Warembo wa Redds Miss Ilala wameondoka usiku huu kuelekea Nairobi, Kenya. Pichani wanaonekana warembo hao wakipanda gari lililowapeleka huko Nairobi kwa ziara ya siku kadhaa katika mafunzo na utalii kabla  ya fainali za Vodacom Miss Ilala Julai 29, 2011.
 
Warembo watakaoshirki mashindano ya kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya Ilala wameondoka kwenda Arusha na Nairobi kwa ziara ya siku nne ambayo ni safari ya kimafunzo na Utalii .
Kesho wakiwa Nairobi, wanategemewa kukutana na Miss Kenya ambaye pia anashikilia taji la Dunia la Urembo wenye Malengo ( Miss World 2011- Beauty with Purpose). Mlimbwende huyo atawapa darasa kuhusu urembo wenye malengo, kujiamini na kujua usichana ni nini. Pia wakiwa Nairobi, warembo watatembelea kambi ya Wasichana watakaoshiri kwenye shindano la kumtafuta Miss Kenya na kufanya nao mazungumzo. Watatembelea  sehemu zenye kuvutia za mji huo na kurejea Arusha.
Warembo wanatarajia kutembelea mbuga ya Taifa ya Manyara kuona wanyama na kujifunza kuhusu urithi wa Taifa letu na baadaye kurejea mjini Arusha na kufanya shoo kwenye klabu ya Matongee.
Msafara wa warembo kumi na tano na unaongozwa na Afisa utamaduni wa Manispaa ya Ilala Mama Shani Kitogo anasaidiana na Afisa Habari Msaidizi wa Manispaa. Wengine katika Msafara huo ni Regina Joseph ambaye ni Mkuu wa Kambi, Bahati Chando- Matron, Adelhard Adex -Mkuu wa Itifaki na Nidhamu na Emma Mbangarara – Ulinzi na Usalama. Warembo wanaosafiri ni Maria John, Jenifer Kakolaki, Priscilla Mchemba, Nasra Salim, Diana John, Faizal Ali, Maryvine Kenzia, Godliver Mashamba, Edna Mnada, salha Israel, Augostina Mshanga, Lilian Paul, Mariam Mashamba na Ritha Joseph.
Safari ya kimafunzo ya kwenda arusha na Nairobi imewezeshwa na Vodacom Tanzania ambao pia wamewawezesha warembo kuendelea kuwasiliana na ndugu na jamaa kwa kuwapatia simu mpya na muda wa maongezi. Tofauti na mitandao mingine kadhaa ukiwa na line yako ya Vodacom unaweza kuendelea kuwasiliana na ndugu na jamaa ukiwa nchi yoyote na kwa warembo watakao kuwa Kenya wataweze hata kuongeza salio, kutuma ujumbe na kufaidika na kufaidika na huduma zitolewazo na Vodacom wakiwa nchini Kenya kupitia washirika wao ambao ni Safaricom.
Shindano la Miss Ilala linategemewa kufanyika Siku ya Vunja jungu, Ijumaa ya tarehe 29 Julai katika viwanja vya Mnazi mmoja katikati ya jiji la Dar es salaam.
Redds Miss Ilala 2011 imedhaminiwa na Redds original, Vodacom Tanzania, Michuzi Blog, Paradise City Hotel, Paris Pub, Tanzania Standard newspapers, Jambo leo, Papazi Entertainment, Fabak Fashion, Channel Ten, TV Sibuka, Syscorp Group, 88.4 Clouds FM na B2C company.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...