Windhoek ni mji mkuu wa Jamhuri ya Namibia, upo katikati ya nchi hiyo
katika miinuko ya Khomas, kiasi cha mita 1,700 kutoka usawa wa bahari. Idadi ya
wakazi wake katika mwaka 2012 ilikuwa 322,500 na inazidi kuongezeka kutokana na
uhamiaji wa wananchi kutoka kilka sehemu.
Jiji hili limejengwa miaka ya
1840 sehemu ambayo kuna mto wa maji moto baada ya mhamiaji kutoka Afrika ya
Kusini aitwaye Kepteni Jonker Afrikaner kuhamia hapo na kujenga kanisa kubwa.
Hata hivyo katika miongo kadhaa baadaye vita vya wenyewe kwa wenyewe
vikapelekea kususwa kwa makazi hayo mapya hadi mwaka 1890 baada ya utawala wa
Ujerumani chini ya Meja wa jeshi Curt von Francois kuamua kuujenga upya.
Jiji la Windhoek hujulikana na
wenyeji kwa jina la Khoekhe (mto wa maji moto) na Otjiherero (mahali pa mvuke)
kufuatia kuwepo kwa mto huo wa maji moto. Haijulikani ni wapi jina Windhoek
lilikotokea ingawa wengi wanaamini kuwa linatokana na neno la Kiafrikaans
Wind-Hoek (kona ya upepo). Wengine wanasema ni Kepteni Jonker Afrikaner
aliyetoa jina la Windhoek kufuatia jina la milima ya Winterhoek iliyoko huko
Tulbah, Afrika ya Kusini, walikotokea mababu zake.
Windhoek ni mojawapo ya majiji katika bara
la Afrika yaliyojengwa kwa mpangillio mzuri na masafi kupindukia. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
wako wachache mno wana haki ya kuwa hivyo
ReplyDelete