Na Shaffie Dauda

Mabingwa wastaafu wa soka  Tanzania bara, Smba SC imetangaza kuwa haitashiriki katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, ikiwa itaandaliwa katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia mjadala ulioibuka katika bunge la Tanzania baada ya waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benard Membe kuhoji hali ya Usalama katika eneo hilo.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema uongozi wa CECAFA ni sharti ubadilishe mahala 
pa fainali hizo la sivyo wao hawatashiriki: ''Hatuwezi kwenda Darfur kuvalia (bullet proof) mavazi yasiyopenya risasi,'' alisema Rage na kuongeza: ''Ni wazi kuwa hali ya usalama katika eneo hilo sio nzuri kama ilivyothibitishwa na serikali.''

Membe aliliambia bunge la Tanzania kuwa alishangazwa sana na uamuzi wa kuandaa fainali hizo katika eneo la Darfur ambalo limekubwa na mapigano ya mara kwa mara. Membe amesema serikali ya Tanzania, inachunguza hali ilivyo na kuwa watachukua uamuzi muafaka kuhusiana na suala hilo.

''Hatuwezi kuwatuma vijana wetu katika eneo ambalo hatuna hakikisho la Usalama,'' alisema Membe.

Mabingwa watetezi Yanga, vile vile kutoka Tanzania ambao walikuwa wameonyesha nia ya kushiriki katika fainali hizo za Darfur, pia nao wanasema watafuata ushauri kutoka Serikalini.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la mchezo wa soka nchini Tanzania, TFF, Angetile Osiah, amesema wao wamehakikishiwa usalama na eneo watakalopiga kambi wakati wa mashindano hayo.

Endapo timu hizo mbili kutoka Tanzania zitajiondoa kutoka kwa fainali hizo, itakuwa pigo kubwa kwa waandalizi wa mashindano hayo.

Timu mbili kubwa nchini Sudan Al Hilal na Al Merreikh tayari zimethibitisha kuwa hazitashiriki kutokana na hofu za kiusalama.

Katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amekariri kuwa eneo hilo la Darfur ni salama kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2013

    HIVI KUSTAAFU NI LUGHA GANI?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2013

    Kiswahili ikimaanisha 'to retire' ndio unajifuna lugha au? itabidi ununue kamusi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2013

    Duh! Hapo Rage alikuwa anaekea wapi?. Naona mguu wa kuku umetuna kiunoni kipande ya kulia!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2013

    Huyo bwana kilichotuna ndani ya t shirt kwenye usawa wa kiuno kulia kwake ni nini?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2013

    Mimi Mwenyekiti wa Timu na Raisi wa Mpira wa Timu ninacheza Namba ngapi Uwanjani hadi nistaafu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2013

    Ama kweli tumegawanyika kimichezo !

    Kumbe Mhe. Mama Tibaijuka na wewe ni Mwana Msimbazi?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2013

    Ohhh!

    Mara zoooote nilikuwa nikiamini ya kuwa Mkoa wa Kagera ni Wana Yanga damu kumbe sio?

    1.Juma Mukambi I fwantasitiki Boyi thirii pozisheni kwa wakati imwe!

    2.Aywi tata Baba Isaya Feliksi Minziro Kataraiya kugenda ku goal!

    3.Ywi tata I Feliksi Minziro Umushaija winning the goals!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2013

    huyo ni mexican RODEO lazima awe ni hicho kiunoni.(soma kofia)
    msomali ni msomali tu!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2013

    Mama Tibaijuka kumbe mcheza kabumbu mzuri. Lakini hebu chunga upande wako wa kushoto usawa wa kiuno kuna kitu kimetuna pale.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...