Ankol hembu tusaidie kuwaambia hawa INVESTORS wa Kitanzania we want friendly services that we can access at comfort of our houses!
Nimeingia nyumbani saa tatu hivi, umeme hakuna ulipowaka nikagundua Kingamuzi changu cha Star times kimekata. Anko amini usiamini sikuwa na uwezo wa kununua kadi kielektroniki! Hakuna cha Em Pesa wala nini inayoeza nunua vocha yao ama mie sijui. nimeingia kwenye tovuti yao kuna viunganishi visivyo hai.
Tafadhali waambie kwamba tunataka tununue huduma kimtandao, inapaswa kuwa inawezekana!
Natanguliza Shukrani
Mdau Dar
Hiyo ndio bongo wenye pesa na wasiokuwa nazo wote wanahangaika sawa katika baadhi ya huduma.
ReplyDeleteWestern Union unalipia photocopy ya kitambulisho chako.
Kwenye mabenki foleni mpaka barabarani,ATM ndio kabisa, haswa NMB.
Mafuta, mwenye bajaji na mwenye M.Benz wote sawa.
Foleni za barabara ni kwa wote maana hakuna Toll road.
Ofisi za serikali mpaka wamalize kusoma magazeti asubuhi na kula vitumbua ndio uhudumiwe.
Ukiishi bongo kubali hali ya kibongobongo,maisha yataenda kilaini ila ukitaka kulinganisha na nchi nyingine utalia mwenyewe.
Unakwenda kununua kitu dukai utafikiri wewe ndio mwenye shida-jamaa hata hawakuulizi unataka kusadiwa nini
BONGO's Customer Service=ZERO
Ni kweli kabisa mdau,mimi pia nahitaji kuweza kununua vocha zao electronically.si sawa kwa maendeleo tuliyonayo kuanza kuhangaika na foleni hadi ofisi zao zilipo kwenda kununua coz hata huko mitaani kulikobandikwa posters zao za "vocha za star times zinapatikana hapa",ukienda unaambiwa huduma haijaanza.
ReplyDeleteMbaya zaidi,hata huduma yao hairidhishi sana kwa kweli,sometimes channels hasa za tanzania,hazitoi sauti,ama remote haisense kabisa,ama sauti inapanda yenyewe,au channels hazionekani kabisa..wametoa namba ya kupiga for customer services,ukipiga kama kawaida hupokelewi kwa wakati unawekwa online kwa kmuda mrefu,huku unalipia/unakatwa pesa ktk simu.mwishowe salio linaisha na kuwapata hujawapata.hii sio sawa kabisa.jamani,nyie mliowekeza,kama gharama mnayochaji kwa kutuhudumia ni ndogo kiasi cha kutoa huduma hafifu,ni vema mkatuongezea malipo ya mwezi,huduma iwe nzuri.Blogu ya jamii tusaidieni kutufikishia ujumbe huu.