Home
Unlabelled
Bill Clinton ndani ya nyumba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
clinton ni moja ya viongozi wanaomkubali sana jk,toka akiwa waziri wa mambo ya nje,kila interview za clinton akiongelea good leader ship always anamtolea mfano jk,jk piga kazi hela za mo ibrahim zinakusubiri ukistaafu 2015,dola laki moja itakusaidia pale kijijini bagamoyo.
ReplyDeleteAnon wa Tue Jun 22, 06:37:00 PM
ReplyDeleteNafikiri hela za MO Ibrahim is nothing kuliko kukumbukwa na wananchi wako kwa kuwaondoa katika lindi la umasikini. First 5 years of JK has been a total waste of resources and time for our country.
Nafikiri alikuwa ameegemea zaidi katika kuwaridhisha wanamtandao kuliko wananchi waliompatia kura, kitu ambacho kimemfanya JK aonekane kama kawasahau wananchi.
Sifa kubwa ambayo mimi binafsi inanifanya nimkubali JK kama atawapiga chini "Maswahiba wake wenye kuangalia maslahi binafsi" ni kuto uhuru wa watu kuongea wanavyotaka, yaani ni mvumilivu na guts za kubeba lawama.
Ombi langu kwa JK: Ninajua kuwa JK kama President hana tatizo bali wapambe nuksi walimuangusha, so kuanzia Nov 2010, asiangalie nani alifanya nini katika kampeni ili amlipe nini bali ni nani atakuwa balozi wake mzuri, Kitu muhimu katika nafasi zake kumi za wabunge wa kuteuliwa basi aangalie hata watu wasio na vyama ila wana uwezo wa utendaji awateue na kuwapa nafasi za uwaziri ambazo ninamsihi zisizidi 15. Ule mtazamo wa mwenzetu ndiyo umeifikisha nchi hapa ilipo.
Kwa kuanza na kujenga mtandao wa wasomi na vijana katika kampeni yake ni dhahiri baraza lijalo la mawaziri litakuwa na watu wenye moyo wa ujenzi wa nchi si ujenzi wa mabangalaw binafsi.
WACHA KUDANGANYA WATU LINI CLITON ALITOWA HOTUBA JUU YA GOOD LEADERSHIP AKAMTAJA KIKWETE WACHA UONGO WAKO, KAMA NI KWELI EBU TULETEE HOTUBA HIYO, MUONGO MKUBWA WE
ReplyDeletewatanzania tuseme ukweli,jk amefanya mambo mengi sana,sema vyombo vya habari vilishikilia ufisadi tu ndo maana walikuwa hawaonyeshi mazuri ya jk,barabara nyingi mno aamejenga,na bado kuna nyengile zinaendelewa kujengwa,mfano ni barabara ya lindi,arusha namamnga ambayo iko katika hatua za kukamilika,tanga horohoro, ni nyingi mno sema ukifuatilia kwenye wizara ya miundombinu utaona,dar pia amejitahidi kuongeza barabara,kama sekilango,samjoma,kilwa na nyengine ndogondogo,muhimbili tumeona inavyoendelea kubadilika na kupanuka,machinga complex,benki ya wanawake,ambayo ilikuwa ni ndoto ya viongozi walomtangulia,chuo kikuu dodoma, na mambo mengi tu,makusanyo ya kodi ameingia madarakani bilioni mia moja tisini kwa mwezi,now bilioni 370 kwa mwezi,na tukumbuke ni miaka 5 tu hii,tusifananishe na kiongozi alokaa miaka kumi madarakani,nadhani hadi na yeye amalize miaka kumi atakuwa ameipeleka hii nchi mbali tu.
ReplyDeleteNdege wafananao...
ReplyDeleteNaona tunapewa kabakuli kadogo...MHHHHH..mmezidi kutembeza mabakuli makubwa sasa hako kakijaa the rest is on you guys....
ReplyDeleteAnon wa Tues 22 Jun 07:57:00PM, nakuhakikishia kuwa mbali na JK kupata hela za Mo Ibrahim, sisi wananchi tuliosahaulika miaka kwa kuwa tu ni waswahili wa ukanda wa pwani na kusini tutamkumbuka JK kwa kutupatia japo hizo shule za kata watoto wetu nao wakaitwe WATANZANIA badala ya kuitwa watanganyika. Tutamkumbuka kwa kutuletea huduma za afya karibu japo sio rahisi kukidhi mahitaji kwa sababu hakuna watumishi wa kutosha, na hawezi kuzalisha watumishi kama vile unapanda mbegu shambani.
ReplyDeleteMwisho tutamkumbuka kwa kujaribu kuweka uwiano sawa kitu ambacho analaumiwa kwa mgongo wa wanamtandao, hicho kisingizio cha wanamtandao ni danganya toto kinachowauma tunakijua ni uwiano sawa kitu ambacho hamjakizoea, sasa kwa taarifa tu hata uswahilini wasomi wapo!
Na kwa kuongezea JK atachaguliwa tena kwa KISHINDO na sisi waswahili wenziwe mtake msitake, na pesa ya Mo ataipata kilaini kwa sababu ni kiongozi mwadilifu na mchapakazi na asiyetumia mabavu, sio kama wengine wameshindwa kuipata kwa ajili ya mabavu na kujilimbikizia mali!
Mswahili
Uhuru wa habari nayo ni maendeleo pia. Tumeona maovu mengi yakifichuka wakati huu wa utawala wa kikwete. Kusema pia miaka mitano ya JK ni waste of time sidhani kama ni sawa. Sio kweli kwamba maisha yamekuwa magumu zaidi wakati wa utawala huu kuliko wakati wa utawala wakujibinafsishia mali za Umma uliopita. Ni kufunguka tu macho kwa watu walio wengi juu ya seriakali,majukumu yao na nini kinaendelea. Nikatika utawala huu pekee tumeshuhudia viongozi wakuu wakiburutwa mahakamani. Ilikuwa ndoto kwa hata wafanyabiashara tu wenye pesa kidogo au connections na viongozi kuguswa na polisi. Maendeleo si mali peke yake!
ReplyDeleteHuyu mshikaji nadhani kila mwaka anakuja bongo kulikoni ana nyumba ndogo nini au safari za bagamoyo?
ReplyDeleteHhahaa, wabongo bana Hovyooo, yaani hakuna kikubwa mnachowaza ni nyumba ndogo, haaa inawezekan maana kuna tetesi kuwa Monica Lawinski yupo SUA anachukua nondoz labda ndo maana Mzee wa cigar(Clinton) haishi kuja bongo hahahahah! Mdau Mbegu Mji wa Kusoma, UK
ReplyDeletei think clinton is in love with tanzania nazani anaweza nunua nyumba ya kupumzikia !!
ReplyDeleteWANATAKA MAFUTA HAO.....WAMAREKANI NI WAJANJA SANA KWA TAARIFA YENU....WAMEONA NCHI YETU INAMAFUTA KIBAO, BASI WANAANZA MAMBO YAO
ReplyDeleteJK oyeeeeee! nitarudi Tz kwa ajili ya kukupa kura yangu, km mtanzania, nathubutu kutamka kuwa unastahili pongezi kwa uongozi wako, umetuletea maendeleo tofauti na awamu zilizopita! JK wanaosema hawaoni maendeleo uliyoleta labda walitaka uwe unawapa pay check kila mwezi bila kufanya kazi au uwabebe mgongoni! mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
ReplyDeleteHhehee unauliza kwanini kila siku anakuja Bongo??!! Yani ujua kuwa siku si nyingi jama atakuwa na kipande hapo Kigamboni??!!. Hivi ni kweli kuwa JK amejenga barabara kuliko Mkapa??!!.Je mikakati mahimili ya elimu na umasikini?(Mkukuta,Memu, n.k.?
ReplyDeletemdau kwa miaka mitano ya jk amejenga barabara nyingi tu,sema media hazipi umuhimu habari hizo,na kama jk kipindi cha pili atafanya same,atakuwa amejenga barabara nyingi kuliko mkapa,tenaa zile zinazopita kwa masikini kabisa.kila kiongozi nchi hii anamazuri yake ya kukumbukwa,nyerere katuletea uhuru na mshikamano,mwinyi ameubadilisha uchumi wa tz kwa muda mfupi mno,maana aliingia madarakani nchi imeoza,watu wamekata tamaa kwa mlo wa aina moja mwaka mzima,sukari ilikuwa anasa,kuja mzee ben mapato yakaenda juu,matumaini ya maendeleo yakazidi na watz wakashtuka kusoma,jk ameingia uhuru wa ghali ya juu ukaja,hali ikabadilika kuanzia bungeni,vyombo vya habari hadi vyama vya siasa,now watz wanaeza kujua uozo wote wa serikali yao,bila shida.mapato pia maradufu.nadhani kila kiongozi ana ubaya na uzuri wake.sema kuna watu wao ni negative tu ka jk,sijui tatizo nini
ReplyDeletemswahili umeniacha hoi kweli,sema hata wakulima hawatamsahau jk,tumeona korosho ilivyopanda bei ttangu jk achukue nchi,atlist now wakulima wa korosho nao wanaheshimika.
ReplyDeletewatz bwana yani mnataka maendeleo mpk mpeleke chombo mwezin km NASA..?hakuna kipindi ambacho watz wengi wamesoma kama kipindi cha kikwete,isipokuwa kuna wa2 wana sera za kupinga kila kitu sasa kama hauna akili ya kufiria unakuwa mmoja wao...lazima watu wajue maendeleo hayapai hakuna nchi iliyoendea katika kila ktu kwa miaka mitano sasa kumlaumu kikkwete ni ujinga uliopitiliza amefanya mambo makubwa katika nchi na ataendelea kuwa raisi mtake msitake...kwa sababu wananchi wanamkubali
ReplyDeleteWatanzania tuache majungu, hivi kuna ubaya gani marekani ikiwekeza tanzania?? Si ndio maendeleo tunayoyataka hayo au tulikuwa tunatakaje?? naona ni kweli watu wanataka kulipwa bila kufanya kazi.
ReplyDeleteHongera JK kwa nguvu mpya zaidi, kasi mpya zaidi na nini vile!!! kama hujui hii ndio kauli mbiu ya JK kueelekea uchaguzi 2010
Acheni kunifix mimi jamani.Hii picha ni baadhi ya popularity za Rais na Wamarekani.Ila Clinton was a serious president siyo kama Bush.
ReplyDeleteKuna mambo ambayo hata kama tusingekuwa na Rais bado yangefanyika. Kuna miradi ambayo ilishapangwa tangu enzi za Mkapa na ilimaliziwa tuu enzi za JK. Kuna mafanikio machache sana na itakuwa ni unafiki bila kutaja matatizo yaliyozailiwa enzi za JK. Baadhi ya mambo ni kama ifuatayo
(1) serikali imeshindwa kusimamia sera za uchumi. Mfumuko wa Bei umeongezeka hadi kufikia tarakimu mbili. Idara ya Takwimu inafahamu pia kuwa takwimu zimekuwa zikipikwa na Ikulu sasa na takwimu halisi kuwekwa kapuni,
(2) Mapato hayajaongezeka kama wengi wanavyosema. Mapato yameongezeka katika "nominal term" na siyo katika "real term". Nitamwomba Kamau au Mashaka aelezee nina maana gani. Serikali imekuwa katika wakati mgumu sana hata kulipa mishahara ya watumishi wake halafu mnasema mapato yameongezeka???,
(3)Serikali imeshindwa kusimamia matumizi mabaya ya fedha za umma. Viongozi wakuu serikalini wamekuwa namba moja kuzurura nje ya nchi bila sababu zenye manufaa kwa taifa. Safari hizi zimekuwa zikigharimu hadi Sh. bilioni tano kwa safari.Mawaziri kama wafanyakazi wa mashirika ya ndege...kila siku angani,...hii ni nchi pekee afrika ambayo viongozi wake wanazurura kuliko wengine;Ununuzi wa magari ya Kifahari ni eneo lingine ambalo linahitaji marekebisho.
(4) watumishi wa Umma wamepoteza sifa na maadili yao. Kuvuja kwa siri serikalini, utendaji mbovu, kukosa motisha ni baadhi ya mambo tu ambayo serikali imeshindwa kusimamia,
(5) siasa imetawala mipango ya maendeleo. Nchi imekuwa bize na propaganda za siasa kama enzi za ujamaa na kushindwa kuwaweka wananchi katika mambo ya maendeleo.Serikali ya awamu hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuua mashirika ya Umma kwa kuweka watawala wasio na sifa ambao ni rafiki wa jamaa zao. ATCL na Daudi Mattaka ni mfano tu wa utendaji mbovu katika eneo hili.
(6) TRA imeshindwa kuwa taasisi bunifu kwa mapatao mapya. Serikali imeendelea kuwabebesha mzigo wa kodi wafanyakazi, huku juhudi za kukusanya kodi katika sekta binafsi zikiwa duni.
(7) serikali imekuwa ya kishabiki na sera zimekuwa zikiibuliwa kutokana na matukio. Mfanio hii Kilimo Kwanza ni usanii fulani wa kishabiki tuu. hakuna mkakati wa kisera hasa katika hili. Hii ilikuwa muafaka ulioanzia kwa wafanyabiashara kisha ukachomekwa serikalini. Serikali haiwezi kufanya kazi kwa ushabiki au matukio, Washauri wa Rais aidha wameshindwa kumshauri ipasavyo Rais au rais hawasikilizi washauri wake,
Kaka Michuzi ni lazima wananchi na Rais mwenyewe na serikali waelewe kuwa kuna tatizo la maendeleo la serikali ya awamu ya nne imekuwa dhaifu kuliko serikali zote zilizopita. Washabiki wanaweza kukataa maoni yangu ila ukweli uko wazi. Ni vyema Rais akafanya tafakari ya maoni ya wananchi na kuangalia namna ya kurekebisha kasoro na kuipeleka Tanzania mbele.
Ni vizuri pia Ikulu ikasoma na kutafakari kwa makini maoni yanayowekwa katika blogu hizi za jamii kwa kuwa zinaelezea fikra halisi za mtanzania wa kawaida.
Clinton hawezi kununua nyumba Tanzania, si raia, zijue sheria za nchi yako, blockhead!
ReplyDelete