Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafnyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, na kufanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2016. 
 
Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kwa viongozi hao juu ya shughuli za Mfuko na faida ya wafanyakazi kupatiwa fidia endapo patatokea madhara awapo kazini. Wengine pichani ni mgeni rasmi, Pendo Z.Berege, (Mwakilishi wa Msajili wa vyama vya afanyakazi na waajiri, na Peter J. Mbelwa kutoka Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umeendesha semina ya siku moja kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kuwalipia michango ya mwezi.

Semina hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Aprili 19, 2016, ilifunguliwa na mwakilishi wa Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri, Bi.Pendo Z.Berege.Katika hotuba yake, Bi. Berege alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatwapo na majanga wakiwa kazini.

Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi No. 20 ya mwaka 2008.Akiwakaribisha wana semina kwenye semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Msomba alisema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi na kwa kutambua kuwa viongozi wa wafanyakazi ndio wadau wakuu wa Mfuko huo, semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.

Akitoa mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi waumiapo kazini.
Naye Bi.Amina Likungwala kutoka WCF, amesema katika mada yake ya Wajibu wa Vyama vya Wafanyakazi ambapo alisema, ni wajibu wa vyama kutoa elimu kwa wanachama wao ambao ni wafanyakazi lakini pia kuwaeleza waajiri umuhimu wa kutoa michango kwa wakati 

Mshiriki akisoma kijitabu chenye maelezo ya kina kinachofafanua majibu ya maswali ya mara kwa mara ambayo wadau wanataka kujua kuhusu WCF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba.
Mzee Mchafu Chakoma, mwakilishi wa viongozi wa wafanyakazi akitoa neno la shukrani.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Malipo yanafanyika baada ya mda gani madai yanapokuwa yamehakikiwa?

    ReplyDelete
  2. Malipo y fidia yanachukua muda gani baada y kuhakikiwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...