TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MZEE MHANDO MUSSA MAKUNGA KILICHOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JANA JUMATANO YA NOVEMBA 02,2011 SAA TANO ASUBUHI.
MAREHEMU NI BABA MZAZI WA MWANDISHI WA HABARI NOVATUS MAKUNGA NA NDUGU ZAKE CHARLES,COLE,MWALIMU JOYCE,ANNETTE,ISRAEL NA ERNEST
MSAFARA WA KUTOKA HOSPITALI YA MUHIMBILI UTAANZA LEO SAA SABA MCHANA NA IBADA YA MAZISHI PAMOJA NA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA MAREHEMU ITAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KIBAMBA SHULE KUANZIA SAA TISA MCHANA WA ALHAMISI.
MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA KIJIJI ALICHOZALIWA CHA PINGO WILAYANI KISARAWE MKOANI PWANI IJUMAA YA NOVEMBA 05,2011 AMBAPO MSAFARA WA MAZISHI UTAONDOKA KIBAMBA SHULE SAA MBILI ASUBUHI.
WAKATI WA UHAI WAKE MAREHEMU ALIFANYAKAZI KATIKA ILIYOKUWA EAST AFRICAN RAILWAYS KATIKA NAFASI MBALIMBALI MPAKA KUFIKIA STATION MASTER NA BAADAYE ALIENDELEA KATIKA LILILOKUWA SHIRIKA LA RELI NCHINI[TRC].BAADAYE ALIJIUNGA NA MAMLAKA YA PAMBA,SHINYANGA AMBAPO ALIKUWA TRANSPORTER MANAGER.
BAADAYE MAREHEMU ALIFANYAKAZI KATIKA MAMLAKA YA KOROSHO TANZANIA KATIKA MAKAO MAKUU YAKE YALIYOKUWA MTWARA AKIWA MENEJA WA UNUNUZI NA USAFIRISHAJI KABLA YA KUWA MENEJA MKUU WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA MKOANI LINDI.
BAADA YA KUSTAAFU KAZI ALIFANYAKAZI KAMA OFISA TAWALA KWA MKTABA KATIKA MRADI WA NATIONAL AGRICULTURE AND LIVESTOCK EXTENSION REHABILITATION PROJECT NALERP)ULIOKUWA CHINI YA WIZARA YA KILIMO
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE,MWENYE MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEENI
I.W.R...Mdau Nova kada mwenzangu pole kwa kuondokewa na kipenzi baba. hakika kwa Mola sote tumetoka na kwake sote tutarejea.
ReplyDeleteJitahidi kuwa na subira na kumuomba mola katika kipindi hiki kigumu.