Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wapili kulia) akipokea vitabu vinavyotumika kuhamasisha jamii hasa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari kujiepusha na matumizi ya Dawa ya Kulevya pamoja na kuhifadhi mazingira kutoka kwa ujumbe kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia Dawa ya Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akisalimiana na Bw. Kishor Thakrar kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia Dawa za Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumpatia vitabu vinavyohamasisha jamii iliyo huru, leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wapili kulia) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia Dawa za Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha vitabu wanavyovitumia kutoa elimu hiyo kwa jamii hasa katika shule za msingi na sekondari leo jijini Dar es Salaam.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...