TAWI LA CCM-MAREKANI. Hili tawi la CCM-MAREKANI ni la watu wa Houston tuu. Kwasababu sikujua hata kuwa kunatawi la CCM hapa USA mpaka juzi mshikaji wangu akaniambia anaenda kwenye mkutano. Cha kushangaza hakuna watu wengine wa state zingine wanao fahamu kuhusu hili tawi.

Sasa cha kushanganza nikauliza kuhusu viongozi, eti viongozi wote pia nao wanakaa HOUSTON, halafu washikaji. SASA SWALI LANGU NI HILI HIKI NI CHAMA CHA CCM-HOUSTON AU MAREKANI ZIMA? Kwasababu huwezi kusema TAWI LA CCM-MAREKANI kama wanachama wengi wa CCM-USA hawajui hata kama kuna TAWI.

Sijawahi ona sehemu yoyote kuna tangazo limewekwa hata kusema kuna mkutano au tunachangua viongozi. Mimi ni mwanachama wa CCM ila sitambui kiongozi wa CCM-MAREKANI hata mmoja na siwajui. Na najua watu wengine pia watakubali hili swala.

Kama hicho chama kweli kina NIA ya kujumuisha wanachama wa CCM-MAREKANI kwanini tusiwe na viongozi state zingine pia? Huu mimi naita ubinafsi wa madaraka. Naomba wote tushirikiane sio kuwa na ubinafsi wa madaraka na kuweka washikaji wote wawe viongozi.

CCM JUU JUU ZAIDI

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI KIDUMU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Achana na mambo ya siasa kaka! Piga boksi tafuta hela yako. Porojo hazitakuleteza maendeleao hata siku moja.

    ReplyDelete
  2. NDUGU MDAU,HONGERA SA KWA DUKUDUKULO HILO,NATOA CHANGAMOTO KWAKO NA WENZAKO WA AINA YAKO KUANZISHA MASHINA STATES MBALIMBALI MLIPO NA KUCHAGUA VIONGOZI KWA MUJIBU WA KATIBA HALAFU MASHINA HAYO VIONGOZIWE MKUTANE KAMA HALMASHAURI KUU YA CCM MAREKANI[TAWI]KWA UKUBWA WA NCHI MLIPO MNA NAFASI YA KUWA TAWI LENYE KINGUVU MKIWA NA UMOJA NA KUFUATA NA KUHESHIMU KATIBA.SISI HAPA UK TUKO KTK MFUMO HUO NA TUKO TAYARI MKITUALIKA KUJA KUSAIDIA KUTOA SEMINA NA MPANUKO WENU..TUMPONGEZE SANA JAKAYA KIKWETE [M/KITI WA CHAMA TAIFA TZ]KWA KUWAPA WATANZANIA JUKWAA LA KISIASA PALE WALIPO NJE YA NCHI ILI TAIFA LIWATAMBUE NA KUVUA VIONGOZI SHUPAVU WA KULIKWAMUA TAIFA LETU....NAOMBA KUTOA HOJA.
    ALLAN KALINGA.
    KATIBU WA UCHUMI NA FEDHA
    CCM TAWI U.K.

    ReplyDelete
  3. subiri FBI waambiwe wanaendesha mambo ya kisiasa ndani houston bila usajili...

    ReplyDelete
  4. Wabongo mlio nje sasa mnaanza kututia haibu. Haya mambo ni kizamani.... Sana sana huwa tunayasikia UK lakini si Marekani.... Hawa ni watu wawili watatu watoto wa vigogo ndo wanaungana na kufungua matawi.... ACHENI KUTIA AIBU TANZANIAN COMMUNITY.... HAPA MAREKANI HUO UMOJA HATUUJUI

    ReplyDelete
  5. wewe mshamba sana unatakatukujuwe kuwa uko usa unadhani kuishi usa ni deal tena mambo yate yako hapa dar usijidanganye na ndio mwanzo wakurukwa na akili huko unaanza kuzungumzia upuuzi wa ccm, maisha yamekushinda rudi kwenu au uliondoka hapa umedhulumu wewe, tadhali mada kama hizi za kiupuuzi usituandikie hapa mtumie dada yako asome hapa kwenye ukumbi tunataka mada zenye faida kwa jamii

    sio upuuzi wako wewe mambo kama hayo ilikuwa aandike mkaazi wa hapa nchini sio wewe huko mshamba mkubwa wewe, kama huna huoni lakufanya na kazi za hata kuuza pizza hupati hapo usa rudi kwenu ujeutangaze ccm

    ila usitopotezee mda kwa mada zako za kijinga, tunapoona mada huwa tunaisoma kujuwa kuwa niyaamaana kumbe utumbo mtupu, jinga moja

    ReplyDelete
  6. Ndugu Mdau ulieleta maoni yako hapa ninakushauri uingie hapa www.ccmmarekani.blogspot.com utapata contanct information za tawi hilo na pia kuna e-mail address yao pale ccmmarekani@gmail.com Mimi ni mwanachama na pia ninawasiliana na uongozi kupitia contact hizo na page ya facebook ya ccmmarekani.
    CCM Marekani iko imara na wazi kwa kila mtu.

    ReplyDelete
  7. Hawa jamaa njaa tupu, wote walio kwenye hiki chama. Ni watu baadhi wanao tafuta majina kwa nguvu wakizani wakifika bongo watapewa madaraka, kama yule demu alifikili atapewa vitimaalum hehehhehe amedoda. Rudi upige box na wanageria wako wakusubiri huku wewe dada.

    ReplyDelete
  8. ANONYMOUS WA Thu Oct 14, 01:44:00 PM
    Inaelekea wewe ni mmoja wa hao viongozi KUBUMBA wa hicho soo called chama huko Houston. Mbona hasira nyingi sana. Mdau kaleta mada hapa na hii mada mimi naona ni ya maana kama kweli hili tawi lipo kwanini watu wote wasijulishwe inakuwa ni tawi la watu baadhi tuu wanaona taka UMAARUFU. Sasa mpaka kutukana kote huko kumekusaidia nini wewe. Grow up bwana matusi hayajengi yanabomoa.

    Mudau uliyeleta mada hii asante sana mimi umenifumbua macho leo ndio najua kuna TAWI LA CCM MAREKANI. SASA VIONGOZI WAKE NI NANI? NA NANI KAWACHANGUA? NA KWA SHERIA IPI? Tupeni hizo data nyie viongozi ambao hakuna hata mtu anaye watambua.

    ReplyDelete
  9. Wabeba maboxi bwana njaa tupu, hawa jamaa walio kwenye hiki chama mimi nawafahamu. Wako kama watu 9 tuu including viongozi wao wanafika hiyo 9. Sasa cha ajabu mkutano wao hata mmoja hutaweza sikia umetangwa hata hapa HOUSTON hapan ni wao hao 9 peke yao ndio wanaambiana basi. SASA HILI NI TAWI AU MTAJI WA WATU BAADHI WENYE NJAA YA MADARAKA NA KUTAKA UMARUFUU KUPITIA CHAMA.

    ReplyDelete
  10. Jamani mimi naanzisha TAWI LA CHADEMA MAREKANI. Whoever wants to join me.
    KIDUMU CHAMA CHA WASOMI KIDUMUUU
    ADUMU RAISI MTARAJIWA 2015 ADUMU
    CHADEMA OYE OYEEEE

    ReplyDelete
  11. ANONYMOUS Thu Oct 14, 02:31:00 PM
    Sasa mbona nimeangalia hiyo blog kwanza ni kama mwenyekiti kasimamishwa mhhhh sasa nani kiongozi hakuna hata picha za viongozi. Hiki chama kinatia mashaka mbona. Kwenye hiyo blog sioni hata wanasema wanafanya nini huku USA naona picha za kikwete tuu zimebandikwa kila corner. MHHHH THIS IS VERY FISHYYYY JAMANI. Sasa huyo kiongozi wamemusimamisha wakinani na kwa sheria ipi? na yeye amekubali kusimamishwa au bado kangangania? Hili jambo naomba liwekwe JF ili watu tujadili.

    ReplyDelete
  12. UK ndio mfano wa kuingwa bwana.

    ReplyDelete
  13. Jinsi hilo tawi lilivyo na majungu na wewe umejitia kimbelembele kulopoka kwenye Blog, expect kuvuliwa uwanachama and may be uraia.

    Tawi lipo lakini limegawanyika sehemu mbili, kuna CCM asili na CCM mamruki... sasa wewe chagua kama wewe asilia au mamruki. Asili wanatokea Dodoma na upande wa fukwe za bahari ya hindi... Mamluki ni walizaliwa mikoani.


    Mwisho ushauri wa Bure, soma pata degree then achana na box pata ajira bora. Bilakusahau karatasi.... CCM hailipi rent hapa, wala car note. sasa wewe leta ujanja ujanja wako uone cha mtema kuni...

    Mdau wa Humble, Houston

    ReplyDelete
  14. Wewe uliyesema kuanzisha tawi la chadema marekani nakuunga mkono. Watu wengi walio hapa wenye akili,hekima na wasomi watajiunga na wewe. Ila hawa jamaa wa ccm marekani wakiona hii kitu kwa michuzi utatafutwa sana. Huu ni mtaji kwao wenzako sasa wewe unataka waharibia mtaji wao.

    ReplyDelete
  15. Hii CCM Marekani ni upuuzi mtupu. Hivi sasa kuna malumbano kibao hapo houston.

    Upande mmoja yuko jamaa anaitwa Michael Ndejembi amabaye anataka kuendesha tawi la cc marekani kama mali yake binafsi. Huyu jamaa hajafanya lolote kuendeleza tawi tangu lifunguliwe. Hasikilizi maoni ya wengine na mpaka leo vikao vya tawi vinafanyika kwenye apatment yake na inaelekea yeye ndio aliye bandika hiyo comment hapo juu yenye blog na email za tawi.

    Upande wa pili kuna Mzee moja anaitwa Isak Kitogo. Huyu pamoja na Zainabu Janguo na Miraji Malewa walijiengua kwenye chama na kumfuta uongozi dejembi. Hivi sasa wanadai chombo anachoendesha dejembi si ccm halali.

    Pia kuna mzee anaitwa juma maswanya. Huyu mzee ndio anajiita mlezi wa tawi lakini ameshindwa kutatua mgogoro kati ya dejembi na kitogo. Anashindwa juchagua upande mmoja sababu uwa hapendi lawama.

    Alafu kuna mtu anaitwa seki adadi. Nasikia nae ameanzisha tawi la tatu la ccm marekani.

    CHADEMA WA HOUSTON NAO WAMEAMKA WAKIONGOZWA NA BWANA ONESMO FUE. Wao kazi yao kila kukikucha ni kumtetea slaa.

    KAMA VIONGOZI WA CCM TANZANIA MNASOMA HUU UJUMBE WAAMBIENI DEJEMBI NA KITOGO WAACHE KUWATIA AIBU HUKU MAREKANI.

    ReplyDelete
  16. Wewe mdau wa Humble Houston
    Hakuna cha kuogopa mtu hapa kwani hao ndio wakinani mpaka waongopwe kwanza wanafany nini cha maana hapa Marekani? Wamesoma au ni njaa tuu? Sasa mimi na wenzangu watano tunaandika barua kwa mama balozi hapo Washington DC kuping hawa viongozi walio jichangua wenyewe kumuambia kwamba tunataka uchanguzi wingine ufanyike tena Watanzania wa state nyingine nao waweze kuchangua viongozi wake. Sasa tutaona hao viongozi waliopo sasa kama hata watambulia vote moja.

    ReplyDelete
  17. Hivi leo ni holiday USA naona wabeba mabox full mtandaoni. Hehehe kazi kweli kweli. Sasa hiyo CCM MAREKANI ndio nini jamani? naomba mutujibu na sisi wapingwa vumbi huku tujue.

    ReplyDelete
  18. Aliyetela hii mada nakuunga mkono sana tuu tena. Hawa jamaa wanataka kuanza kutapeli watu tuu hakuna lingine hapa. Hakuna mtoto mdogo au mjinga hapa ishieni huko huko Houston mliko zoea kuibiana. Hakuna cha ccm marekani wala nini. Watu tuna piga box letu that's it. Naomba msitupotezee muda na ujinga wenu eti ccm ccm so what?

    ReplyDelete
  19. Nahisi John Mashaka ameleta hii mada anataka apewe uongozi jamani. Haya jamani mpeni basi.

    ReplyDelete
  20. Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

    ReplyDelete
  21. Jamani hata mimi nashangaa mikutano ya chama inafanyiwa kwenye apt ya mtu.kazi kweli kweli. Inaimanisha kwamba hakuna wanachama wengi zaidi ndio maana haitajiki sehemu kubwa

    ReplyDelete
  22. Asante sana uliyeleta hii mada na huyo aliyepost hii blog. Ninapeleka kwa wahusika ili watupe jibu na kutumalizia hizi issue. Stay toon. Nchii hii ukiishi hutakiwi kuanzisha vyama vya siasa unless umepewa ruhusa na wauu na kujua hicho sio chama cha ugaidi. Sasa nariport hii ili tuwajue hawa watu wanakibali cha kuanzisha tawil la chama huku? Kama wanapenda chama wangekaa huko tanzania. Na tawi la nini kwa kujifichaficha ...we will see...

    Mpenda nchi yangu mtanzania halisi...NIliko hapa kila nimwonaye namtreat kama mtanzania mwenzangu lakini mambo ya kubeba vyama na kuvuka mipaka nanyo tuone yatawafikisha wapi..Wote mtadeportiwa...

    ReplyDelete
  23. COUNT DOWN TO GET MY USA PASSPORT IS 3YRS,THE VERY DAY I WILL BURN MY TZ PASSPORT.HOW'S THAT

    ReplyDelete
  24. CHADEMA KIKO WAPI MAREKANI NA WENGINE TUJIUNGE?

    ReplyDelete
  25. huu kweli ni upuuzi gani tena umeenza huku peponi?? nilizani mambo ya CCM waachiwe wapiga box wa UK... sisi huku tumefika na kwa sheria ya nchi yetu hii tukufu ya Marekani hatutaku kabisa vyama vyenye siasa ya ujamaa ( socialist party ) naona itabidi tuanze kuwaripoti kwa wanausalama wetu maana huu ni upuuzi wa hali ya juu na hatutaki ujinga huku!!

    ReplyDelete
  26. Sheria za marekani haziruhusu mtu yoyote kujiunga na kujihusisha kwa aina yoyote ile na chama chochote chenye siasa za kijamaa kwa hiyo ole wako wewe mtanzania utakayejiunga na CCM au kujihusicha kwa namna yoyote ile maana naona umefika wakati wakuanza kuwapunguza humu nchini!! Watu wamezizi sasa naona wengine wameshaanza kujamba cheche na kujiunga na CCM. Kama unataka amia UK kwa walalahoi... hii land of opportunity kama bado unapiga box na una makaratasi kalaghabao !!! ila pls pls NO CCM hapa....

    ReplyDelete
  27. Na mie naanzisha tawi la TLP Marekani!!!!

    ReplyDelete
  28. Mukifungua tawi mimi nitawachongea kwa kuendesha siasa bila ya kibali, kuchangisha michango bila ya kufuata taratibu.

    Ili tukae kwa amani musituletee siasa zenu hapa.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  29. Thanks for bringing up the issue to our attention. This is very simple issue that can be solved in many ways than one. Further, there are so many solutions to addressing (fixing) the issue as well as seeking alternative CCM affliates registered on the east coast and the west coast. Let the Houston CCM people have their Texan branch, while concerned Tanzania should be allowed to establish other branches around North America. There is no monopoly or so called exclusivity in that regard. Just make sure you get over twenty members or more from your region who are willing to build strong CCM foundations in your respective region. The Brits, Ausies, Germans, Irish, Dutch, South Africans, Haitians, et al who are based in America have their political parties registered on American soil, and I don't see why Tanzanians cannot the same. Let Texans have their CCM cake, but in the meantime, let's bake our own CCM cakes in our respective region. There should not be a monopoly on such an issue. That's what UHURU is all about.

    ReplyDelete
  30. WASHIKA DAU, CUF TAYARI INA WANACHAMA 15 HAPA NEW YORK. NITAPOST BLOG YA CHAMA HIVI KARIBUNI KWA ATAYEPENDA KUJIUNGA

    ReplyDelete
  31. acheni upuuzi wa vyama hapa Marekeni.watu tuna mambo ya maana hapa kuliko kubeba maboksi na kujiunga na vyama. we kama bado unafikiri ya mwaka arobaini shauri yako kalage baho wenzio tumeamka tunajitafutia maisha bora kwa kila mtanzania hapahapa. Na habari ndio hiyo kaeni na vyama vyenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...