Taarifa kwa wote,

Mkutano mkuu na tafrija ya mwaka ya TPN itafanyika tarehe 05/06/2011, Luther House, Azania Front, kuanzia saa 8 mchana.

Naomba wanachama wote na wanaotaka kuwa wanachama tuthibitishe ushiriki wa mkutano huu, hakutakuwa na ada ya ushiriki hivyo wanachama wote tujitokeze kwa wingi.

Agenda ni :
i. Kuwasilisha taarifa ya muda ya fedha ya TPN
ii. Kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi wote (Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mtaunza hazina na Naibu wake, na wajumbe wa kamati ya utendaji.
iii. Kupitia upya na kuweka malengo na mikakati mipya ya TPN.

Ni matarijio yetu kuanzia 8 hadi saa 12 tutamaliza agenda zote hizo na tutapumzika kwa muda ili kujiandaa na chakula cha pamoja cha jioni kwa watakaopenda kushiriki kuanzia saa 1 usiku.

Tafrija itafanyika siku hiyo hiyo baada ya mkutano kuanzia saa 1 usiku, ili kurahisihsa tumeona ni vizuri kila mwanachama akalipia chakula na kinywaji chake siku hiyohiyo na hapo hapo ukumbini kwa kadri atakavyoona inafaa hakuna bei maalumu, tunaongea na Hotel mojawapo ili tukapate chakula cha usiku pale na kupongezana kwa mafanikio mbali mbali miongoni mwetu, Tutachagua hotel ya karibu na ukumbi tutakaofanyia mkutano,taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Maoni mbali mbali pia yanakaribishwa jinsi ya kufanikisha au kuboresha matukio hayo.

Naomba wote tuthibitishe ushiriki wa matukio hayo , utuambie kama utapenda kushiriki mkutano tu au na chakula cha usiku.

Naomba kutoa wito kwa wanaopenda kuwania nafasi za uongozi pia wajitokeze, siku ya mkutano kutakuwa na fomu za kujaza pale ukumbini, mnaruhusiwa kuweka nia kuanzia sasa.. nafasi zote ziko wazi.

Naomba tuwafahamishe na wengine wote tunaowafahamu.

Naomba tushirikiane, nawatakia kila heri.

Phares Magesa
Makamu wa Rais-TPN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...