1. Ninamuomba manani, tuidumishe
amani
Tusipate tafurani,
kuipoteza amani
Utujarie imani, tusifanye
yakihuni
Utuongoze manani
tuidumishe amani
2. Amani iwe motoni, tusiibebe
kichwani
Tena ikae tumboni,
wasiione jirani
Wao wanaitamani, kwao
haipatikani
Utuongoze manani
tuidumishe amani
3.
Mashekhe misikitini, Makasisi
kanisani
Waumini waambieni, madhara
yake ni nini
Amani haipatikani,
ipoteapo nchini
Utuongoze manani
tuidumishe amani
4.
Amani bidhaa gani, kwa pesa
haipatikani
Dukani hata sokoni, dola
za marekani
Yeni pia za Japani, Euro
za Kijerumani
Utuongoze manani
tuidumishe amani
5.
Tukipoteza amani, tutakuwa watu
gani
Hatusomi kwa jirani,
wanaishi ugenini
Nani atakuthamini kwenu
hakujulikani
Utuongoze manani
tusipoteze amani
6.
Unapoteza Amani, Kwa simu ya
mkononi
Vocha atakupa nani,
waonekana muhuni
Unaishi vichakani, roho
iko mikononi
Utuongoze manani
tusipoteze amani
7.
Tukumbuke majirani, wamejaa
Marekani,
Kwao wanakutamani, lakini
haiwezekani
Kuishi ukimbizini, upate
faida gani
Utuongoze manani
tusipoteze amani
8.
Kuikamata sukani, ndicho chenye
thamani
Wakujue ni rubani,
utakapokaa kitini
Ujulikane ni nani, umetua
baharini
Utuongoze manani
tusipoteze amani
9.
Maisha yetu zamani, kwetu
hatuna kifani
Japo kuwa ni mgeni,
hatumuweki pembeni
Utapewa biriani, tena
katika sahani
Utuongoze manani tusipoteze
amani
10.
Tunakuomba Rahamani, Zidisha
yetu imani
Tukeshe misikitini, pamwe
na makanisani
Utujazie imani, tuishi
kama zamani
Utuongoze manani
tusipoteze amani
11.
Kwaherini kwaheri, tukijaliwa
mwakani
Yangu haya yashikeni,
tusiwe kama manyani
Aingiapo shambani, hata
huruma haoni
Utuongoze manani
tusipoteze amani
Mimi Mpenda Amani
Bi. Tunguri Rajab Tambwe
Dar Es Salaam, Machi 2013.
Bi.Tunguri Rajabu Tambwe ni mtoto wa pili wa Mshairi wa zamani Enzi za akina Amri Abeid na Mzee Saadan Kandoro. Huwa anaandika mashairi ambayo yanatumika zaidi ndani ya familia. lakini hili hapa ni kwa watanzania wote. Bi Tunguri Rajab Tambwe alizaliwa tarehe 17 April 1945, mkoani Mbeya.


AMANI NCHINI TANZANIA:
ReplyDeleteNi wazi wapo waliopoma ya pazia wasioitakia mema nchi yetu, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo Siasa na Itikadi za KiDini.
HATUKUBALI KUCHEZEWA NA KUYUMBISHWA NA MAGENGE HAYA MACHACHE YA WATU WANAOHESABIKA YANAYOTAKA TUINGIE KTK MISUKO SUKO YA KIMAISHA NA MUSTAKABALI ILI WAO WAFIKIE MALENGO YAO MACHAFU!
TUTAILINDA AMANI KWA GHARAMA YEYOTE ILE HATA KWA MTUTU WA BUNDUKI!!!
Nakushukuru mwanetu,Kutupa yako maoni
ReplyDeleteAmani ni kila kitu, kwa ustawi makini
Bora kula kidogo tu,na ulale kuvulini
Nasisitiza kiutu, Amani ikumbatienie
Namuunaga mkono kwa maoni ya kweli. Mimi niliwahi kuwahudumia wakimbizi wa nchi fulani miaka ya siombi hata siku moja kuwa mkimbizi. Ukikaa nao utaona ni jinsi gani wanaumia kwa hali walizonazo. Nina mengi ya kuongea kuhusu amani ila yanahitaji muda.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Unanikumbusha zamani sana wakati kabla ya simu za kiganjani na facebook.
ReplyDeleteAmani ni tunu ni vyemakuienzi
ReplyDeleteTuenzi majumbani ,nabarabarani pia
Tuepuke ushabiki,Wa kuingizwa mitegoni
Yarabi tunakuimidi,tupe upeo tuieshimu amani
Bi Tunguri shikamoo, Asante kwa lako shairi
ReplyDeleteMimi pia niwapo, kuepusha hiyo shari
Sote tujue tupo katika hali ya hari
Mungu tujaliepo, Tanzania yetu shwari
Hakika kweli wapo, wanaotamani ushari
Bila kufikiri iwapo, Amani hii itaghairi
Wao wale kiapo, tena wao waghairi
Mungu tujaliepo, Tanzania yetu shwari
Kama kuna kichapo, basi wapewe bahari
Ndicho kiwatoshapo, kwa kutaka shari
Wengine huko hatupo, hata kupewa dinari
Mungu tujaliepo, Tanzania yetu shwari
Tamati sasa nifikapo, salaamu zangu ni heri
Niwasalimu na wapo, wa mbali kwa buheri
Karibuni sote tupo, Tanzania yenye heri
Mungu tujaliepo, Tanzania yetu shwari
Selina
Potelea mbali!
ReplyDeleteAcha dunia ituelewe itakavyo tuelewa hatuna jinsi.
Tumesha watambua (TUNA WAFAHAMU VIZURI TU) wanao hatarisha amani nchini, TUNAWEZA KUWACHINJIALIA MBALI HAO WATU WASIOZIDI 200,000(LAKI MBILI) ili tuweze kunusuru Taifa la watu 45 Mil.!
Dunia imeshuhudia mahala popote penye Jitihada za Kupiga hatua hapa kosekani Wapinga maendeleo hata kama atakuwa mtu mmoja tu.
ReplyDelete''MFANO HAI NI YOMBA YOMBA KTK SINEMA MOJA YA ZAMANI HAPA TANZANIA, WATU KIJIJINI WALIKUWA WANANIA YA KUFANYA KAZI ZA KULETA MAENDELEO LAKINI YEYE AKAWA MPINGAJI MKUWA''
Nchi mbali mbali duniani zili hakikisha Dira inafikiwa Mifano:
1.ITALIA:
Iliuwa MAFASHISTI kadhaa waliokuwa wapinga maendeleo ili Dola isimame.
2.UFARANSA:
Ililazimika kuuwa MABEBERU wachache wapinga maendeleo ili wasonge mbele.
3.UINGEREZA:
Ilihakikisha MABWENYENYE wapinga maendeleo wanatokomea na kuacha Mabwenyenye wachache wenye faida ili wasonge mbele.
4.JAPAN:
Iliangamiza MADIKTETA wote ili isonge mbele.
5.URUSI:
Iliwaangamiza MAKABAILA wote ili isonge mbele.
Hivyo safari ya kuelekea kwenye AMANI iliyodumu ina mabonde na milima ambayo pana hitajika maamuzi magumu KAMA MNAVYOONA KTK MIFANO HIYO HAPO MITANO (5) JUU, UKIWEPO MFANO WA KUBWA LAO HAPA HAPA TANZANIA YOMBAYOMBA NA UPINZANI WAKE KIJIJINI KWAO ili kufikia malengo kwa faida ya walio wengi!
Amani yetu ni tunu, isiyokuwa kifani
ReplyDeleteidumu na zetu mbinu, pasipo na tafurani
Wachochezi kama kinu, hutwanga na kurubuni
Vurugu kwao kicheko, amani kwao ni kero.
Tuilinde amani yetu kwa mbinde na kwa upinde!
AMANI IDUMU (MKAZO)
ReplyDeleteShkamoo Bi Tunguri, mwanao kuniitika,
Hongera shairi zuri, vina mizani pangika,
Ujumbe ni 'santuri', sokoni umeuzika,
TUIDUMISHE AMANI, NCHI DUNIA ZUNGUKA.
AMANI tia mkazo, chonde isije toweka,
Ikajazuka mizozo, na vilio hasikika,
Kwetu kubwa yetu nguzo, nguvu zote meishika,
TUIDUMISHE AMANI, NCHI DUNIA ZUNGUKA.
AMANI tuidumishe, hilo sifanye dhihaka,
Dua na sala tukeshe, tataqabali RABUKA,
Mitafaruku iishe, popote ilipozuka,
TUIDUMISHE AMANI, NCHI DUNIA ZUNGUKA.
AMANI mithili jua, nuruye kote itaka,
Sijegeuka mvua, jibanza hahangaika,
Ama gharika ikawa, hajakosa pa kushika,
TUIDUMISHE AMANI, NCHI DUNIA ZUNGUKA.
AMANI ni malighafi, kuitunza inataka,
Kiidumisha haifi, kuienzi ni baraka,
Ndipo huwa mambo safi, ndani nje hasifika,
TUIDUMISHE AMANI, NCHI DUNIA ZUNGUKA.
AMANI tuombe Mungu, nchi yote kuzunguka,
Itande mithili wingu, kama radi kusikika,
Tuwe mbali na machungu, tafrani sijezuka,
TUIDUMISHE AMANI, NCHI DUNIA ZUNGUKA.
AMANI iwe kioo, jitazama tukicheka,
Pasi waita njoo, wengi kwetu tafurika,
Hapa na pale masoo, na mengi yatatwepuka,
TUIDUMISHE AMANI, NCHI DUNIA ZUNGUKA.
Namaliza wasalamu, kidoto hapa naweka,
Sichoki omba RAHIMU, sifa zote lojitwika,
AMANI daima dumu, ulimwengu kuzunguka,
TUIDUMISHE AMANI, NCHI DUNIA ZUNGUKA.
asante binti Tambwe
ReplyDeleteukiweza kuniandikia email , nitafurahi
mimi mu omani , nilizaliwa Urambo
namjua mzee marehemu Rajabu tambwe
saeedmarjiby@hotmail.com
00968 99813400
Amani
ReplyDeleteAmani shika hatamu, vurugu kwetu haramu,
Na sisi tuwe na hamu, kuishi kwa ufahamu,
Amani na ukarimu, isiwe ni ya msimu,
Asante bi Tunguri, kwa hilo lako shairi
Twaomba tunga lingine, elimu na izagae
Hakuna nchi nyingine, hapana tutapakae
Amani na si jingine, fujo na isisambae
Asante bi Tunguri, kwa hilo lako shairi
Asante Bwana Michuzi, kwa huo wako uwanja
Malenga wana ujuzi, fujo haina mjanja
Likivunda ni la juzi, si la udi wala ganja
Asante bi Tunguri, kwa hilo lako shairi
Tanzania ndipo kwetu, katu hatuna kwingine
Tuiliinde nchi yetu, na wala si vingine
Wachochezi si wenzetu, maadui pande nne
Asante bi Tunguri, kwa hilo lako shairi
Dar Es Salaam, 16th June 2013. A.P.M