Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
UONGOZI Profesa Joseph Semboja (wapili kutoka kushoto) akizungumza na kundi la
waandishi wa habari kutoka nchini Finland (hawapo pichani) mapema leo
walipotembelea taasisi hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano
katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen, Mshauri wa
masuala ya Ushirikiano kutoka Taasisi ya UONGOZI Bi. Liisa Tervo na Mkuu wa
Utafiti na Sera kutoka Taasisi ya UONGOZI Bw. Dennis Rweyemamu.
Kundi la waandishi wa habari 15
kutoka nchini Finland waliotembelea Taasisi ya UONGOZI mapema leo ikiwa ni moja
kati ya mafunzo yao katika programu maalum ya maendeleo na sera inayoratibiwa
na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland. Waandishi hao ambao wapo nchini kwa muda
wa siku tano pia walisindikizwa na watumishi wawili kutoka Wizara ya Mambo ya
Nje ya Finlan.
Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika
Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen (kushoto) akitoa neno
lake la shukrani kwa niaba ya waandishi wa habari na maafisa kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje ya Finland, walipotembelea Taasisi ya UONGOZI kufahamu shughuli
zake mapema leo.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...