Unkal pole na kazi,

leo lalamiko langu ni hawa askari wa usalama barabarani. Jana mchana walinikamata wakisema nimevunja sheria kupita wakati taa nyekundu inawaka jambo ambalo si kweli.

Tukaenda kituoni ili kutatua hilo tatizo. Cha ajabu nilipofika kule walikuja zaidi ya askari watano wakinilazimisha nilipe faini jambo ambalo sikuliafiki na wakaniambia waniweke ndani hadi ijumaa wanifikishe mahakamani.

Je hivi kweli ni sahihi mtu unapoenda kituoni kulazimishwa kulipa faini au kuwekwa ndani? Halafu nilipo lipa faini wakasema hawana risiti nifate kesho na hiyo copy niliyotuma ilibidi niombe waandike tena kwani ilikua haioneshi kitu? Je hii ni haki wadau?

Mdau NBC
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. KWA NINI ULIKUBALI KULIPA WAKATI UMEONEWA????...KWA KUFANYA HIVYO BASI, POLISI WATAENDELEA NA MCHEZO HUO HUO. UNGEKATAA KULIPA FINE AND THEN WAKUWEKE NDANI, HALAFU IJUMAAA UNGEENDA IPP MEDIA (ITV) KUTOA STORI YAKO....ILI SAIDI MWEMA AIONE, HALAFU AUNDE TUME YA UCHUNGUZI - KWA MAONI YANGU, WEWE ULIKOSEA KULIPA. USIOGOPE POLISI KAMA UNA HAKI, HAWA NI BINADAMU WA KAWAIDA TU.

    ReplyDelete
  2. huu ujinga umeenea pote tanzania na kwa bahati mbaya hautamalizika siku za karibuni kwa sababu walichokitaka hawa asikari ni wewe utoe rushwa. ilipoonekana hutaki kutoa posho ghafla ukawa adui yaani mtu asiyeelewa lugha ya afisa wake!!
    Dawa yako wewe adui unakomolewa ili siku nyingine upate kuzungumza ile lughha ineayoeleweka na inayotkiwa.
    ushauri wangu kwako; kama wewe ni mtu wa biashara, okoa muda wako wote na iwe marufuku kutembea njiani bila 3,000= hapo kwenye dash. you will save a great deal of your valuable (to you) time kwa kuwatupia hao mbw*
    mfupa uende zako. la sivyo watakusumbua tu.

    ReplyDelete
  3. Aliyekwambia kuna hki dunianai ni nani?

    ReplyDelete
  4. Uliyeleta hii mada ungetaja na ni police wa mtaa gani huo na kama majina unayo sema tu. Na hivi receipt kwanini zisiwepo?
    Na unayesema tupia mbwa mfupa ndio mnawaendekeza hawa watu..

    Baba yangu (RIP) aliibiwaga na alichukua miezi sijui mingapi kufuatilia report police ili akafile insurance claim. Hao police walikua wanamzungusha tu. Baba hakujua wanataka rushwa....Baba yangu alifariki bila kupata report yake lakini guess what walianza kufa mmoja mmoja kwenye hicho kituo cha police. Kuanzia mkuu wa kituo mpaka sijui mshika mlango...Machozi ya mtu hayaendi bure. Sijui kilichowaua lakini nadhani wana watoto wao ambao nao wanasononeka kama siye tulivyokua tunamwonea huruma baba yetu akifuatilia hiyo report kila siku. Na baada baba kufa habari ikafika kwa mkubwa wao wilayani report ilipatikana within a week. Nyie watu mnaopenda rushwa do the right things hamjui mnaumiza roho za watu kiasi gani.

    Hii nchi inatakiwa kubadilika

    ReplyDelete
  5. hao watu wanataka pesa wanalimbikiza
    dhambi lakini ukimwi itawamaliza.hizi hela wanatutoza ni kunyima watoto wetu chakula.

    mungu atawa komesha hapa hapa ulimwenguni.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa "baba yangu na Report" inaonekana baba yako aliondoka na roho za watu.Yaani baada ya kifo chake polisi nao wakaanza kumfuata kaburini.Dah hii sayansi yetu kwa nini tusiitumie kimaendeleo.

    ReplyDelete
  7. nimeipenda hiyo ya mzee alifariki na police nao kumfuata. mbinu gani ilitumika na cc tutumie maana wanatusumbua sana hawa watu. hayo malalamiko yako yarushe hawani kwa kova, ili washugulikiwe

    ReplyDelete
  8. pole kaka,

    Lakini kuna utitiri wa wanasheria kwa sasa takriban kila kona, masaki hadi manzese kwa mfuga mbwa.

    waone watu wa sheria badala ya kulalamika kwenye globu, humu kuna baadhi ya watu watakuprovoke tu kwa comments za kichovu.

    ReplyDelete
  9. Wamezidi sana hao wanaoongoza magari pale kamata, kile kituo kidogo kifungwe kinanuka rushwa watu wanalizwa huwezi kuamini.

    Pili wanafuatia hawa wa movenpick na halafu salender

    ReplyDelete
  10. Hiyo itakuwa mataa ya Sayansi au Bamaga jamaa wananjaa hao mimi hawachukui hata shng kumi,

    ReplyDelete
  11. juzi nilisimamishwa na askari wa barabarani nikiwa na gari yangu ndogo saloon , alivyofika ananiuliza leseni kwa ukali utadhani vile mwanae mimi , nikampa tena nilikuwa nishatoa leseni mpya za kisasa , akaiangaliaaa kama dakika kadhaa hivi kana kwamba yeye mwenyewe haijui ikoje then akaendelea kuniuliza vitu vingine fire extingushe na triangle nikamwambia ninavyo huku akiwa ameendelea kuishikilia leseni yangu mpya mara akazunguka kwenye insurance kuangalia mbele na kukuta kila kitu sawa ( yaani sina kosa ) akawa anajitahidi apate kosa lakini hamna , duhh akanicheki na kuniambia nanukuuu ( mzeee jua kali hapa ) mwisho wa kunukuu , mimi nikamwambia sio kwako tu jua kali hata kwangu , akanipa leseni yangu nikaondoka , roho ilimuuma kweli , mimi nasema hii nchi na RUSHWA ni tumbo moja haviwezi kuachana kabisa , tunadanganyana tu ooh eume ya rushwa sijui nini , mi naona wanazidi kupoteza pesa zetu za kodi kwa kufungua ofisi zengine kibao zisizokuwa na maana na kuwalipa watu mishahara ...

    na huu mtaji wao wa kubadilisha leseni ni mtaji wa polisi , asiyejenga mwaka huu atajenga ...

    mdau
    Dar-es-salaam

    ReplyDelete
  12. rushwa ndani ya polisi ni mwendelezo wa uongozi mbovu. kama viongozi wa juu ni mafisadi kwa nini watu wa chini wasile rushwa. badili system nzima mtaona mabadiliko.

    ReplyDelete
  13. wewe mdau wa mwanzo ushawahi kufkishwa kituo chochote cha polisi tanzania au unaropokwa tu?

    Kwa taarifa yako vituio vyetu vya polisi sio kama vya ulaya na marekani, usidhani kuwa mtuhumiwa ana haki zake, ni uhuni mtupu na bullying tactics ndio zinazotumika vituoni.

    ReplyDelete
  14. sahibu yangu alizidisha kukaa tanzania kwa siku moja na alipofika airport akaambiwa ni lazima alipe faini, hakupinga ila alitaka apewe risiti na surprise surprise akaambiwa risiti zimekwisha kama anataka risiti yake na amtume mtu siku inayofuata kwenda kumchukulia. Jamaa alishangaa sana na aliposema hiyo ni sawa basi nitampa huyo mtu hizo pesa kesho aje nazo alijibiwa usijifanye mjanja hapa!

    ReplyDelete
  15. Yote haya ni alama za nyakati. A change is coming to Tanzania, mark my words. Don't give up the struggle!!

    ReplyDelete
  16. Hao polisi usingewapa rushwa pili hakuna faini inayotolewa polisi bila proper receipt hawana receipt waambie uende mahakamani na usiogope ndugu yangu

    ReplyDelete
  17. Chanzo cha yote haya ni Uongozi mbovu unaokumbatia mafisadi na wapenda rushwa. Kama hata presidah leo anasimama kusema kuwa Lowasa mtu safi unadhani kwa nini mapolisi wasiige mfano wake na kuendeleza rushwa. We fikiria hata Redet imeshindwa sema ukweli ulio wazi kuhusu uchaguzi kwa kuogopa macho ya the fisadis.

    Na wewe mdau wa kwa Kulala kituoni si mchezo, labda kama ni mwehu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...