UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

BUSINESS SCHOOL

OFFICE OF THE DEAN

University of Dar es Salaam Business School (UDBS) ikishirikiana na Columbia Business School ya Marekani, kwa mara ya pili, inawapa fursa ya pekee wanawake wajasiliamali kwa kuwapatia ufadhili kutokaThe Goldman Sachs Foundation ya Marekani kwa ajili ya kusoma kozi ya “Advanced Certificate in Entrepreneurship and Business Management”. Kozi inatolewa kwa mwaka mmoja nani wakati wa jioni tu.

Lengo kuu la kozi hii ni kuwawezesha wajasiliamali kuendesha na kukuza biashara zao kitaalamu zaidi na kwa faida. Kwa kupitia wahadhiri waliobobea katika masomo ya biashara kutoka katika vyuo hivi viwili washiriki wataweza kuongeza uwezo wa kutambua na kunufaika na fursa mbalimbali za kibiashara, watakuza uwezo wa uendeshaji wa biashara, wataweza kuandaa michanganuo ya biashara yao inayokubalika katika taasisi za mikopo na wataunganishwa na vyanzo mbalimbali vya mitaji.

Mwombaji wa ufadhili anatakiwa awe mwanamke mjasiliamali mwenye biashara na awe na uwezo wa kuongea na kuandika lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

Kozi itaanza Terehe 6. 7. 2011 na kumalizika mwezi June mwaka 2012. Mwisho wa kupokea fomu za maombi ni tarehe 13.5.2011. Fomu za maombi zinapatikana kwa Dean, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, jengo la UDBS, chumba namba 310, au katika tovuti ya www.udbs.udsm.ac.tz .

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0715-004-280 au 0767-004-280

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. This is a very good opportunity. Natumaini wajasirimali watanzania wanawake watachukua hii fursa...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...