Na
Eleuteri Mangi – WHUSM.
Serikali imesaini Mkataba
na Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa pamoja na Uwanja wa Uhuru kwa
ajili ya michezo yote ya Kimataifa pamoja na michezo ya Ligi Kuu ya ndani.
Mkataba huo umesainiwa
leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Serikali na Kaimu Katibu Mkuu
wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit kwa niaba ya Klabu ya Yanga.
Katika Mkataba huo,
Klabu ya Yanga imeruhusiwa kutumia viwanja hivyo kama viwanja vyake vya
nyumbani kwa sharti la kuvitunza viwanja hivyo wakati wote wanapovitumia.
Miongoni mwa masharti
hayo ni kutunza viwanja, mali na vifaa vyote vilivyopo katika viwanja hivyo, na
endapo kutatokea uharibifu wowote utakaofanywa na wachezaji ama mashabiki,
Klabu hiyo itawajibika kubeba gharama za matengenezo yote yatakayotokana na
uharibifu huo.
Aidha, Klabu ya Yanga
inaweza kutumia viwanja hivyo kwa mazoezi ya kujianadaa na mechi
zinazowakabili.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akisaini Mkataba kwa niaba ya Serikali na Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam ambayo iliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Baraka Deusdedit (kulia) leo jijini Dar es salaam. Mkataba huo unahusu Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na Uwanja wa Uhuru katika mechi za Kimataifa na Ligi Kuu. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Evordy Kyando.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akibadilishana Mkataba waliosaini na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit leo jijini Dar es salaam. Mkataba huo unahusu Kalabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na Uwanja wa Uhuru, Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) mara baada ya kusaini Mkataba na Klabu ya Yanga leo jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...