Katapila likizikanyagakanyaga kwa lengo la kuziharibu bidhaa mbalimbali zikiwemo pampasi na dawa za meno zilizopitwa na wakati na zingine zisizo na ubora katika Dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam.  Bidhaa hizo zenye thamani ya sh. mil. 20, kutoka Marekani na China zilikamatwa  na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA ZOTE  NA RICHARD MWAIKENDA



Na Charity James


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeteketeza bidhaa hafifu na zilizokwisha muda wake zenye thamani ya sh. milioni 20 kutoka nchini Marekani na China.


Akizungumza wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo,Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa TBS, Roida Andusamile alizitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za meno, pampas, sabuni za kuogea na wipes.


Alisema miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni kwaajili ya kutoa msaada katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara huku nyingine zikiingizwa kwaajili ya biashara.


"Kazi ya kuteketeza bidhaa zenye ubora hafifu ni endelevu lengo letu ni kuhakikisha tunaepusha madhara kwa watumiaji ambao wanashindwa kutambua bidhaa hafifu," alisema.


Alisema bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe za biashara au misaada ni lazima zipimwe kwa lengo la kuondoa changamoto ya kuwauzia au kugawa zikiwa ni hafifu au kuisha muda wake.


Kwa upande wake, Ofisa Mdhibiti Ubora wa TBS, Salome Emmanuel alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuakikisha wanaingiza bidhaa zenye ubora na kuongeza wafanyabiashara ndio walinzi tosha wa kuhakikisha bidhaa hafifu haziingizwi nchini hivyo ni vizuri wakafuata sheria kukwepa tatizo hilo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wataalamu wa mazingira na uteketezaji wa visivyotakiwa tusaidieni namna bora ya kuteteketeza bidhaa nk. Hili la kusadia pampers ambazo ni plastic ardhini kwa uelewa wangu mdogo sioni kama ni sahihi. Baadha ya bidhaa hizi zingechambuliwa kwa aina na kufanyiwa recycling ingekuwa bora zaidi. Niko tayari kwa usahihishwaji ili kujifunza.
    Mdau wa mazingira bora na salama

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...