Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema yeye si mfanyabiashara wa dawa za kulevya ila anatajwa kwa nia ya kunyamazishwa asizungumze ukweli.

Kardinali Pengo akizungumza na vijana katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana alisema hajapata kuona wala kujua dawa za kulevya, lakini anajua anatajwa hivyo na wanaotaka anyamaze, “Mimi mwenyewe nimewekwa katika orodha ya dawa za kulevya, naona kwenye vyombo vya habari, dawa zenyewe wala zisijui, lakini naendelea kuzungumza kwa sababu najua yanafanywa na wanaotaka kuninyamazisha … sitanyamaza ng’o,” alisema Pengo.

Alikuwa akiwaeleza vijana kuhusu utandawazi na kuwataka waache kuyumbishwa na kuamini kila wanachoona kimeandikwa kwenye mtandao.

Alisema mambo mengi ya ajabu yamekuwa yakiandikwa na kusemwa, lengo ikiwa ni kunyamazisha maaskofu na mapadri wasiendelee kufundisha ukweli, ili watu wachache wafaidike, “Ni uzushi unaofanywa na watu kuharibu na kuchimbachimba Kanisa tusiseme ukweli, wachache waendelee kufaidika, naomba vijana msisombwe na hali hii, kwani watu hawa hawana woga ili mradi lengo lao la kuharibu Kanisa lifanikiwe … vijana mna uhai ndani yenu na mna uwezo kama maaskari wa kupambana na waovu wa Kanisa,” “Silaha ya vijana ni maisha yanayojua mnaamini kitu gani, msikubali kuyumbishwa na watu wanaotoa mambo vichwani mwao. Kama mnasikia natajwa, njooni mniulize, Baba mbona nimesikia habari fulani, badala ya kuyabeba na kushabikia…imani yenu si ya kutetereka, endeleeni kuwa imara watetereke wanaotaka tutetereke,” alisema.

Alisema vijana pia wamekuwa wakitumika kama vyombo katika biashara ya kulevya huku watu wachache wakitajirika na kwamba baadhi yao wanaokemea au kuzungumzia, wanapuuzwa au kuambiwa ndio wafanyabiashara wa dawa hizo, jambo ambalo nyuma yake halina ukweli wowote.

Kardinali Pengo alisema lengo ni kutaka kuwanyamazisha watu wanaosema ukweli ili wachache waendelee kutajirika na biashara hiyo kwa kuwatia hasara vijana.

Naye Mhashamu Askofu Salutaris Libena, ambaye aliongoza Ibada Takatifu, alisema vijana wamekutana ili kumshukuru Mungu na kumwomba neema .

Libena ambaye pia ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, aliwataka vijana kuingia mwaka mpya kwa kumjua na kumtukuza Mungu.

Mbali na vijana kushiriki ibada hiyo lakini pia zilikuwapo burudani mbalimbali za kwaya na ngoma, sambamba na vijana kupima kwa hiari damu kwa ajili ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Kila mwisho wa mwaka vijana kutoka makanisa mbalimbali ya Kanisa Katoliki hukutana kwa lengo la kumtukuza Mungu na kumshukuru kwa kumaliza mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Sasa nimefumbuka macho kwanini viongozi wa dini wanaambiwa ni wauza dawa za kulevya...kuwafanya wanyamaze na wasikemee uovu huu.....Mungu wangu! Haya yalitokea Latin Amerika kwa Askofu Mkuu Romero!

    ReplyDelete
  2. Hiyo ndo Bongo baba..
    Ukiingilia dili za wakubwa lazima wakupe kesi ya Bangi.
    Kuchafuliwa ni dakika moja tu.

    ReplyDelete
  3. Sema usiogope, sema usiogope!

    ReplyDelete
  4. Lakini na yale madhehebu tunayoona kwenye TV ya hapa nchini waumini wakitoa ushuhuda wa utajiri kwamba walikuwa hawana kitu lakini baada ya kuingia kwenye hayo makanisa mambo yamebadilika ghafla na wakijisifia sijui nina nyumba, nina magari matatu na kadhalika, Je hizo hela wanatoa wapi just baada ya kujiunga na hilo kanisa tu maisha yanabadilika ghafla?! Na kwa bahati mbaya utakuta kila anayetoa ushuhuda anaeleza tremendous changes kwenye hali yake ya kiuchumi. Kwa nini hawaoneshi kwamba walifanya biashara gani na maisha kubadilika?
    Tunajua watu wanaweza kuchafuliwa sawa na huyu mkubwa naamini ni mmoja wa waliochafuliwa kwani siamini kama anaweza kuwa anadili na madawa. Ila naamini wapo wengi tu wanaotumia mianya ya dini zetu kujinufaisha na kutumia waumini kusambaza hayo maovu kutokaba na historia zao za kimaskini. Wanapoahidiwa donge nono na kutishiwa maisha endapo watatoa siri maisha yanaenda. Kwa hiyo naweza kumtetea Pengo lakini ukweli ni kwamba wapo viongozi wengi tu wanaotumia didni zetu kufanya maovu kama hayo.
    Mwaka 2009 kuna mchungaji alitaka kunitapeli kwa kujifanya ananitafutia scholarship mimi na rafiki yangu nilipomaliza form 6 lakini alipoanza kudai aanze kulipwa nikashtukia. Shame on them, Washindwe!!

    ReplyDelete
  5. MHASHAMU HUENDA KUNA DALILI DALILI ZA KUHUSIKA KWAKO. MBONA BASI HUJATUTAJIA ANAEKUZULIA? MCHUNGAJI MTIKILA KWA MIAKA MINGI AMEKEMEA MAOVU MBONA HAJAHUSISHWA NA MADAWA? TAFADHALI BWANA ASKOFU TUELEZE A TO Z, KAULI YAKO INABAKISHA MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU. MAJOHO YA MISIKITI NA MAKANISA YAMEKUMBWA NA ABUSE YA HALI YA JUU, SO MSIBABAISHE BABAISHE, KAMA SI WEWE BASI TWAMBIE NI NANI? MIMI SIJAONA HAYO MAOVU ULIYOFICHUA. WADAU SAMAHANI KAMA NIMEKUWA HARSH, NATUMIA UHURU WANGU WA KUTOA MAONI. Mdau, Ukerewe

    ReplyDelete
  6. Big Up anon wa Mon Jan 02,10:47:00 AM 2012 - Nakuunga mkono usemi wako.

    ReplyDelete
  7. Kardinari Pengo unaongea sana unapoteza muda kurumbana na walimwengu kama vile humjui Mungu au hujui kazi kuu za Mungu, kama binadamu wanakuzulia ingia katika maombi na novena umwombe Mungu na Mama Maria akusafishie njia na wabaya wako wauone usafi wako badala ya kupoteza muda kurumbana na dunia!

    Pia nakunukuu kwa kwa kusema huoni cha kustaajabisha kwa askari/komandoo kuvunja tofari kwa kichwa - haya hayakupasi wala hayakuhusu wewe kuongea hasa ukizingatia ni mtu mwenye nafasi na heshima katika taifa hili. Sasa hivi watu watakushusha thamani nakuanza kukudharau kwa kuonekana mtu wa porojo unaependa malumbano na kujihusisha na kila jambo livumalo.

    Omba hekima, busara na uongozi wa mwenyezi Mungu zaidi naona unapoteza dira sasa hivi.

    ReplyDelete
  8. baba sie si wa kukufundisha hekima wewe, tunaamini elimu yako na uzoefu umekufundisha mengi sana, basi tumia "silence is gold". ila kama wako wanaokuudhi waseme waziwazi mbele ya kadamnasi kama vile kwenda pale maelezo ukasema na kuulizwa na waandishi wa habari face to face. haya ya kuzungumza na vijana ufukweni yanaleta masuali mengi...

    ReplyDelete
  9. Binadamu hawana jema ukisema kosa ukinyamaza kosa.

    ReplyDelete
  10. Looh wa Bongo Mungu kawapa bongo big up Taifa letu asanteni kumsaidia Mkuu wa kanisa Pengo ameteleza wazungu wana sema usibishane na mpumbavu muelevu hato ona tofauti basi Kardinari usilumbane waombee wabaya hao na ombi lako zito usipite ufukweni kujiosha,kama una ushahidi ulio yasema nenda mahakamani wataje usiweke waumini njia panda hio inajenga chuki waumini wako wataona ni Waislamu wana kupakazia come clean

    ReplyDelete
  11. Mungu wetu wa rehema awasamehe kwa mawazo yako potovu.
    Mungu akulinde na hao wasiopenda kuona kanisa linasonga mbele kwa kusema ukweli.by rose

    ReplyDelete
  12. Kadinali naona umesahau kuwa pindi unapofungua mdomo heshima yako inakuwa hatiani. Mimi naona ungenyamaza ili kulinda heshima yako maana sasa imeshaanza kuingia matatani!! Kazi kweli kweli!!

    ReplyDelete
  13. kadinali ana haki ya kuongea kama kiongozi hamjuia huyu ni zaidi ya rais? mnaochangia mawazo yenu nafikiri wote ni waislam lakini sioni kosa aliloongea kadinali anahaki ya kutetea kwa sababu anaona tunavyopelekwa sio kuzuridi

    ReplyDelete
  14. I love yu anon wa Mon Jan 02,08:41:00 PM 2012

    ReplyDelete
  15. Anon wa Tue 03, 09;06;00 AM 2012 - Acha udini tafadhali tena ondoa mawazo potofu sasa kwa taarifa yako mie pia nimechangia hapo juu na ni MKRISTU na zaidi mie ni MKATOLIKI! - kwenye ukweli lazima tuseme tuache unafiki.

    ReplyDelete
  16. Ivi kina Prosper Minja nao waislamu eeh!? hapa Mhashamu katugusa wote bila kujali dini lazima tuseme kama anavurunda.

    ReplyDelete
  17. huyo ni rais wa wakatoliki na si zaidi ya rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, mimi ni mkistro na la sikubaliani na Pengo, mbona hatuweki wazi ni maovu gani aliyofichua? Pengo ana bwabwaja na kusahau kuwa yeye nani. anajishushia heshima yake. kwani nagekaa kimya ingekuwa nini huwezi kujisafisha kwa style hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...