UONGOZI WA NEW YORK TANZANIAN COMMUNITY PAMOJA NA WANAJUMUIYA WOTE TUNATOA PONGEZI ZETU ZA DHATI KWA MUHESHIMIWA MLEZI WETU BALOZI OMBENI SEFUE KWA KUTEULIWA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI.
TUMEPOKEA KWA FURAHA TAARIFA ZA UTEUZI WAKO NA TUNAAMINI UTEUZI WAKO UMETOKANA NA UPEO NA HISTORIA YAKO KATIKA KUONGOZA.TUNAAMINI KUWA BUSARA NA HEKIMA ZAKO NI HAZINA KWA TAIFA LETU CHANGA.
VILE VILE TUNAMPONGEZA MUHESHIMIWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,DK. JAKAYA KIKWETE KWA MAAMUZI YAKE YA BUSARA..
TUNAMUOMBA MOLA AKUZIDISHIENI HEKIMA MARADUFU NA AKUPENI AFYA ILI MUWEZE KUTUONGOZA VEMA..
HAJJI KHAMIS
CHAIRMAN
NEW YORK TANZANIAN COMMUNITY
kweli watanzania kazi tunayo,yani hadi leo hii wewe unaamini Tanzania ni Taifa changa!!!!!!!!!!!kuna nchi lukuki ambazo tulipata nazo uhuru mwaka mmoja ila leo ziko mbali kimaendeleo pia kuna nchi tulikuwa nazo sawa kiuchumi katika miaka tunapata uhuru ila leo hii wametuzidi mbali...sasa Uchanga wetu uko wapi?
ReplyDeleteAnnoy wa dec 31 10:15:00am 2011 asante sana.maana kuna watu wanachekesha sana eti TZ nchi changa kivipi na tathimini gani aliyotumia kusema changa kweli amechemka.kwa rasilimali tulizokuwa nazo tungekuwa mbali sana kimaendeleo ila upuuzi unaoendelea hapo hatutaendelea kamwe!
ReplyDeleteNadhani siyo busara kutukana pasipo sababu.Na hata kama kuna sababu basi ustaarabu waweza kutumika.
ReplyDeleteNirudi kwenye hoja ya msingi.
Tanzania kuwa Taifa changa.Hii ni kweli bado ni taifa changa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
1.Nchi ambazo zinakabiliwa na umaskini mkubwa-Tanzania pia.
2.Nchi ambazo hazijafanikisha elimu ya msingi kwa kiwango kikubwa-Tanzania imo.
3.Nchi hambazo hazijahamasisha usawa wa jinsia na kuwezesha wanawake-Tanzania ndo inaanza 50% by 50%.
4.Nchi ambazo zinakabiliwa na vifo vya wachanga[watoto]-Tanzania imo.
5.Nchi ambazo hazijaweza kuondoa vifo vya akina mama-Tanzania imo.
6.Nchi zilizoshindwa kuthibiti maambukizi ya ukimwi,malaria na magonjwa mengine-Tanzania imo.
7.Nchi ambazo zimeshindwa kufanikisha ustawi endelevu wa mazingira-Tanzania imo.
8.Nchi ambazo zinategemea misaada ya wafadhili na wahisani kutekeleza mipango ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu-Tanzania imo.
Kwa ufupi,ni vigezo vingi vinavyo dhihirisha uchanga ama uendelevu wa Taifa husika.Kwa lugha ya kiingereza nchi changa ndizo zinaitwa the poor least countries au Third World Countries ama the developing countries na pengine zinaitwa beggar countries.
Nawasilisha!
Basi ungesema taifa ambalo liko nyuma kimaendeleo ila sio uchanga. Tuna uchanga gani?
ReplyDeleteHalafu kama barua umeandika kwa niaba ya community, jina lako la nini?
Ninaelimisha jamii na lengo langu ni kila Mtanzania na raia yeyote wa dunia hii awe huru kifkra kwanza ndiyo aina nyingine za uhuru zifuate.
ReplyDeleteAnonymous: Sat Dec 31, 02:51:00 PM 2011:na watanzania wengine wenye kutafuta uhuru wa kifkira!
Tunapokuwa tunaainisha na kuchambua dhana mbalimbali zinazolenga taifa lelote duniani,wataalam wa mambo tunaangalia na kuzingatia nyanja ama maeneo mbalimbali yanayoumba dhana ya utaifa.
Neno uchanga kama lilivyotumiwa na Mwenyekiti wa Jamii ya Watanzania waishio New york, huo ni msamiati uliozoeleka na unaotumiwa na mtu yeyote,taifa lelote,asasi yoyote na shirika lolote nk. katika jumuia ya kitaifa ama kimataifa.
Taifa siyo binadamu tunayempima weledi,ufahamu,maarifa,busara,hekima,uelewa nk. kwa kuzingatia kigezo cha umri kama inavyodhaniwa na watu wengi.
Hata hivyo haya ni maoni yangu binafsi sijatumwa na jamii ama kikundi cha watu ndiyo maana nahitimisha kwa kuweka jina.
Naomba ieleweke hivyo!
Tupunguze "siasa za uongo". Tanzania sio Taifa changa. Sasa sisi tukiwa taifa changa Sudan kusini wao wajiite jina gani?
ReplyDeleteili swali la jina la nini sio lako Global
ReplyDeleteNi changa kwa viwango duniani. Ni sawa na kusema taifa kiwete may be kutokana na kiwango cha maendeleo.
ReplyDeleteShida hapa ni lugha tu na si maana ya muda ama tumepita nchi ngapi kwa maendeleo.Tuangalaie umaskini tulionao na hali halisi ya maisha ya watanzania.
Again ni lugha ya kawaida-uchanga wa kimaendeleo kwa kuangalia shali ya maisha na huduma za msingi na sio nchi ina umri gani ama tumepita wangapi.
Your arguement ina maana ila ni utamaduni kujiita hivyo na sio sayansi ama real facts
Baadhi yetu Watanzania huwa tunapenda kutumia kauli mbaya sana, kila mara tunajidharau katka kila sekta na hii imezoeleka sana ndio maana hata jirani zetu wanatumia udhifu wetu kutushusha. Kauli za 'Tanzania nchi changa', 'Tanzania nchi maskini' hazina mashiko kwa sasa. Hatuna uchanga wowote miaka yote hii 50 bado tu wachanga!!, utajiri wote huu tuliokuwa nao wa madini, maliasili, ardhi yenye rutuba n.k bado tunajiita maskini!!!. Lazima tujitutumue, tutumie utajiri tulionao tujiendeleza na tuache kauli za kujishusha za uchanga, umaskini.Tujiulize ni lini tutakomboka kifikra kama sio kujikomboa wenyewe? Tanzania tumezisaidia nchi nyingi kujiondoa katika lindi la kutawaliwa lazima tujivunie heshima yetu, hivi hata hao tuliowasidia leo hii wanatupita kwa nini?
ReplyDeleteHuu ni ujinga. Taifa changa, taifa changa kitu gani? Taifa changa huku wewe unakula raha New York. Unazijua hata tabu wanazozipata victims wenyewe walio katika rural areas na interior Tanzania? Au unazisikia tu? Kama alivyosema msemaji mmoja humu, hizi ni siasa za uwongo! Na mimi naongeza, pia ni unafiki wa hali ya juu na kujipendekeza!
ReplyDeleteImagine jana tu hapa tulikuwa na debate kali humu kuhusu issue ya TRA, ambayo ilinifanya nifikirie sana jinsi serikali yetu na wanasiasa wake wote wanavyojua kupiga domo tu huku utekelezaji ukiwa wa hovyo kabisa. Hao maofisa wa TRA wanavyoporomosha majumba na magari ya kifahari huku wanasiasa mkizidi kutuletea hadithi za "taifa letu changa" na huku ninyi mkiendelea kula misaada kutoka kwa donors na kodi ya wananchi kwa kutumia vigezo hivyo na kauri mbiu hizo zimetuchosha sana haki ya Mungu. Tumezisikia toka miaka 50 iliyopita!!
Na mimi nasisitiza tena kama wenzangu waliopita, Tanzania siyo taifa changa, ni taifa "zee" linaloliwa na "wajanja". Hivyo wewe usituletee longo longo yako hapa Watanzania sasa hivi tumeamka na tumesoma, and I promise you we'll get you people one day.
Mdau.
Taifa changa lakini wezi wake wamekomaa...utadhani walikuwapo miaka 200 iliyopita....!!
ReplyDeleteMdau-USA
Hii ni uchanga wa mendeleo na siyo
ReplyDeleteuchanga wa taifa, wakati nchi hizo
zilikuwa zinafanya maendeleo sisi tulikuwa tunafanya ujamaa, kwa hiyo
ilibidi tuanze upya which was only 15 yrs ago.
I Agree with you anony-Sat Dec 31, 08:46:00 PM 2011, One day we'll wake up and sing our new song...time will tell! Huku tuliko "kwa watu" wanatushangaa, nchi gani yenye kila kitu then mnajiita maskini! wakati mwingine wanaona kama tunaigiza ili tupate misaada! Kwa kweli inatia uchungu! Mwenyezi mungu wasaidie watawala wetu wakumbuke na kuwaonea huruma wananchi wao...wasio na chakula, maji, nyumba bora, hospitali n.k. huku watawala wakiendelea kugawana nchi yetu kama vile urithi kutoka kwa baba zao!!!
ReplyDeleteati nchi changa utamuita baba mtu mzima wa miaka 50 mchanga? huyo si baba mwenye wajukuu kabisa? kungekuwa hakuna rushwa na mambo ya kubebana nchi ingekuwa inapaa ni hayo tu, kila mahali ni ulaji tu na umimi!
ReplyDeletemwenzenu anajigonga hapo apate njia ya maisha yake na ndugu zake wakienda kupata misaada na kusaidiwa kula na hao wakubwa.
ReplyDeleteulaya watu wanagombania kuwa wenyekiti sababu wanakula pesa za serikali bureeeee.
wengine wanagombana na hii inatokea nchi nyingi.
nadhani huyu chairman angewapatia copy hii watanzania wa new york wasome basi wangemkosoa atoe vijineno kabla ya kurusha humu.
Michuzi usibanie comment yangu please, inabidi watanzania kujifunza kwa kukosolewa.
Wacheni ubishi wa kijinga. Tanzania ina miaka 50 ya uhuru. Marekan na Ufaranza zina miaka zaidi ya 200 kama taifa. Uingereza zaidi ya miaka 300, the list goes on and on and on. Je, ukiangalia miaka hii, Tanzania sio Taifa Changa?
ReplyDeleteKama hiyo haitoshi, Tanzania ni maskini wa kutupa. Huwezi ukalinganisha nchi za Marekani, Ufaransa, Uingereza, Uchina, Brazili na nyinginezo nyingi kwa utajiri, kwa sayansi na teknolojia. Tanzania ni changa hata upande huu.
Katika soka, Tanzania tunasota. Hatujawahi kucheza fainali za kombe la dunia, tumecheza fainali moja ya kombe la Afrika, hatujawahi kutia mguu Olimpiki kama Taifa Stars. Tanzania ni Changa hata upande huu.
Tukija katika viwanda. Tanzania tuna viwanda hata kumi vya maana havifiki. Tanzania ni CHANGA hata hapa.
Tukinda katika sekta za barabara na reli. Barabara zetu bado si nzuri. Huduma za reli si nzuri. Air Tanzania mwendawazimu, Tanzania ni changa hata hapo.
Listi hii inaendelea.
Kwahiyo ubishi wa kijinga haufai.
Balozi Sefue hongera sana sasa katibu mkuu, Tanzania tunahitaji viongozi makini kwa wewe. Nchi imeonza na mafisadi.
ReplyDeleteHongera sana.