Na Mwandishi Wetu
Sekta ya pamba nchini ina uwezo wa kuwakwamua wakulima wa pamba katika dimbwi la umaskini endapo serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wataweza kusaidia uwepo kilimo cha mkataba nchini.
Akiongea na vyombo vya habari hivi karibu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Gabriel Mwalo, alisema kuna faida nyingi katika kilimo cha mkataba lakini kukosekana kwa usimamiaji mzuri pamoja na ukosefu wa uungwaji mkono wa kutosha kutoka Serikalini kunawafanya wawekezaji kutochangia fedha nyingi zinazohitajika katika mfumo.
Sasa wakati umefika kwa Serikali kuyaangalia matatizo yanayokwamisha kilimo cha mkataba na mkazo uwekwe kwenye uzalishaji wa pamba pasiwepo ucheleweshaji wa utekelezaji wa sera ya Serikali,” Bw. Mwalo alisema.
Kilimo cha mkataba ndio kilimo gani hicho?
ReplyDeleteWabunifu ni wengi pale ubunifu unapokuwa ni kuwatizamia. Kilimo cha mkataba nao ni ubunifu. Hilo nalo neno. Utasikia hiyo ndiyo sera siku si nyingi.
ReplyDeleteKilimo cha Mkataba ni utaratibu wa kuishirikiana kati ya mkulima wa zao husika na mnunuzi ambapo mnunuzi anaingia katika makubaliano ya kisheria na mkulima ili amsaidie kuzalisha zao ambalo yeye atakuja kulinunua.
ReplyDeleteKwa hiyo kimsingi ni mkataba wa kuzalisha zao na kuuziana kati ya mkulima na mnunuzi. Wajibu wa msingi wa mnunuzi katika makubaliano haya ni kumsaidia mkulima kuzalisha kwa kumpa pembejeo mkulima kwa mkopo na wakati mwingine hata kumlimia na wajibu wa msingi wa mkulima ni kumuuzia zao huyu mnunuzi na kumlipa deni mla pembejeo alizokopeshwa wakati wa kumuuzia zao ( kwa kumkata kutoka katika mauzo ya zao) Lakini jambo muhimu makubaliano haya yanasajiliwa kisheria