Bwana michuzi nashukuru sana kwa kazi yako ya kutuelimisha na kutujulisha kwa mambo yanayotekea nyumbani nashukuru pia kwa kuweza kutuwekea hoja kubwa kama hii katika mtandao na kutupa uwanja wa kuweza kuchangia maoni yetu katika kupata katiba ambayo itakuwa ni ngao ya watanzania wa bara na visiwani,

Ni kweli muungano umetuletea mambo mazuri mengi na kunamambo ambayo ukiangalia kwa kirefu au kwa upana unaona kuna makosa ambayo yanaweza kutatuliwa na watu wanaoipenda Tanzania (maana yake naposema hivi kuna vibaraka wanaotumiwa na watu kutoka nchi za nje ili kuvunja muungano huu hau kuigawanya nchi kwa makabira na kwa dini)
Wa Tanzania kubomoa ni rahisi na kujenga siyo mchezo ndugu zangu tukumbuke kitukimoja sisi kama waafrica tumetawailiwa na waarabu wariotoka makwao tumetawaliwa na wazungu walio toka makwao na kutufanya watumwa na kuuwa mababu zetu waliokuwa wakitembea maili na maili na kutufanya sisi ni mbwa na leo hii hayo yote tuna aanza kuyasahau na kutaka kurudi katika ukoloni wa mambo leo,
Ndugu zangu tukumbuke haya yote na damu za mababu zetu kutokea mwanza,kigoma,tabora,songea, tanga manyema congo,na ungunja,pemba, na mikoa yote ya TANZANIA,Damu iliyomwangika isije ikapoteabure tukumbuke tunapotoka ndio tupate katiba yenye utaifa, ni mazuri ghani yaliyopo kwenye katiba ya zamani? na mambo ghani ambayo hayafai kwenye katiba hiyo ya zamani,
je mfumowa serikali mbili unafaa au vipi? au serikari tatu? au tuwe na serikali moja tuu na nchi iwe na state maana yake itakuwa inaitwa UNITED STATE OF TANZANIA and tuwe na Raisi ,makamu waRaisi na Waziri mkuu ?ndugu zangu kwanza hapa shida siyo serikari tatu au mbili au moja shida ni moja tuu ambayo inarudisha maendeleo nyuma na kufanya asilmia karibu 65 ya waTanzania kubaki masikini na kuendelea kuwa masikini,Tatitizo ni hili hapa ni Good governance, Responsibility.Acountabilty, Deliverance and good economic policies.nakingine ni hiki agenda ya Tanzania au Manifesto ya Tanzania iko wapi wakati wa mwalimu ilikuwa ni ujamaa wa kujitegemea je sasa hivi nini?
kwa upande wangu kutokana na nchi yetu kuwa bado ni maskini hatuwezi kuwa na serikari tatu uendeshaji wake utakuwa ni wagharama na pila atuwezi kuwa na maraisi watatu,maoni yangu yako very simple ningependa tuwe na serikali moja tuu maana yangu mimi sijui kuna nchi inaitwa Tanganyika au Zanzibar kitu nachojuwa ni kwamba nchiziliungana na kutengeneza au kuzaa taifa linaloitwa Tanzania,
kwa maana yangu au kuelewa kwangu ni kwamba tunapashwa kuwa serikali moja ambayo itakuwa na Raisi na makamu wake na waziri mkuu,
baadala ya ya kuwa na mikoa tuwe na state na hizi state zitakuwa chini ya serikali ya katikati au central,
hizi state zitakuwa na Katikiro natumia jina la kiafrika ambaye hatakuwa anachaguliwa na wananchi na kazi zake ni kuwatumikia wananchi na kuhakikisha hanatimiza mipango yote ya serikali kwa uhakika na bila mchezo na muda wake wa kufanya kazi ni miaka kumi mitano,na mitano kama hatachaguliwa na wananchi tena.
Raisi hatachaguwa Governor ambaye kazi yake ni kuangalia mambo ya utendaji wa sela za serikali yani sera za nchi siyo za chama na kazi ya usalama yaani ataitwa Overseer na hii ndiyo itakuwa kazi yake tu na anaweza kuongezewa majukumu mengine,
Jee hizi state zitaendeshwa vipi zitakuwa zinakusanya mapato na asilimia 37 yawe yanabaki kwenye state na asilimia 63 yanaenda kwenye Central government na tuwe na mawaziri wa kuitumikia nchi moja na na tuwe na bunge moja tu lenye wabunge 250 wabunge 70 kutoka visiwani na wabunge 180 kutoka bara na tuwe na bunge la wezee au nyumba ya juu amabayo itakuwa na wazee 50 tuu ambayo itakuwa na wawakilishi wa dini waislam2,wakristu2,wahindu2, wazee wetu wa au wakuu wa chief2,nafasi zilizi baki watachuguliwa na bunge na kuteuliwa na raisi yaani retired jaji,police,wakuu wa majeshi,doctors,Raisi, mawaziri,na kiwango cha umri ni kuanzia miaka 60.
Pamaoja na haya yoteniliyosema bado tutakuwa pale pale kama hatutaweza kuwa na agenda au manifesto ya nchi siyo ya CCM,au CHADEMA ,au CAF,DP,auTLP ni mengi ya kusema hapa lakini naona kwanza ni achihe hapo kwenye swala la serikari moja,
Je kuhusu serikali mbili ni vipi? Kama tutaendela kuwa na serikali mbili je nini kinachotakiwa kufanywa sababu visiwani kunaonekana kwake mpaka sasa inaonekana kama ni nchi ndani ya muungano iko na bendera,iko na wimbo wa taifa, lakini bara hakuna wimbo wala bendera kw upande wangu tungeweza kujifunza kwa wenzetu wa hapa uingereza wako na nchi nne ndani ya muungano wa united kingdom, je nini ambacho tunacho weza kujifunza kutoka kwao au tunaweza kijifunza nini kutoka kwa hawa jamaa wa united emirates
Ndungu zangu ningependa sana hoja hii tuichambuhe kwa makini na kwa kirefu kutokana na historia yetu na tunapotoka sababu naamini Tanzania ya leo iko na wasomi wengi na wenye vipaji naomba sana tufunguke tuwe wazi tutoe maoni kwakirefu
Natanguliza shukrani kwa bwana Mchuzi na kwa waTanzania wote watako soma maoni yangu au kuchangia maoni yetu
Asanteni sana
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRICA
MDAU YUSEF
Una mawazo mazuri ndugu Yusef,suala hapa ni kwamba mawazo yako yatafikaje kwa viongozi wetu?.Ankal print hii mpelekee mkuu asome."Mwanadamu aliumbwa kusolve problems na siyo kucreate problems...'(Mbunge mmoja aliongea kwenye bunge lililoisha majuzi)
ReplyDeleteDavid V
Serikali tatu inawezekana kama zitapangwa vizuri. Hoja ya gharama kubwa haizuii kuwa na mfumo wa serikali tatu!
ReplyDeleteHoja zako hazina masshiko tunahitaji muungano wa usawa. Znz daima
ReplyDeleteMdau wa 3 hapo juu:
ReplyDelete'''Hoja zako hazina masshiko tunahitaji muungano wa usawa. Znz daima'''
Hakuna kitu kama hicho, kwa kuwa Uwiano ni lazima uzingatiwe popote penye Muungano hata iwe kwenye Matokeo ya Uchaguzi wa Kidemokrasia MWENYE KURA NYINGI (YAANI UWIANO WA JUU) NDIYE MSHINDIA AMA MWENYE KIPAUMBELE HATA AWE NA KURA MOJA ZAIDI.
HIVYO KTK SUALA LA VISIWANI NA BARA HAIINGII AKILINI KILA KITU IKAWA SAWA BARA NA VISIWANI.
KAMA YULE BWEGE MMOJA WA UINGEREZA JANA ALITOA MAONI KWENYE MAKALA HAYA HAYA AKISEMA ZANZIBARI INAHITAJI MGAWO WA 50 KWA 50 KTK KILA KITU, HILI HALIWEZEKANI.
DUNIA NA JUMUIYA YA KIMATAIFA NA WASHIRIKA WA KIMAENDELEO HAWAWEZI KUKUBALIANA NA MAHESABU YA MCHAMBAWIMA-ZANZIBAR KAMA HAYO!
Mfano:
1.IDADI YA VITI HAIWEZEKANI ZANZIBARI NA BARA ZIGAWANE 50 KWA 50.
2.MAPATO YAGAWANWE 50 KWA 50 BARA NA VISIWANI.
3.MISAADA IGAWANWE 50 KWA 50 BARA NA VISIWANI.
HAYO YAKAKUWA NI MAHESABU YA ABUNUWASI, HATA WASHIRIKA WA KIMAENDELEO MFANO WORLD BANK, IMF NA UN NA JUMUIYA YA KIMATAIFA HAWAWEZEZI KUWAKUBALIA MADAI YENU HAYA YA KIPUUZI NA YASIYOZINGATIA MANTIKI YA KIUSOMI.
WAZANZIBARI MNAOTOA MADAI MTOE MADAI MKIWA NA AKILI TIMAMU!
Wazanzibari msilete Siasa za kutaka muwekwe kama 'Special Citizens' hapa ktk Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
ReplyDeleteMsifikiri mtakuwa mnapewa kipaumbele kwa kila mnachotaka.
Mtegemee Muungano ulio kuwa na Fair Play, na sio kuwaweka ninyi Watu wa Visiwani kuwa juu ya Watu wa Bara.
Ninyi kuwa 'Special Citizens' ili iweje?
tuachane na dhana za ubara na uvisiwani, uzanzibari na utanganyika. dhana hizo zinaleta mivutano na ndiyo chanzo cha muungano wetu kuyumba.
ReplyDeleteSuala la Serikali moja hata mimi ni wimbo wangu wa kila siku.
ReplyDeleteMtazamo wangu uko hivi.
-Kuwe na serikali moja tu yenye Rais moja tu ambaye atagombea Urais huo kama mtanzania halali kutoka kokote kule haijalishi anatokea Zanz au Tanganyika.
-Tawala nyingine nyingine zibaki chini ya wakuu wa mikoa na wilaya kama ilivyo sasa kuanzia Zanz hata Tanganyika. Kwa kifupi, Visiwa vya Zanz visitofautiane na vya Ukerewe kiutwala na mgwanyo wa rasilimali. Kinachotakiwa bajeti iende kwenye halmashauri husika kwa usawa kulingana na waizara ya fedha ilivyo panga kulingana na mahitaji ya eneo husika.
-Naungana na Bwn Yusef ktk suala la uundaji wa States/Centrals, lkn kwa kuwa mwaka 2015 tutakuwa na Rais mpya ambaye hajawahi kukalia kiti hicho; ingefaa mchakato wa kuunda Centrals ungeanza 2017-2018.
Lengo ni kumpa Rais mpya muda mzuri wa kupata uzoefu, kujipanga na kufanya maandalizi ya kutosha ya kiutawala.
-Tukiwa na Serikali moja hatutaitana tena WAO na SISI, kwani hakutakuwa na nchi mbili zilizounganishwa, bali nchi moja.
-Kwa mtazamo wangu naona, Serikali moja ni suluhisho la migogoro mingi sana ya muungano na mgawanyo wa rasilimali Tanzania.
---------------
Abel A. Kingiya
0784 248 121
ukweli ni kwamba sisi wazanzibari walio wengi hatutaki tena muungano , na hilo sio jipya katika maisha ya kibinadamu , hata mke na mume ambao huwa wameoana kwa mapenzi ikifika muda hawaelewani basi hupeana talaka kwa amani , tafadhalini mtuachie nchi yetu tujiendeleze wenyewe, tutashirikiana kwa namna nyengine lakini sio kikatiba wala kiserikali kwa sababu tumeshachanganya damu tayari.
ReplyDeleteMoja kwa moja napinga kuwa na serikali tatu.Hizo mbili hatuwezi,je hizo tatu tutazimudu?
ReplyDeleteKuna maswala mengi yatatuchanganya, hatutajua tuyapeleke au tuyatatue kwenye serikari ipi...Hivyo kwa maoni yangu tupitishe referendum kupata maoni ya Watanzania wanamsimamo ghani kuhusu huu muungano kwa ujumla.Tujifunze ni jinsi gani muungano wa Ulaya (European Union)unaendeshwa endeshwa vipi,na pia toka USA Federal governments governance structure,Vilevile tujifunze kwa nini USSR ilivunjika?.Yote hayo tuyachambue tupate government system yetu.
Tusifanye haraka au kuchelewa sana kutatua hili tatizo la muungano kwani muda wa kutatua hili tatizo umeiva!..muungano mbaya au muugano wa kulazimishwa is a timed bomb.
Baadhi ya desturi za kiafrika ni kulazimisha kuoa au kuolewa;hapa sioni ajabu kwa hao wanaolazimisha kuwepo kwa kwani mentalitet na tabia ya kulazimisha mambo yako kwenye damu zao.
ReplyDeleteMuungano uvunjike kwani hakuna haja ya kung ang aniza kuwepo kwa muungano wakati Wazanzibar wengi hawataki.Ni afadhali kuwa majirani wema kuliko kuwa maadui kwenye nyumba moja.
Kila mtu anauwezo wa kutoa maoni anayofikiria kwa kutegema vile yeye anavyoona mimi kama mzanzibari wa damu ninaishi ujerumani nimesoma maoni ya bwana yusef ni maoni mazuri sana sana ni maoni ya mtu anayeangalia mbali na sio karibu kuwa na serikali moja ndio kutatatuwa matatizo mengi yaliyomo katika huu muungano,na pia kuna namna nyingine ya kuweza kutatua kero ya muungano kwa kuwa kujaribu kujifunza kwa wenzetu wa uk,usa,au hapa Ujerumani au UAE kama bwana yusef alivyosema ,je viongozi wa bara na visiwani wako tayari kuangalia utaifa wa Tanzania badala ya kutanguliza vyama vyao vya siasa?je wako tayari kuangali kwamba maendeleo ya nchi yanakuja baada ya kuwa na msingi imara na msingi wenyewe ni katiba namweomba bwana yusef kama ataweza kutuandikia tena maoni yake kuhusu muungano wa serikali 2 au yuko na maoni ghani tofauti ili nasi tunaofatilia tuweze kutowa yetu ya moyoni,
ReplyDeleteBwana michuzi unaweza kuyasukuma maoni ya huyu bwana yusef kwenye Radio au magazeti ya TANZANIA AU KWENYE BLOG THE VYAMA VYA SIASA NAO WATOWE MAONI YAO PIA
ASANTE
HUSENI BIN JUMA