Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Deo Mtasiwa akifungua rasmi Maonesho ya kutimiza mkiaka 10 ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye viwanja vya hospitali hiyo jijini Dar. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.William Lukuvi (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maonyesho haya kesho tarehe 16 Aprili 2010.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Leonard Lema akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua maonyesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kuadhimisha miaka 10 toka ilipoanzishwa Aprili 2000.
wafanyakazi wa Muhimbili katika sherehe za ufunguzi wa maonesho hayo
Wananchi wakijumuika na wafanyakazi wa Muhimbili katika ufunguzi wa maonyesho
Wananchi wakipata maelezo mbalimbali kwenye maonyesho hayo
Wananchi wakipata vipeperushi kwenye maonyesho
Wananchi wakipata maelezo ya huduma kwa mgonjwa
Wafanyakazi wa Muhimbili wakitoa maelezo kwa wananchi
Kinamama wakipata maelezo ya huduma za MuhimbiliMAONYESHO YA HUDUMA KUADHIMISHA MUHIMBILI DAY
Hospitali ya Taifa Muhimbili inatimiza miaka 10 mwezi Aprili 2010 toka ilipoanzishwa na Sheria ya Bunge Na.5 ya mwaka 2000. Katika kuadhimisha miaka 10, Hospitali imeandaa maonyesho ya huduma yaliyoanza jana tarehe 14 hadi 16 Aprili 2010 ndani ya Hospitali.
Maonyesho haya yanatoa fursa kwa wadau wa hospitali hiyo kuona kwa karibu huduma zinazotolewa na utaratibu unaotumika ili kupata huduma Muhimbili, kujua maendeleo ya hospitali yao, kufahamu huduma mpya zilizoanzishwa pamoja na kutoa maoni na kero zao. Jumla ya Idara 19 za Hospitali ya Taifa Muhimbili zinashiriki maonyesho haya.
Huduma za macho, pua, koo na masikio, meno, kupima sukari, shinikizo la damu, pumu na magonjwa ya matumbo, zitatolewa bure. Elimu kuhusu macho, meno, na uzazi, athari za madini kwenye ngozi, mishipa ya fahamu, na ushauri wa kitaalamu kwa magonjwa mbalimbali inatolewa bure.
Huduma za macho, pua, koo na masikio, meno, kupima sukari, shinikizo la damu, pumu na magonjwa ya matumbo, zitatolewa bure. Elimu kuhusu macho, meno, na uzazi, athari za madini kwenye ngozi, mishipa ya fahamu, na ushauri wa kitaalamu kwa magonjwa mbalimbali inatolewa bure.



mbona wafanyakazi kibao hapo nani kabaki kuangalia wagonjwa?huu mgomo wa sura nyingine,Duuu! Tigo hiyo!!
ReplyDeletemsaada tutani!
ReplyDeletekwani hii hosipitali ni ya 2000???
mimi mbona nimeifahamu tangu nilipozaliwa??
naombeni mnifafanulie.
miaka 10??????????
ReplyDeleteHAPA TUNAZUNGUMZIA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI NA SIYO SIYO SHIRIKA LA AFYA MUHIMBILI.HONGERA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,HONGERA MENEJIMENTI NA WADAU WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KWA MIAKA KUIMI YA MAFANIKIO NDANI YA CHANGAMOTO NYINGI.JENGENI UWEZO KWA VITUO VYA AFYA VYA KATA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM,HOSPITALI ZA WILAYA,MANISPAA NA MKOA ILI MUHIMBILI IBAKIE NA SURA YA KITAIFA NA SIYO HOSPITALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM.HOSPITALI ZA MANISPAA ZIJENGEWE HADHI NA UWEZO WA HOSPITALI ZA MIKOA.MKOA UJENGE HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DAR ES SALAAM.
ReplyDeletevipi mbona hawagusi matatizo ya akili? au bongo hayapo? au hiyo ni idara ya prof maji marefu?
ReplyDeleteUmesema kweli mdau wetu hapo juu.
ReplyDeleteWakati umefika kwa Jiji na manispaa za mkoa wa Dar es salaam kuacha kucheza mdundiko na kusahau huduma muhimu kwa jamii.Huduma mbovu katika zahanati,vituo vya afya na hospitali za Jiji zinaifanya Muhimbili kuwa hospitali ya mkoa wa Dar es salaam.Sasa Jiji lijenge chumba kikubwa cha kuhifadhia maiti[City motuary] pale kwenye kituo cha afya mnazi mmoja ili kitumiwe na wakazi wa Jiji na kupunguza misongamano kwenye hospitali za manispaa na muhimbili na kuongeza ufanisi na kupunguza urasimu.
Mtu asikudanganye pale hospitali bado mambo ni magumu sana. Unabidi uhonge mgonjwa wako apate kitanda. Alafu pale reception ya emergency kuna watu wana nyodo sijawahi kuona. Kuna mama moja anapenda kuvaa sijui ni wigi anafanana na Blandina Nyoni, yaani ni hafai kabisa. Kuna siju tumepata kesi ya emergency ndugu zetu walipata ajali sikuamini yaliyotokea. Kwanza kuna wale jamaa wauguzi wenye uniform za kama khaki walikuwa wamelala usiku wakati mtu kafika pale hoi nusu kifo na anahitaki X-ray ya haraka hawati hata kumpeleka kwenye X-Ray. Jamani ni AIBU kubwa na kufanya maonyesha kama haya ndiyo hasa tunaona watanzania bado tunaweza kuadhimisha hata ujinga!!
ReplyDeleteHongereni sana muhimbili na sasa saidieni mkoa wa Dar es salaam ili uwe na huduma zake kamili na nyiynyi mbakie na masuala ya kitaifa tu.Mkoa wa Dar umelezwa sana na huduma za kitaifa na kusahau kuwekeza kwenye huduma za kimkoa.Hata maktaba za mkoa na manispaa hakuna na hata viwanja vya michezo vya mkoa na manispaa hakuna na pesa nyingi zinakusanywa kwa ajili ya huduma za kijamii.
ReplyDeleteAnkal ni MAONESHO na sio MAONYESHO
ReplyDeleteI see my Dr. Mpoki right there doing what he does best. Big up brother and God bless you. Luv u lots. Lil sis
ReplyDeleteMaonesho na maonyesho vyote vinakubalika.Angalizo ni kwenye matumizi usichanganye maonyesho na maonesho kwenye mada moja.
ReplyDeleteMdau wa Kiswahili
Dar TZ.