Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi akiongea na waandishi wa habari mara bada ya kuwasili kwa ndege mpya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108.
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikata keki kusherekea ujio wa ndege ndege mpya aina ya Boeing 737-500. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakishuka katika ndege mpya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108. Ndege hiyo itaanza kuruka bada ya wiki moja.
Mmoja wa wafanyakazi wa ATCL akiwaamebeba ujumbe wa kumkaribisha Waziri Harisson Mwakyembe baada ya uteuzi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Wahudumu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakipozi mbele ya kamera ya blogu hii.
========= ===== ===
Ndege ya ATCL aina ya Boeing 737-500 kuanza safari baada ya kuwasili
NDEGE mpya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na Shirika la ndege la AIR Tanzania (ATCL) imewasili nchini wikiendi hii na itaanza safari za Dar-Mwanza-Kilimanjaro kabla ya kuanza safari za kimataifa, Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa ATCL Paul Chizi amesema.
Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 108 iliyokodishwa toka kwa kampuni ya Aero Vista Dubai, Chizi alisema kuwa ATCL itaanza safari zake katika kipindi cha wiki moja kuanzia sasa na kuonyesha uwezekano wa kuiunganisha Dar es Salaam na Dubai katika safari zake katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
“Watanzania watarajie huduma bora waliyoikosa kwa kipindi kirefu sasa. Tutarudisha safari zetu katika kipindi cha wiki moja. Tunaitaji watuunge mkono kama ilivyokawaida yao katika siku za nyuma.
“Huduma zetu ni za uhakika na ni kwa ajili ya wateja wetu. Muda ni kigezo chetu kikubwa katika kazi na sasa tunatarajia kutoa huduma kwa wakati lakini pia huduma zenye unafuu kwa wateja,” alisema.
Chizi alisema kuwa kampuni inatarajia kuungana kibiashara na makampuni ya kimataifa ya ndege katika lengo la kutanua safari zake lakini alisisitiza kuwa hali hiyo itakuwa na faida na matunda pande zote mbili.
“Kupitia muungano huo wa kibiashara, tutahakikisha kuwa kila mmoja anafaidika. Ambapo katika muungano huo kampuni inapokosa faida, daima muungano huo wa kibiashara hauwezi kudumu,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa ndege nyingine ya kampuni hiyo aina ya Dash 8 ambayo inafanyiwa matengenezo Terminal 1 nayo itakuwa tayari katika kipindi cha wiki sita zizajo na itasaidia kuboresha utoaji huduma zaidi wa kampuni hiyo.
Ndege mpya ya ATCL Boeing 737-500 imeshafanyiwa uchunguzi na timu ya wataalam kutoka katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Cairo nchini Misri na tayari hati ya kibali cha ufanyaji kazi wa ndege hiyo nchini kimeshatolewa.
Ndege hiyo iliyonakshiwa na rangi za shirika la ndege la ATCL inachukua abiria wapatao 12 katika daraja la kwanza (business class) pamoja na abiria 96 katika daraja la kawaida (economy class) ATCL hivi karibuni ilizindua tovuti katika lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja pamoja na kukuza ubora katika utendaji kazi wa shirika hilo la ndege la kitaifa.
Tovuti hiyo inawawezesha wateja kupata huduma za ukataji tiketi bila ya kufika katika ofisi za ATCL au kupitia mawakala na kuwasaidia wateja kutoa maoni yao kupitia mitandao ya kijamii.
Safi sana the wings of Kilimanjaro..sasa naweza kupumua kidogo.Nilikuwa naulizwa na rafiki zangu wa nje shirika letu la ndege nataja 'lile jingine'..aibu hey?.Hapa nacopy hii picha naenda 'kuwaonyesha'hee hee heee.
ReplyDeleteKukiwa na malengo ya dhati,shirika letu litanyanyuka..fanyeni kazi kwa bidii..be serious.ondoa ubabaishaji..nchi yetu ina vivutio vya watalii kila kona..Kila la kheri.
David V
Hao wahudumu picha ya chini wa siku nyingi sana..nilikuwa nawaona kwenye boeing zile zilizokuwa zinapiga kelele sana.Wahudumu wa ATCL wako 'fiti' kweli kwenye kazi basi tu ndege zenyewe hazipo.
ReplyDeleteDavid V
Nafikiri kinachofuata kingekuwa kupunguza wafanyakazi na kuwalipa stahi zao shirika lifanye kazi kibiashara nasi kutoa huduma ya ajira.
ReplyDeleteI tell you this man Mr Chizi, just doesn't talk the talk he actually walks the walk.....just just watch this space watanzania wenzagu big things are about to happen.
ReplyDeleteLooking forward to see Airtanzania ina Amsterdam ni utalii tosha kabisa so fanyeni kazi kwa bidii mashirika mengi yanwahitaji mkiwa wakweli na kufanya kazi kwa bidii mimi ni Abiria wenu toka miaaka ya nyuma najuwa mwanza yote mtawabeba sio kile kikampuni chenye share na mafisadi!!!
ReplyDeleteWatanzania karibu wote wanampongeza kaimu wa atcl Mr. Chizi kwa kuleta B737-500.
ReplyDeleteSasa hivi ajitahidi aitoe ndege iliyopo kwenye matengenezo ya check C haraka iwezekanavyo ili iendelee na huduma za Kigoma na Tabora na kujipatia pesa zake yenyewe.
HIVI HUYU NDO YULE CHIZI WALIOSEMA KAOKOTWA BARABARANI. DUH SASA NAAMINI KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU ILIHONGWA KWAKWELI. MTU ALIYEOKOTWA BARABARANI HAWEZI FANYA VITU VIZYRI HIVI. SERUKAMBA ITABIDI UJIHOJI MWENYEWE KAMA UNAFAA AU LAH!
ReplyDeleteATCL:
ReplyDeleteLingine la zaidi ni kutoa IPO (Initial Public Offering) ili kupata pesa za Hisa kuweza kununua Madege yenye maana badala ya kukodi.
Nchi zingine masikini ambazo hazina rasilimali kama sisi (mfano Rwanda ambao Uchumi waounategemea kilimo cha majani ya chai na Maua ya Mapambo) wameweza kuagiza Ndege kadhaa tena 'mpya' kabisa na bado wanategemea kuagiza zingine nyingi mpya kutoka kiwandani!
Sembuse sisi wenye kila kitu mfano:
1-Almasi
2-Dhahabu
3-Urani (Uranium)
4-Gesi
5-Coal (Makaa ya mawe)
6-Bahari zenye mazao kibao na Misitu yenye wanyama kibao,
Na upuku puku wa mali na utitiri wa rasilimali.
Sisi tunaweza kuwa na Shirika lenye uzito mkubwa sana ktk Afrika ya Mashariki na maeneo jirani kama tutatumia tulicho nacho vema na kuacha Mabilioni ya Fedha za mali yakivunwa na kugawana Mafisadi!
Corporate colour ya ATC ni ipi?. Angalia rangi za ndege na rangi za wahudumu!
ReplyDeleteDavid K
Siafiki suala la kukodi ndege, ni ghali mno. Kwa nini tusiagize na kununua ndege zetu wenyewe kutoka kampuni za Boeing na airbus?
ReplyDelete