Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi kitita cha kuhamasisha ulishaji bora wa watoto katika jamii kwa kukata utepe wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 7.8.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia waalikwa na wananchi wa Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani.yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 7.8.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahi alipokutana na mtoto Muktar Abdul mwenye umri wa miezi sita akiwa na mama yake Lucia Lingwanda, mkazi wa Chanika, wilayani Ilala, wakati Mama Salma alipotembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya unyonyeshaji duniani katika sherehe zilizofanyika Mnazi Mmoja tarehe 7.8.2013.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika Mnazi Mmoja na kufungwa rasmi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 7.8.2013.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...