Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mh. Mathias Chikawe (aliyevaa suti nyeusi katikati), akiwa na Mbunge Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (kulia kwake) wakipiga makofi pamoja na wanachama wa kikundi cha Kuweka na Kukopa cha PFT, baada ya kufungua ofisi za kikundi hicho, Tandika, Dar es Salaam
Wasanii wa kikundi cha TMK Wanaume Family wakifanya mashambulizi pamoja na wasanii wa kikundi cha wachekeshaji cha The Orijino Komedy cha TBC, wakati wa hafla ya Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu kukabidhi hundi ya sh. milioni 12 kwa vikundi 27 vya VICOBA pamoja na harambee ya kuchangia mfuko wa kikundi cha PFT. Hafla hiyo ilifanyika jana kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.
Chakawe na wageni wengine wakifurahia shoo hiyo
Wanachama wa kikundi cha VICOBA cha Afya (kushoto), wakifurahia baada ya kupokea hundi ya sh. 444,000 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia). Anayekabidhi hundi hiyo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mh. Mathias Chikawe (aliyevaa miwani).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group, Bw. Yusufu Manji (kulia), akijadiliana jambo na Mbunge wa Temeke, Mh. Abbas Mtemvu (kushoto) pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Ndg. Ramadhan Madabida baada ya kuchangia kikundi cha PFT, sh, milioni 20 katika harambee hiyo. Zaidi ya sh, milioni 50 zilichangwa. Picha na Kamanda wa Matukio  Richard Mwaikenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...