Na Bashir
Yakub
Kisheria yapo mambo
mengi ambayo huweza
kubatilisha mkataba wa
ajira kati ya
mwajiri na mwajiriwa. Mkataba wa
ajira sawa na
mikataba mingine yote huzaliwa, huishi
na hufa. Huzaliwa pale
tu unaposainiwa , huishi
pale unapoanza kutekelezwa
na hufa pale
yanapojitokeza baadhi ya
mambo ambayo yameainishwa
na sheria kama
mambo yanayoua mkataba wa
ajira.
Aidha zipo taratibu maalum
za kumaliza/kuua mkataba
wa ajira na
hii ni katika
mazingira yote, yaani mazingira ya kumaliza
mkataba kwa hiari
na yale ya kumaliza kwa
kulazimika kutokana na
sababu mbalimbali.
Kumaliza mkataba
wa ajira kwa
hiari kumekuwa hakuleti
shida sana kama
ilivyo kumaliza mkataba
wa ajira kwa kulazimika hasa linapokuja suala la sababu za kinidhamu
kama tutakavyoona.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...