
Tanzania imepoteza rasilimali ya madini nyingi na mapato mengi huku umasikini wa wananchi ukiongezeka. Sasa sheria Mpya ya madini inakuja Bungeni tarehe 19 na 20 April 2010 kwa hati ya dharura ambayo wabunge wanatakiwa kujadili na kupitisha siku hiyo hiyo! Tunauliza, kwanini hati ya Dharura bila ushirikishaji na majadiliano ya kutosha?
Ewe Mbunge, Hatima ya Nchi hii sasa ipo mikononi mwako, kataa kuburuzwa kwa masilahi ya wengine, Jadili kwa umakini, pinga usiri, sheria kandamizi na nyonyanji ya nchi. Tanzania tajiri na yenye ustawi inawezekana!
Tangazo Hili linaletwa kwenu na:
Agenda Participation 2000 kwa ushirikiano na
Revenue Watch Institute (RWI)
Ghorofa ya Tano
Ubungo Plaza
Simu: +255 22 2460036/39
Sms + 255 782 550379/ 0758318914
Ghorofa ya Tano
Ubungo Plaza
Simu: +255 22 2460036/39
Sms + 255 782 550379/ 0758318914
Viongozi legelege na wasanii...kumezaa serikali legelege na ya kisanii.Hii Nchi imekosa mwelekeo.Kuna mambo mengi yanayoitaji dharura kama vile mama zetu wanaolazwa chini Odi za wazazi kwenye hospital zetu.Huo mswaada wa madini hautaji dharura yoyote.Kwani madini yanaoza?.Vinginevyo watuambie wanatafuta pesa za uchaguzi.Naungana na wazalendo wa kweli kuukataa uo mswaada kupitishwa kwa hati ya dharura. Please wabunge msitusaliti.
ReplyDeleteJamani watanzania ni lini tutabadilika na kuwa na uchungu na inchi yetu? ni kwa nini tunaburuzwa na watu wachache wenye maslahi binafsi?Hii sheria nina amini tayari watatu wachache viongozi aidha wameishapewa au wameahidiwa fungu fulani na hawa mabepari kama ikipita.Jamani wabunge jitoeni kwenye hii zambi msikubli kuburuzwa na hao mafisadi na wabinafsi ambao familia zao zinaishi kama wapo peponi wakati asilimia kubwa ya watanzania tunaishi katika hali ya umasikini wa kutupwa. Eeeh mungu uko wapiii?
ReplyDeleteMdau
UK
Piga, ua, garagaza Bongo bila usanii haiwezekani. tulipanda magugu, tusitarajie kuvuna mchicha. na tunaandaa shamba kupanda magugu zaidi!!!! shamba linateketea nasi huku tukicheka.
ReplyDeleteAsante wadau kwa kujaribu kuelimisha umma, lakini nguvu ya giza ni kali mno.
Mungu ibariki bongo
Nyie ma-NGOs acheni ubabaishaji. Kila siku ni kuikosoa Serikali tu,bila ku-suggest solutions.
ReplyDeleteMmekalia kula pesa za Wafadhili tu,hatuoni lolote. Kama mko serious kwa nini hamuendi vijijini? Mmekalia kujazana mijini tu.
Mkiambiwa muonyeshe mahesabu yenu tuone mnavyopewa na kutumia pesa za wafadhili mnakuwa wakali kama pilipili. Mnaogopa nini? Acheni ubabaishaji wenu!
Asante sana anoni wa 07:37. Unajua, watu wengi sana, hata wakubwa kwenye nchi, wanalichukulia hili swala la madini kisiasa mno.Hawajui biashara yenyewe ina riski kiasi gani na wala kuwa mrahaba unaolipwa (3% for metals na 5% for stones) ni halali kabisa. Kwanza nchi zingine wala haziweki mrahaba ili kuvutia uwekezaji zaidi.
ReplyDeleteMigodi hainufaishi nchi kupitia mirahaba tu. Kuna kitu kinaitwa LINKAGES with other sectors. Hichi ndicho kinacholeta maendeleo - SIYO MIRAHABA jamani. Kwa mfano, ni kwa nini Tanesco imeshindwa kuuzia umem mgodi wa Geita mpaka ibidi Rolls royce ya Uingereza ije iiuzie huo mgodi umeme kwa bei karibu maradufu ya tariff za Tanesco. Halafu leo Tanesco inalia haina pesa.
Mifano ya missed opportunities ipo mingi lakini wala hatuizungumzii. Tunabakia kulilia mrahaba mrahaba. Nchi imeuzwa nchi imeuzwa. Sijui ni lini tutaamka na kuwa na mtazamo wa kibiashara zaidi.
Mzee wa Ankal naomba kujibu hawa ndugu wawili wa juu kama ifatavyo. Kwanza hakuna ubaishaji wowote kwenye ili issue ya madini hususan huu muswada. Mjumbe anasema eti NGOs ni wa babaishaji na kila siku wanakosao serikali, nafikiri si kweli wala kukosa serikali pale inapofanya makosa si vibaya. Manake ndio role yenyewe ya NGOs, iwe vijini au mjini. Kwa tarifa, NGOs au Raia wema hawa wezi wakakumbatia maovu. Raifiki mzuri ni yule anayekukosao pale onapokosea. Mjumbe anasema eti NGOs hazipo tayari kuota tarifa ya mapato na matumizi, nafikiri sio kweli. Nigependa mjumbe aseme amekwenda kwenye NGO ipi akaulizia mapato na matumizi asipewe? Ripoti za mapato na matumizi ni PUBLIC documents na kisheria zinatatikwa kuwekwa wazi na kutolewa kwa mtu yeyote, kwahiyo nafikiri si sahihi kujaribu kubeza kazi NGOs haswa kwenye jambo nyeti kama ili ya Muswada wa madini? Yeye Mjumbe angefurahi NGOs zikishangilia kwamba serikali imefany mambo mazuri pamoja na mapunguzu yote yaliyo jaa kwenye muswada huu? Mjumbe awache unafiki, kuna mambo mengine, si ya kupongeza. Kimsingi NGOs hawazijapinga muswada , NGOs zinalamika kuhusu utaratibu na mwenendo wa kutengenza huu muswada.
ReplyDeleteNgu mjumbe wa pili anasema tuwe na fikra ya kibiashara zaidi na hakuna haja ya kujikita kwenye Mrahaba kwasabu nchi nyingine zimeshaonodoa. Ndio, lakini kama atafatilia zaidi mjumbe atagundua kwamba kwa Tanzania kitu tunachopata kutoka migodi sana sana ni mrahaba kwasababu makampuni mengi yote yamekuwa yakitangaza hasara. Kwahiyo haya makampuni yalikuwa hayalipi kodi. Pili-Kwenye hizi nchi nyingine kuna regulatory framework kali kiasi kwamba hata bila mrahaba wanapata kodi yao na mchango mkubwa kutoka makampuni ya migodi. Sisi regulatory framework yetu ni mbovu-ndio mana hatupati kiasi cha kutosha. Kwahiyo kulinganisha Tanzania na nchi nyingine kuhusu ili jambo ya mrahaba in kama kulinganisha Kifaru na ngombe. Wanyama hawa wanafanana lakini sio kitu kimoja! Naunga mkono wa CSOs asilimia 10,000 kwa 10,000%
Nawasilisha!