waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata maelezo katika banda la Tanzania kwenye mkutano wa teknolojia huku Geneva, Uswisi
Mh. Pinda akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la Kenya
Mh. Pinda akipata maelezo ya mtandao wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA) unaoshughulika na taarifa muhimu kuhusu HIV/AIDS


wadau katika banda la Tanzania kwenye maonesho ya teknolojia
mdau katika banda la Tanzania akitoa maelezo kwa wageni wanaotembelea banda hilo





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Pinda mbona umevaa suti? Nilifikiri kauli yako kuhusu mavazi unaitekeleza kwa vitendo!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Huyu PM si ndo juzi tu alisema watu wasivae suti, sababu nchi yetu maskini...! Sasa yeye kavaa nini? Au ndo anahubiri maji kisha yeye mwenyewe anakunywa bia! Viongozi wa Tanzania ni wasanii tu, hakuna mwenye dhamira ya kweli ya kuwakomboa watanzania wanaoishi kwa kubahatisha! Wote wapo kwa maslahi ya matumbo yao na familia zao basi! Lakini kilicho kizuri ni mwisho wa siku wote tutakufa tunarudi kwa muumba mikono mitupu! Mungu ashukuriwe yeye hapokei rushwa wala hana upendeleo!

    ReplyDelete
  3. Katika picha ya pili, ni mheshimiwa Pinda akiweka SAHIHI au akiweka SAINI? Kwani nijuavyo mimi kuweka sahihi ni kuweka kitu pahala pake kutoka pahala ambapo si sahihi...naomba nikosolewe.

    ReplyDelete
  4. Inapendeza sana. Ila mzee wa 'sera ya mavazi' inaelekea alisahau kubeba suti ya kiBongo au bado yuko katika boksi analotaka kujitoa lakini anakwama au anakwamishwa!! ingependeza zaidi!!

    ReplyDelete
  5. i like that tekelinaokujia

    ReplyDelete
  6. Mkuu wa Wilaya ya Nanihii, kama hatuna vazi la kitaifa basi angalau tukubaliane rangi za kusona hasa kunapokuwa na uwakilishi wa Taifa au kitaifa nje ya nchi.
    Kombinesheni ya rangi hizo mbona ni kama bendera ya nchi fulani?

    ReplyDelete
  7. Pinda anatuchezea akili sasa. mbona bado anavaa suti badala ya mashati ya vitenge na batiki? tena ameshindwa na hata hao vijana hapo waliovalia mavazi ya vitenge.

    ReplyDelete
  8. Msameheni waziri mkuu alikosa cha kuhutubia...... nilimuona akihojiwa na ABC kuhusu ALBINO... you can just tell alikuwa hajajiandaa.....alikosa cha kuongea.... alichemsha sana

    ReplyDelete
  9. Huyu Pinda mzushi tu! ameulizwa na mwandishi wa abc news kwa nini hakuna aliyefikishwa mahakamani kwa mauaji ya albino two yrs now?eti anajibu we dont have resources! punguzeni ufisadi resources mnazo, kwanza hayo magari ya kifahari mnayopeana wabunge mnatoa wapi hela ya kuyanunulia? na hayo masafari ya kila siku nje? ungekua una mtoto albino ungeziona resources haraka!

    ReplyDelete
  10. Yaani ina maana Pinda amesahau wale jamaa watatu waliohukumiwa hivi majuzi kifo kwa mauaji ya maalbino? Si angetoa hiyo kama mfano kwamba serikali imeendesha kampeni kali, baadhi ya wahusika wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na kuna wengine tayari wameisha hukumiwa!
    Alishindwa kusema hata hilo jamani?

    ReplyDelete
  11. anon wa Oct 7, 10:29 pm,

    mahojiano ya Pinda na ABC 20/20 yalifanyika kabla ya hukumu ya kesi. mwishoni mwa kipindi cha ABC 20/20 ilielezwa kwamba kuna some progress baada ya watuhumiwa watatu kuhukumiwa kunyongwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...