole city is behind u!!!Go hard or go home!!

    ReplyDelete
  3. Albino anatisha.. yani tofauti kabisa na video na wasanii wetu hapa bongo... ujumbe umekaa.. uigizaji mzuri sanaaa... nimelia mara kadhaa...Mzuka mwanangu

    ReplyDelete
  4. Jamaa anakuja juu mnooo. Mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete
  5. Kiswahili nacho...machachali au machachari??

    Mdau Zenji

    ReplyDelete
  6. Babu sikuwezi! hii kitu imetulia! Juu juu juu!!!

    ReplyDelete
  7. hahaha Mdau wa Zenji hana maana KABISA... yani kashindwa kuchangia husu muelekeo mzuri na mfano wa kuigwa toka kwa AF, ameamua kusahihisha kiswahili alafu amemaliza... hahahhahahaha!!

    Zenji toa maoni yenye akili sio kuandika tuu sababu umeazimwa kompyuta.

    Zaidi ya hapo, ujumbe mzuri na nnakuunga mkono AF. Njoo bongo tutashirikiana kwa hali na mali kukomesha mauaji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...