Moja ya changamoto kubwa zinazoikabili miji katika kanda ya Afrika Mashariki, ni uchafuzi wa mazingira, hasa kutokana kushindwa kusimamia kwa ufanisi suala zima la usafi.
Kwa mujibu wa uchumbuzi wa DW, ukiacha mji wa Kigali, ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa kudhibiti uchafuzi wa mazingira hasa utupaji hovyo wa takataka, miji mingine kama vile Dar es Salaam, Nairobi, na Kampala bado ina safari ndefu ya kufikia kiwango cha usafi.
Kigali ni mji mkuu wa Rwanda na pia mji mkubwa kuliko mingine yote nchini humo.
Iko karibu sana na mstari wa ikweta kwenye kimo cha 1400 - 1600 m juu ya UB. Hali ya hewa ni ya wastani hakuna baridi kali wala joto kali.
Kigali ina wakazi 600,000.
Kigali ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani mwaka 1907 kama kituo cha mwakilishi wa Afrika ya Masharikiy a Kijerumani Richard Kandt. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivamiwa na Wabelgiji ikawa sehemu ya eneo la kukabidhiwa la Rwanda-Urundi chini ya utawala wa Ubelgiji.
Baada ya kugawa kwa Rwanda-Urundi kuwa nchi mbili za Rwanda na Burundi Kgali ikawa mji mkuu wa Rwanda mwaka 1962.
Mauaji ya Watutsi ya mwaka 1994 yalianza Kigali. Mji ulipungukiwa wakazi 100,000 wakati ule. Hivi sasa Kigali imebadilika na kuwa mojawapo ya miji misafi na yenye wananchi wanaotii sheria bila shuruti katika bara la Afrika.
Mji wa Kigali kama umepigwa deki. Mhe Paul Makonda na wakuu wa mikoa wengine wote na wakuu wa wilaya mpo hapo? Iko haja kwenda huko na kujifunza wenzetu wanatumia uchawi gani kufanikisha hayo...
Mitaa kama sebule ya hoteli
Utii wa sheria bila shuruti. Kwenye taa nyekundu hata bodaboda wanasimama
Hivi ndivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anavyotaka miji yake ionekane. Safi na watumia barabara watii sheria bila shuruti.
Katika kutii sheria bila shuruti huko ni pamoja na kila dereva wa bodaboda na abiria wake kuvaa kofia. Sheria kali ndogondogo zikiwekwa na kusimamiwa na kutekelezwa ipaswavyo kama ilivyo katiia mji wa Kigali hili linawezekana kabisa!
Tanzania itafikia huko miaka 50 ijayo kama tabia hazitabadilika. Utakuta msomi mzima anakunywa maji kwenye chupa ya uhai, halafu anarusha chupa tupu barabarani bila aibu. Mimi hata watoto wangu huwa nawaambia endapo tunatumia usafiri binafsi kuwa "ni vizuri kutunza uchafu wote kwenye gari, tukifika nyumbani tutatupa kwenye shimo la taka" mindset ni muhimu, watu kuharibu miundombinu wanayowekewa kwa makusudi, barabara mbovu zinazokosa repair za mara kwa mara, mfano barabara za mitaani ni mbovu kuliko maelezo, ndiyo maana hata ukiweka mifumo ya taka, haiwezi kudumu, ulinzi wa miundombinu inapotengenezwa haupo. Lakini pia Serikali haijachukua hatua za kuhakikisha Wizara inayosimamia mazingira inaandaa mifumo mizuri ya uyeyushaji taka taka. Wawape watu fursa za kuweka makampuni mahsusi kwa kukusanya taka na kuziharibu. Sjui inawezekana hayo makampuni yalishakuwapo lakini yanashindwa kujiendesha kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. Nashauri mamlaka husika zichukue hatua na kuthubutu. Nafikiri lile wazo la Mhe. Rais lingeendelea kwa vitendo la kufanya usafi, kidogo kidogo wazipe kampuni zabuni na kuwalipa, watafanya tu. Watanzania tunasifika kwa mawazo mazuri, lakini utekelezaji 0. Hivi vitu tunavyovisema havifanyiki bila fedha, lazima kuwekeza kwenye maeneo muhimu kama haya!
ReplyDeleteNdugu hapo juu naona umeupigia debe kwa bidii mji huo wa Kigali. Kweli ni mji safi na wenye ustaarab na wastaarab.Ningependa sana kuona miji yetu ifikie usafi kama huo.Lakini kumbuka kama uko uchi huwezi kuvaa kilemba.WABONGO BADO WANA MATATIZO MENGI.Watoto hawana sembe,mama watoto mjamzito na mgonjwa nawe jogoo huna hata senti mfukoni, jee kaka katika hali hiyo ukisahau usafi kidogo ni dhambi? I am making no excuses.We must strive to get there by hook or crook.Al awal pawepo na sheria moto moto, ukikamatwa unatupa taka, urithiswe ufagio na debe la taka na ufagie barabara kwa wiki mbili,Ikiwa barabara yenu safi mpewe tunzo angalau free airtime au tikiti za daladala. THE CARROT AND STICK STUFF
ReplyDeleteNatamani miji yetu yote iwe misafi na michirizi ilyochorwa taa za barabarani tujifunze kwa wenzetu na uinua viwango kunawezekana.
ReplyDeleteHiyo mitaa mnayo sifia ya Kigari yote haina nuru wala harufu ya amani na mwenye jicho la 3 hatopata taabu kunielewa ila sisi watanzania uchafu tunajitakia wenyewe kwa ujinga wa viongozi wetu wa maeneo yetu ila wakiweka sheria kali za kuwa wajibisha watupa taka ovyo mambo yangekua sawa hata kesho
ReplyDeleteHivi mnaijua Rwanda aum mnadanganywa na mnayoyaona mijini? Tanzania haina la kujifunza huko. Labda kujifunza UDIKTETA. Kwa hilo tu. Na udikteta Tanzania haukubaliki kamwe.
ReplyDeleteWeee anon hapo juu, wenzako wameweka msisitizo wa kujifunza kuyaweka mazingira yetu katika khali ya usafi wee nawe unaleta msahara mwengine mara udikteta mara hiyo Rwanda myonage hivyohivyo. Hayo yote yanatokea Wapi? Hapa habari ni usafi, Tanzania tu wachafu jeee wala hatuyapendi mazingira yetu mpka majumbani mwetu kwa walio wengi alafu kutwa kusingizia umasikini ndio maana magonjwa kama ya vipindupindu, magonjwa ya njia za mkojo, typhod,maralia hayaishi ni kutokana na muendelezo wa jamii kuchukulia uchafu ni sehemu mmja wapo ya jamiii wanayoishi, tena mtu utakuta anakutilia sisi wagumu huku khali zote tunaziweza hmmm uvivu tu, wachafu kweli. Na huu mji wa dar ni kiooo cha jamii yetu sisi watanzania tusipoupenda tunaoneka wite ni wachafu tu
ReplyDelete