Hi Ankal Michuzi!!
 
Naomba msaada kwenye tuta!!
 
Mimi Magreth Pendaeli Mushi namtafuta mwanangu mpenzi ZUHURA STANLEY MGWENO ambaye nimepotezana nae tangu mwaka 1995 ila ninachofahamu ni kwamba yuko nchini Finland. Naambatanisha picha yake ya mwisho aliyowahi kunitumia akiwa na rafiki zake hapo chini. Juu akiwa nyumbani Tanzania
 
Natanguliza shukrani zangu nyingi sana kwa atakae nisaidia kumpata mwanangu jamani.
 
Anaweza kunitafuta kwa namba zifuatazo:-
Magreth Mushi 0715 810118
Hamza Kiterebu 0716 234729
 
 
Akhsante

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2011

    hello michuzi,nimejitahidi kumsaidia huyu mama,mie niko norway nimejaribu kuunganishwa na telephone operater wa finland wametafuta hilo jina wamelikosa via telephone,nimepata adress yake ambayo ni Zuhura Stanley Mgweno
    kalevantie 21B
    26,90570
    OULU
    FINLAND..
    mama pole sana natumaini utampata tuu kupitia blog hii ya jamii.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2011

    Jamani namuhurumia huyu mama,sasa huyu msichana mzima au vipi kweli mara ya mwisho kuwasiriana na mama yake ni toka 1995?mimi nimekuja uingereza miaka 19 sasa lakini sipiti week bila kuwajulia hali wazazi wangu,.
    Tuombe mungu huyu msichana mzima wa afya njema,pole sana mama je kama unamarafiki zake wengi labda ujaribu kuwasiliana nao kwakweli ili jambo ni zito.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2011

    Mama wasiliana na chama cha watanzania kiitwacho KILIMANJARO mwenyekiti wake anaitwa Zamu hao jamaa wanaweza kukusaidia kwani nimesikia mda si mrefu watakwenda Finland kucheza mpira
    Vinginevyo nitajitahidi mimi mwenyewe nimtafute Majidi Mjengwa ambae yuko Sweden sasa tujue anaweza kukusaidia vp
    Pole sana mama
    Mdau Iceland

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2011

    Wabongo kwa ngenga mmezidi,jiulizeni kwa nini kapausha namna hiyo bila kuwasiliana na wazazi then utapata jibuI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2011

    Nimeongea na mtoto wa Zuhura jana,anayemtafuta ni ndugu yake, nimempatia mawasiliano na amesema kupitia kwa mwanae (kwani yeye mwenyewe ana matatizo ya kusikia hivyo hawezi kuongea)kuwa watamtafuta na wameahidi kumtafuta.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2011

    Haingii akilini tangu 1995 mtu hawasiliani na wazazi wake!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2011

    ni watu wengi sana tumekuwa tukiwatafuta ndg zetu walio nje... hili ni tatizo kubwa... mim binafsi kuwasiliana na kaka yangu mara ya mwisho ni mwaka 2004 hadi leo familia nzima hatujui anaendeleaje huko aliko. alikwenda australia miaka ya mwanzoni mwa 1980 hadi leo hajarudi Tanzania wasifu wake;-

    jina lake: William Dominic (Wills)
    umri wake kwa sasa ni zaidi ya miaka 50
    kabila: Mbena - asili yake njombe iringa
    wazazi wake wanaishi mbeya

    kama kunamtu anaweza kuwa na taarifa zake tuwasiliane kwa francylumbo@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2011

    Ughaibuni sio Tambarare!! Ndio dunia wengine wanapata mafanikio na wengine wanapata mashaka. Kilichobaki ni kwamba anayemjua amsaidia mama yake kumpa taarifa ili wawasiliane.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 18, 2011

    Anony hapo juu usiseme haingii akili, sisi yaliotutokea ndio tunaojua ukweli, kaka yangu alikaa ugiriki miaka 29 hatukujua habari zake, mpaka siku alivyorudishwa, tulistukia hodi mlagoni tu, ni kweli yapo

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2011

    Watu wengi wakishafika huku mambo yakawaendea vibaya wanajilipua na kujiita majina mengine hasa Watz, wengine wanabadilisha majina au uraia na kujita wasomali, alikuwa mkrisdatu anakuwa mwiisilamu hata mimi namfahamu dada mmoja Tz anamtafuta mume wake tangu aje Ulaya 1992, alikuwa anatuma hela za matumizi ghafla akaacha hadi leo hatuji. Watz tubadilike tusiwape wazazina ndugu zetu pressure

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 20, 2011

    JAMANI NANI KAMA MAMA? MUWE MNAULIZIA SANA WAZAZI WENU MSIWASAHAU MTAKOSA BARAKA KAMA NI FINLAND MBONA KARIBU TU NA KAMA UNATAKA URAIYA BORA OLEWA UTAUPATA TU NJOO NYUMBANI UKIKUTA MAMA KAFA UTALILIA WAPI NDIPO UTABAKI NA LAANA TU

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 20, 2011

    achenu zenu kubadili majina au kua wasomali imeingiaje hapo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...