ALIYEBUNI JINA LA TANZANIA?




Mwandishi Alphonce Tonny Kapelah kutoka Mtwara Leo ameona aufahamishe umma juu ya mwasisi wa jina la Tanzania.
Nimeona niwafahamishe hili huenda likatusaidia hasa kwa hivi sasa wakati tukisherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tangayika, najua wengi wetu hatujui historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar maana tuliwakuta waasisi wetu wameishafanya zoezi hilo, tusilijadili sana kwa kuwa lengo laolilikuwa zuri.
Lakini je unamjua huyu Bwana aliyetunga jina la Tanzania pata historia ya namna alivyofanikiwa kupata jina la T A N Z A N I A?
Kupata habari zaidi mtembelee mwanalibeneke wa Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2011

    Muongo sana siku zote alikuwa wapi kuujulisha umma kwamba yeye ndiye mwanzilishi. Kwanza hajagundua, kama ni yeye kaunganisha tu majina

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2011

    Very insightful...Thank you. Maybe the remaining 15 did not show up because they couldn't make it for various reasons and also maybe the price was not worth traveling, commuting for e.t.C

    Mr. Iqbal is very creative and deserves some credit but I still think that he should not get all the credit for the name just because he was the only one who showed up at the ceremony. I believe the remaining 15 also had their own unique stories in the making of this beautiful name Tanzania. I would love to also hear how they came up with the name---that could be a good book to write about:)

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2011

    "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" Huyu ndugu anastahili kupongezwa na kuthaminiwa wala si busara kumpuuza maana alitoa ufumbuzi mkubwa ambao leo taifa lina kitambulisho ambacho ni hilo jina Tanzania;na ukweli ni jina zuri. Hizo ni kazi za Muumba huwapatia watu vipaji vya ubunifu hajalishi dini rangi wala kabila. Big up my brother!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2011

    Sasa alipotunga hili jina na kulihusisha na jina lake na dini yake (kwamba "I" inahusiana na herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na "A" kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya) hao walioendesha chindano walikubaliana na hoja yake? deninitely NO. Kama ni yeye alitunga jina la tanzania, sawa lakini justification ya neno Tanzania haihusiani na dini au jina la mtu. Wataalam wa historia chuo kikuu cha dar es salaam watakua na maelezo ya kueleweka zaidi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 17, 2011

    I dont believe you, you need more people. Baada ya miaka yote ya Muungano leo ndo tunasikia hizi kelele. Kwenda zako huko. Ina maana hakuna kumbukumbu za serikali za kuthibitisha hii stori? Maktaba ya Taifa lazima ina vithibitisho vya nani alitunga jina la TZ.Mfano kuna mama toka Bukoba aliniambia mwalimu wake wa primary alishiriki kama sio kutunga hili jina.Watz tunaamini sana stori za vijiweni ndo maana hatupo intelligent.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2011

    Nyinyi kila kitu hamuamini kwa kuwa yeye muhindi au vipi? Inawezekana alifanya hivyo kwa imani yake na akafanikiwa, kwani vibaya?

    Wewe mdau wa kwanza huyu Muhindi alishatokea kwenye tv zamani kidogo na akatoa maelezo, labda wewe ulikuwa hujazaliwa au bado ulikuwa shamba.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2011

    mi ningeiita ZANTANIA, na hizo IA baada ya ZANTAN zinamaana katika lugha ya kiarabu kama uraia. Mfano Arabia maanaye mwarabu. Tunisia ni Mtunis.

    Zanzibar ndo chanzo cha sisi kuungana kwani Mwl aliogopa maadui watakitumia kisiwa hiki. Mbona hatukuungana na nchi nyengine?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2011

    Sawa yeye alilibuni mwaka 70s ya muungano,sasa ukisoma GREEK'S Periplus of the Erythraean Sea kutoka karne ya 1 AD,UTAKUTA JINA AZANIA LIMETAJWA NA NI SEHEMU KUTOKEA ETHIOPIA SOMALIA HADI RUFIJI IKIWEMO VISIWA VYA ZANZIBAR WAKATI HUO VIKIJULIKANA KAMA MENTHUAS Ngoja nikuwekee kidogo extract KUTOKA LUGHA YA KIMANGA... emporíou stis aktés tis Azania , pou onomázetai Rhapta , KWA KIENGEREZA "Two runs beyond this island [Menuthias = Zanzibar?] comes the very last port of trade on the coast of Azania, called Rhapta,

    SASA SIJUI KAMA ALIBUNI TU BILA KUJUA HISTORIA ILOANDIKWA TOKEA KARNE YA MWANZO,NA PIA KABLA KARNE YA KWANZA Pliny the Elder ALISHAANDIKA KUHUSU "Azanian Sea" mnamo(N.H. 6.34).

    JE MKWELI NANI? (MDAU WA JIJI LA HISTORIA UGIRIKI)

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2011

    kutumia lugha kali kujibu hoja ya huyu ndugu sio vizuri. Tujaribu kumjibu kiungwana tu pasipo kutukanana. Je anao ushahidi wowote wa hati au barua yoyote ya kuthibitisha madai yake.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 17, 2011

    hana lolote!! mwongo tuh!!, wahindi kwa misifa lol.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 17, 2011

    Hivi ndo tukiambiwa kuna watu watanzania bado wako mashimoni kweli tukubali. Maana hii habari kuna mijiutu inapinga katika maoni yao bila uthibitisho wowote halafu wanasema pumba wakati hiyo pumba ina kila uthibitisho. nyie mnayo ipinga hii habari toeni bas uthibisho wenu na nyie sio mnapinga tu. kama hamna mjue basi nyie mnaopinga ndo mnaongea pumba. Maana apo pana kila uthibitisho hadi no simu ya huyo mtu. Tupingeni kwa hoja sio kupuliza mavuvuzela tu. Wake up !!!!1

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 18, 2011

    Very interesting. Nakumbuka zamani niliwahi kusikia kuwa kulikuwa na mashindano ya kutafuta jina la muungano huo mpya na wa kwanza Afrika. kwa mujibu wa mwalimu wetu Form 6 Mkwawa, Mwalimu Nyerere alisita kati ya kuchagua Tanzania na Azania, hatimaye Tanzania ikapitishwa. Mimi naamini makala hiyo kwa kuwa nasikia kule Nationala Archives (Nyaraka za Taifa) kuna stori hiyo hiyo, ijapokuwa mimi mwenyewe sijaziona nyaraka hizo. Mbarikiwe wote.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 18, 2011

    Bana Iqbal asente sana bana. Sisi Tanzania yote dugu, Tanzania hakuna dini. Krito sawa, Islam sawa, Pagani sawa tu. Sisi yote napenda sana wewe iqbal.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...