Mgombea urais wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa akihitimisha mikutano yake ya kampeni jijini Mbeya leo. Chini ni wafuasi wa chama hicho na bango lao
Aliyekuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Goodluck Haule, akimakabidhi moja ya mavazi ya chama hicho mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kukihama na kujiunga na Chadema.
wafuasi wa CHADEMA katika mkutano wa mwisho wa kampeni wa mgombea urais wa chama hicho Dk. Wilbroad Slaa huko Mbeya leo
Nyomi ya CHADEMA katika mkutano huo
Dk. Slaa akihutubia umati wa wafuasi wa CHADEMA
Dr. Slaa akiondoka eneo la mkutano baada ya kuhutubia huko mbeya leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Michuzi ulivyotuhabarisha kuhusu matukio ya mwisho wa kampeni za urais ndio kaida sahihi ya uhabarishaji na ndio tuliyokuwa tukiitarijia katika kipindi kizima cha kampeni. Lakini uzalendo ulikushinda ukashindwa kuzui kuonesha ukereketwa wako. Ukawa unatulisha pumba za kijani tuuuu. Mimi niliacha kabisa kufungua globu yako. Leo umeonesha kuwa kazi unaijua ila tu hukupenda kufanya hivyo. Mdogo wako ni mwanablogu aliyekomaa- yeye aliendelea kubandika matukio kama alivyoyapata na kuacha mamuzi kwa msomaji. Kwa vile kampeni zimekwisha nami ninarejea kuendeleza libeneke kama kawa. Sasa tujadili jinsi dola linavyoendeshwa na faida au hasara katika maisha yetu ya kila siku.

    ReplyDelete
  2. Nayaona mabadiliko yakija Tanzania. Kama si 2010 basi 2015. Mungu atue uzima tuione Tanzania ikistawi.

    Uongozi ni muhimu sana kwa maendeleo. Rwanda imebadilika sana katika miaka 15 iliyopita. Yote hiyo ni kwa uongozi madhubuti wa Kagame.

    Kama tuna ardhi, watu na siasa safi basi nini kimekosekana katika miaka 50 ya uhuru wetu? Jibu: Uongozi bora.

    ReplyDelete
  3. Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha!! kumbukeni kuna mungu.

    ReplyDelete
  4. I hope he wins...good luck and surprise the whole world...

    ReplyDelete
  5. kwa nini ulitufanya vile mcihuzi? why? ninauchungu sana moyo naulivyo tugeuka
    anyway hongera sasa umerudi zizini leo hata nimesisimka tulikuwa hatujui pa kupata habari sahihi siku zote uchaguzi ulipokuwa ukikalibia tulikutegemea sana
    tunaomba uwe fair unapotoa matokeo plz
    sisi huku ng'mbo tunakutegemea wewe
    tupe matokeo kadri yanavyo tangazwa na hapo tutakuwa tumekusamee

    ReplyDelete
  6. Du kweli leo uchaguzi yaani mpaka Michuzi umeweka wazi libeneke la CHADEMA NA CUF badala ya kulalia upande wa CCM? Nakupongeza kwa hilo. Ukifanya vyema nakupongeza ukileta za kuleta nakupa ukweli wako kama kawa

    ReplyDelete
  7. Kuna mchanganyiko wa unafiki na ukada!! Ni kama gazeti moja hapa nchini lililojitokeza mwishoni kuelezea kuwa ni mbadala wa Uhuru!! Likishitakiwa kwa utapeli liko tayari kulipa fidia!!

    ReplyDelete
  8. hongera michuzi,hata kama ulikuwa biased...watu walikuonakule mtwara upo ndani ya ''PRESS KIKWETE'' ...hukusoma alama za nyakati hata kama ulikuwa unakataa..nimerudi tena blogin kuendeleza libeneke..ila ungeendelea na ukijani wako usingenona kamwe huku ...nitabp bp kuona unaendeleza vipi tz ya leo

    ReplyDelete
  9. Michuzi , me sikupendezwa na Unazi wako wa Kijani na Njano, nika comment ukanibania. Nilikuja kujua baadae kuwa ww ni kada wa Thithiemu, nikaona nisikulaumu. Hongera kwa kurudi kwa wanajamii sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...