WAZIRI waNchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh,George Simba Chawene amempa siku tatu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda kuhakikisha anaunda kamati maalumu ambayoitafanya uchunguzi kubaini viongozi wa vijiji na wakuu wa sekondari wa wilayaya karatu wanaotumia vibaya uongozi wao hali iliyopelekea kuwepo kwamalalamiko.
Waziri Simbachawene aliyasema hayo wakati alipokuwa kwenye uzinduzi wa majengo ya ofisi na maendelo ya parokia na Karakana ya Chuo cha Ufundi Audrey Veldamaniliyopo kijiji cha Kitete Wilayani Karatu Mkoani Arusha ambavyo vinamilikiwa naKanisa katoliki Parokia ya Kitete.
Alisema kuwa kutokana na malalamiko aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja nawananchi katika Wilaya ya Karatu kuhusiana na kuwepo kwa baadhi ya viongozi wavijiji na wakuu wa shule za Sekondari kutumia vibaya uongozi wao ahakikisheanaunda kamati hiyo ili watakapobaini ukweli waweze kutumbuliwa majipu harakasana.
‘’Mkuu waMkoa nakupa siku tatu fatilia jambo hili kuna ubadilifu mwingi upo wizi wafedha wakuu wa shule wamekuwa wakiiba hela za wazazi,ufaulu kwa wanafunziumeshuka sana katika shule zote za Karatu ,viongozi wa kijiji, kata hawako makini na kazi sasa unda kamati ili tupate ushahidi wa kudumuili tuwatimue’’alisema Simbachawene.
Pia alimpasiku saba Mkuu huyo wa Mkoa kuhakikisha anashushughulika suala la kuboreshamiundo mbinu hususani barabara ambayo imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa vijijivi navyozunguka Wilaya ya Karatu akidai kwamba anapaswa kukutana na wakurugenziwa monduli na karatu kukutana na kupanga namna ya kufungua barabara kuanziaManyara,inayopita sabasaba ,kitete ,Lostete mpaka serera katika kipindi hikicha mwaka huu wa fedha huku akimsihi kuanza kufikiria Barabara ya Namangakupitia Monduli ,ziwaNatron ili iwe ya Mkoa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...