Mtandao wako wa Varsity College Tanzania
unawashukuru wadau wote kwa juhudi zao na ushiriki wao wa kila siku katika kutafuta majibu ya matatizo mengi ya kijamii nchini kupitia mada mbalimbali zianzishwazo na nyinyi wadau katika mtandao huu.
Tunawapongeza wadau wote vile vile kwa jitihada zao za kupost nafasi lukuki za ufadhili wa masomo, ndani na nje ya Tanzania. Hii inaonyesha jinsi gani tunavyowajali wenzetu na nchi yetu kiujumla.
Tunawakaribisha wadau wote wanaojiunga na mtandao huu kila siku. Tunasema karibuni na tuna hakika kuwa pamoja tutaweza. Tuna programs kadhaa mbele yetu zinazolenga kuchangia maendeleo ya elimu nchini. Kwa kuanza, siku chache zijazo tutakuwa na shindano la essay kwa wadau wote wa varsitycolletgetz.
Kutakuwa na zawadi za fedha na vifaa kwa washindi mbalimbali watakaochaguliwa na nyinyi wadau.
Tunawakaribisha wadau wote kujumuika nasi katika mtandao huu wa wasomi Tanzania
Kitogo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...