MWALIMU J K NYERERE (1922 – 1999)
This is the Nyerere legacy I hold close to my heart when I see today's Tanzania: Nyerere - A Leader Who Dared! (Nyerere - Kiongozi aliye thubutu).
Whatever may be your view of his legacy, Nyerere was the author of his story; and to the benefit of many across Africa and the world at large, he dared to do it his way. Nyerere challenges leaders of today to dare to be the authors of their story and to dream and act in support of a vision greater than the moment, even when faced with the greatest odds and most compelling adversity…
Pengine bila kiongozi kama Nyerere kusingekuwa na Mandela wala Afrika Kusini ilio huru na ndiyo maana Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza aliyo itembelea Mandela baada ya kutoka jela. Lazima tukubali na kujivunia kuwa na kiongozi shupavu na mwenye muono wa namna hii. Hususani mwaka huu wa Kombe la Dunia, dunia ilipo shuhudia manufaa halisia ya ukombozi wa Taifa kubwa kama Afrika Kusini na kuweza kulileta Kombe hilo ndani ya bara letu. Tulistahili tumpe sifa Mwalimu kwani ndie kiongozi pekee aliye thubutu kusimamia mapambano dhidi ya Mabeberu bila kikomo. Si Mmarekani, si Mchina, si Mholanzi bali ni Taifa changa la Tanzania lililo kuwa mstari wa mbele likiongozwa na Mwalimu J K Nyerere - Kiongozi aliye thubutu.
Pengine bila kiongzi kama Nyerere tusingekuwa na taifa lenye mshikamano na lenye kuchukia utengano kama ilivyo sasa Tanzania. Siwezi fikiri ni wangapi walio na ujasiri wa kupangua mifumo ya utawala wa kikabila na wa kikoloni ili waweza kusimamia mwono wao wa Taifa moja linalo takiwa. Nyerere alidhubutu kufanya hivi. Hakutumia muda wake mwingi kulalamika na kushangaa mapungufu. Bali alithubutu kupangua na kupanga upya mambo jinsi alivyo ona yeye inafaa bila kujali maneno na minong'ono ya wanafiki wachache na wasio jali maslai ya wengi au kuwa na muono wa mbali. Hii ndio ilikua tabia yake mzee wetu Mwalimu J K Nyerere - kiongozi aliye thubutu.
Kama Baba wa Taifa alithubutu kufanya makubwa kama haya mbele ya upinzani mzito na vitisho ndani na nje ya nchi, je wewe Mwana wa Taifa unathubutu katika lipi?
C V Magavilla
www.magavilla.com

Magavilla,
ReplyDeleteNi vema kumpenda mtu na kumsifia kama unavyofanya. Lakini jambo moja muhimu ni kuhakikisha kuwa kila unachoandika hadharani kiko sawa. Kuna watu wengine tukishakumbana na kosa la wazi tunashindwa hata kuendelea kusoma. Ndivyo ilivyotokea leo kwenye hiki ulichoandika.
Sina hakika na madai yako kuhusu Afrika Kusini na Mandela lakini nikusahihishe tu kwamba Mzee Madiba Mandela hakutembelea Tanzania kama nchi ya kwanza baada ya kutoka gerezani. Ni kweli ilitangazwa hivyo kwanza, lakini alibadili uamuzi na kuamua kuzuru Zambia kwenye makao makuu ya ANC kwanza, na kisha ndiyo akaja Tanzania. Nenda kasome magazeti maktaba utaona hii kitu.
Mdau,
Unyamwezini Majuu.
sikliza kwa upande wako sawa lkn kwa sisi wenye kujuwa nyerere ni aduwi wetu ametuharibia kila kitu chetu
ReplyDeleteAhsante sana Bw. Magavilla,
ReplyDeleteInabidi watanzania tuamke, kwa kweli.
Tanzania yangu, nchi yangu, nchi yetu. Moyo unaniuma kwa kweli nikiona kule tunakoelekea.
Kweli kama mdau ulivyosema, kazi kubwa, ambayo kama wewe nakubali kuwa huu ndio mhimili wetu. Alitujengea na kutuachia umoja, Tanzania hatujui udini wala ukabila wote ni ndugu.
Kinachoniumiza hivi sasa ni utabaka unaochipukia kwa kasi kubwa sana, na hii ni kati ya matajiri na walala hoi. Viongozi wa kisiasa wanapiga kelele juu ya dini na makabila. Lakini tatizo letu hivi sasa ni chimbuko la matabaka.
Dini/Kabila mpya ya hao watu ni pesa.
Tunaendekeza sana sera za kibepari.
Tanzania ni taifa lililokuwa limejengwa kwa misingi ya ujamaa, mpaka mwanzoni mwa miaka ya tisini ndipo sera zilianza kubadilika. Ni kweli kwamba baadhi ya madadiliko hayo yalikuwa ni muhimu kwa taifa letu kuweza kusonga mbele na kupata maendeleo. Lakini mabadiliko hayo yangeleta maendeleo ya ukweli, maendeleo ya taifa kama maslahi ya watanzania yangekuwa yanapewa kipau mbele. Inasikitisha kuona kwamba makampuni mengi(karibu yote) yameuzwa kwa wageni, tena kwa bei mbovu(bei ya kutupa), Raslimali zetu zinagawiwa kwa bei ya sawa na bure. Mfano mwepesi wa jinsi ya mikataba ya madini tuwaangalie wenzetu wa Botswana, hawa ni majirani zetu tu hapo nyumbani. Hebu tuangale Jamaa zetu wa hapo uarabuni na jinsi mafuta yao yalivyowaletea maendeleo. Sisi pamoja na madini yote (dhahabu, almasi, metali za chuma na mengineyo mengi) bado tunalia umaskini.
Mabadiliko ni muhimu sana.
Tanzania itajengwa na sisi wenyewe watanzania, na si wageni.
Mungu amlaze mahari pema peponi Baba wa Taifa.
The one and only JK.
Mungu Ibariki Tanzania
Usisahau siasa ya ujamaa na kujitegemea haukuleta maendeleo ndio maana nchi ikarudishwa kwenye mikopo ya IMF na World bank.Je ni legacy gani hiyo ya kuiachia nchi? Na hao ndio wameibadilisha nchi hii katika mfumo wa sasa kupitia masharti ya madeni. Chini ya nyerere tulikuwa tunafata mfumo sawa na wachina. Angalia wachina walipo na angalia sisi tulipo?
ReplyDeleteNi kweli Mwl Nyerere alikuwa ni kiongozi ambaye nchi yetu itachukuwa miaka mingi kuja kupata kama yeye.
ReplyDeleteWe anoy wa kwanza ni kweli Tz ilikuwa moja ya nchi za mwanzo kutembelewa na Mzee Mandela alipotoka Jela sioni sababu ya wewe kubisha ovyo.
Nafikliri tungeanza kuandaa vijana wetu kama Mwalimu kusudi waje kuwa viongozi wa kesho.
Mdau.
Some Tanzanians have no clue how lucky and blessed they have been. To view Mwalimu Nyerere as an enemy just because he didn't usher the fangs of capitalism into Tanzania at earlier point and time, is fail to see the greater
ReplyDeletepicture.
His legacy will live on and Tanzanians should be proud that he infused national pride into the hearts and minds of millions of Tanzanians.
The South African apartheid regime was so scared stiff of Mw. Nyerere's involvement in the liberation movements in South Africa, Angola, Mozambique, Zimbabwe and even Namibia.
Majority of the Tanzanians were so united, patriotic, well informed and fearless that an enemy from without (spies) found it so difficult to penetrate the nation and cause damage.
There is no question about, Mw. Nyerere advocated for their freedom and independence, not just in words but in his actions and direct support for those involved. And it changed the political tides in those respective nations.
Let's give credit where it's due and hold our heads high given the strong foundation that were established by Mw. Nyerere. A legacy that will last throughout the existence of the next six to twelve generations.
On the dark side of capitalism, look no further, DRC, Angola, Mozambique, Sudan and Chad. Who owns their mineral fields and most of the nation's other natural resoucres? Foreign corporations, not the national givernments or the citizenry.
The Usambara individual, should understand that, there is no point in having modern cities built at the expense of meaningful development around the nation.
With all due respect to some of our neighbours, why would we want to have the great divide as it exists today in so many parts of Nairobi?
Visit some of the posh estates in the city, then head to Kibera, Kwangare, Eastlands, Mathare and regions of the neighbouring slums.
Let there be progress in Tanzania, but for all the citizenry and not just in certain enclaves or for particualr individuals.
I would really hate to begin seeing second class citizens and third class citizens of Tanzania just because of economic disperities.
Give credit wwhere its due. To Mw. Nyerere.