Meneja wa Hisa wa Benki ya CRDB Makao Makuu, Emanuel Ng'ui, akizungumza na wenye hisa wa CRDB Bank, katika semina ya uhamasishaji kuhusu matumizi ya Hisa.
Mkurugenzi wa CRDB Bank, PLC, Tawi la Lumumba, John Almasy, akizungumza na Meneja wa Hisa wa Benki ya CRDB Makao Makuu, na Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Vijana, Pelesi Fungo, wakati wa semina hiyo.

Umetolewa Mwito kwa Watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji kwa ununuzi wa hisa katika soko la hisa la Jumuiya ya Afrika linalotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni, na ili Watanzania nao waweze kufaidika na umiliki wa hisa kupitia masoko ya hisa, mitaji na dhamana.

Wito huo, umetolewa na Meneja wa Meneja wa Hisa wa CRDB Makao Makuu, Bw. Emanuel Ng’ui wakati wa semina ya uhamasishaji kwa wanahisa wa Benki ya CRDB, iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Peacock.

Bw. Ng’ui amesema, Watanzaniaq bado wana mwamko mdogo wa kiuzitumia fursa za uwekezaji kupitia masoko ya hisa mijaji na dhamana, ambapo mpaka sasa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, DSE, tayari tunao raia wa nchi za kigeni waliojisajili, huku Watanzania wenyewe tukiendelea kusua sua, hivyo Benki ya CRDB, imeamua kuwahamasisha wanahisa wake na wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa hizi.

Mkurugenzi wa CRDB Bank, Tawi la Lumumba, Bw. John Almasy, amewahimiza Watanzania kuchangamkia fursa hizo, hivyo kuzuia Watanzania kuachwa nyuma katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, ambapo uanzishwaji wa soko la pamoja la hisa la Jumuiya ya Mashariki litaanzishwa.

Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Kijitonyama, Bw. Lucas Busigazi,  amewahimiza wanahisa wa Benki ya CRDB kuendelea kujitokeza kwa wingi katika semina hizo, ili kutimiza malengo ya Benki ya CRDB kuwa ni benki kiongozi kwa uwezeshaji Watanzania kuumiliki sio tuu uchumi wa Tanzania, bali hata uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nae Mkurugenzi wa CRDB, Tawi la Vijana, Bw. Pelesi Fungo, amesema semina hizo ni za manufaa sana kwa wanahisa wa Benki ya CRDB na Watanzania kwa ujumla ili kuwapatia Watanzania elimu na ufahamu kuhusu uwekezaji katika hisa, hivyo kuwa ni wamiliki wa makampuni mbalimbali.

Semina hiyo imehudhuriwa na washiriki zaidi ya 100, ambapo CRDB Bank, itaendelea kufanya semina kama hizo kwa mikoa yote Tanzania nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...