Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (MB) ametangaza kuanza rasmi kwa msako wa wafanyabiashara wa sekta ya utalii (makanjanja) wanaofanya biashara kinyume na taratibu. 
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania, Mamlaka ya Rufaa na Kamati ya Ushauri wa Kitaalam vya Wizara alisema, serikali imeamua kupambana na wafanyabiashara wa sekta ya utalii wanaoikosesha mapato kwa kufanya biashara hiyo kinyume na taratibu. 
 “Leo ninazindua Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania inayoundwa na watu makini, watu ambao hawawezi kusukumwa na rushwa ndogo ndogo ili kuziba mianya yote ambayo inasababisha serikali kukosa mapato. 
Hivyo kupitia bodi hii, sasa mfanyabiashara na serikali wote watapata faida,” alisema Mhe. Kagasheki. 
Aidha aliongeza kuwa, hivi sasa leseni nyingi zimekwisha muda wake na hivyo wafanyabishara wanalazimika kuomba upya na hapo ndipo vyombo hivyo vipya vitakapoanza msako kwa kutekeleza majukumu yake ya kusaidia katika usimamizi, kutoa miongozo na ushauri wa kitaalam kulingana na sera na sheria. 
Mhe. Kagasheki aliongeza kuwa, kuundwa kwa vyombo hivyo ni suluhisho katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini.
 Mwenyekiti na Wajumbe wateule Mamlaka ya wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (MB) (wapili kutoka kulia kwa waliosimama msitari wa mbele) mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Ngorongoro ulioko Maqkao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es salaam.
Wenyeviti na Wajumbe wateule wa vyombo vitatu, Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania, Mamlaka ya Rufaa na  Kamati ya Ushauri wa Kitaalam wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (MB) (wanne kutoka kulia kwa waliosimama msitari wa mbele) mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Ngorongoro ulioko Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ahsanteni sana Mawaziri wa Serikali kwa Operesheni mbalimbali zinazo ashiria kuboresha mambo nchini Tanzania!

    Baada ya Kimbunga cha Dr. Nchimbi na sasa tunapata Kiama cha Balozi Kagasheki, pia unaomba na Mawaziri wengine waanzishe Operesheni zao kwa kuboresha Tanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...