Waziri wa Maliasili na utalii Mh. Khamisi Kagasheki (wa tatu kushoto mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wadau wa utalii katika sekta binafsi na baadhi ya viongozi wa wizara mara baada ya kukutana nao kwa mazungumzo hivi karibuni katika hoteli ya serena jijini Dar es salaam.
Wadau wa utalii katika sekta Binafsi wameiomba serikali kuongeza bajeti ya utangazaji utalii kwa Bodi ya Utalii Tanzania – TTB ili kukiwezesha chombo hicho kumudu ushindani na kuitangaza vema Tanzania kote duniani kwani bajeti inayotolewa ni ndogo isiyokidhi vema shughuli za utangazaji ambazo ni ghali sana.
Aidha Wamesifu na kuipongeza Bodi ya Utalii Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inayotoa kwao katika suala zima la kuitangaza nchi yetu katika sekta ya utalii na kusifu pia juhudi za Bodi katika kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi licha bajeti ndogo inayotolewa na Serikali.
Kauli hizo zimetolewa na wadau hao wakati walipokutana na Waziri wa Maliasilina Utalii Mheshimiwa Khamis Kagasheki katika chakula cha jioni alichokiandaa kwa wadau haokatika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam hivi karibuni kwa lengo la kukutana na kufahamaina nao.
Wakitolea mfano wa namna wanavyoshirikiana na Bodi ya utalii mbali ya kushiriki pamoja na katika maonesho na misafara mbalimbali ya utangazaji utalii duniani inayoratibiwa na Bodi, lakini pia wanashiriki katika kuandaa mikakati ya kuitangaza nchi.
“Tunashukuru kuwa hivi sasa sisi kwa kushirikiana na TTB tuko katika mchakato wa kukamilisha mpango mkakati wa kuitangaza Tanzania” alisema Katibu Mtendaji wa TCT Bw. Richard Rugimbana.
Katika hafla hiyo Waziri alisikiliza matatizo mbalimbali yanayowakabili wadau hao wa utalii na kwa pamoja kujadiliana namna gani bora ya kukabiliana na changamoto hizo. Aidha Mheshimiwa Waziri alifahamishwa pia kuhusu mikakati kadhaa iliyowekwa ana wadau hao katika kuinua na kuboresha huduma wanazotoa kwa watalii.
Waziri ambaye alitoa majibu kwa hoja nyingi zilizojitokeza wakati wa mazungumzo hayo aliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa kwa lengo la kuboresha na kuendeleza sekta ya utalii na akawahakikishia kuwa wizara yake itaendelea kushirikiana kwa karibu sana na wadau hao wa utalii kutoka sekta binafsi kwa kuwa wana mchango mkubwa sana katika sekta ya utalii .
“Ninyi ndio watu mnaotoa huduma kwa watalii katika nyanja mbambali hivyo mna mchango mkubwa sana katika maendeleo ya utalii hapa nchini, nawaahidi kuwa wizara itaendelea kutoa ushikiano mkubwa kwenu” alisema waziri Kagasheki
Hii ni mara ya kwanza waziri Kagasheki kukutana na wadau hao toka ateuliwe kuiongoza Wizara ya Maliasili na Utalii na ametaka kuwepo kwa mikutano ya namna hiyo mara kwa mara kwa lengo la kuendelea kubadilisha msawazo zaidi.
The problem isn't the budget it's the fact that their advertising strategy is all wrong .first they must come up with a feasible strategy that will ensure maximum exposure of the country and create the necessary awareness secondly they must look into the the fact that it's too expensive in Tanzania that is why the tourists opts for the southern Africa countries and Kenya in east Africa.
ReplyDeleteSip kuongezewa budget.
Mkereketwa.