Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti amewataka Wananchi Wa Wilaya ya Buhigwe kuzingatia kanuni za ujenzi kwa kujenga Nyumba zenye ubora na kupanda miti katika Nyumba zao ili kuepukana na majanga yatokanayo na Upepo mkali pamoja na Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha na kusababisha madhara makubwa .

Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Mnyegera ambapo upepo mkali ulitokea huko na kusababisha nyumba tisa kuezuliwa na kusababisha uharibifu wenye thamani ya Shilingi milioni 13 wakati akitembelea kuangalia uharibifu huo, Gaguti alisema nyumba nyingi zilizoezuliwa hazijajengwa kwa kuzingatia kanuni za ujenzi.

Gaguti alisema ili kuhakikisha tatizo hilo linakwisha Wilaya imeandaa utaratibu wa kupanda miti milioni moja na laki moja kwa Wilaya nzima na wananchi wote wanatakiwa kuzingatia utaratibu huo,Viongozi wa vijiji wanatakiwa kuzingatia zoezi hilo kila nyumba kupanda miti ya kutosha ili kuepukana na madhara ya kuharibikiwa Nyumba.

Aidha Gaguti aliwaomba viongozi wa kijiji kuwasaidia wote waliopatwa na majanga hayo kwa kipindi hiki ambacho serikali inatafuta namna ya kuwasaidia ili waweze kupata mahali pa kuzihifadhi familia zao.

"Poleni sana kwa majanga yaliyo wapata nimetembelea kote ambapo kimbunga kimeezua nyumba lakini hakuna majanga yaliyo tokea ya watu kupoteza maisha wala uharibifu wa mazao ni jambo la kumshukuru mungu kunabaadhi ya Bati zinaweza kutumika nahisi tasmini iliyofanyika inaweza kupungua, niwaombe tupande miti ilikujikinga na tatizo hili wakati tunasikitika kwa tukio lililojitokeza na niwaombe viongozi nione jitihada zenu kwa kuwasaidia sisi tutawasaidia kama Wilaya baada ya kuona juhudi zenu za kusaidiana",alisema Gaguti.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mnyegera Alfonce Ntatie alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 6 Januari, ambapo kulitokea upepo mkubwa ambao ulieezua nyumba tisa na Kusababisha uharibifu wa shilingi milioni 13 ambapo Mpaka sasa juhudi za kuwasaidia wathilika wa tukio hilo zinaendelea kufanyika na Wananchi wanaendelea kuwachangia wenzao. 

kwa upande wao Baadhi ya Wananchi walio haribiwa nyumba zao na upepo mkari walisema Mpaka sasa wanalazimika kulala nje na familia zao suala ambalo linawapa wakati mgumu hasa ukuzingatia wakati huu ni wakqti wa Mvua.zinaendelea kunyesha na zikinyesha wanalazimika kunyeshewa na watoto wao.
 Moja ya nyumba iliyoezuliwa paa kama ionekanavyo pichani.
  MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akiratibu tukio la kuezuliwa paa baadhi ya nyumba za wakazi wa kijiji cha Mnyegera wilayani Buhingwe kufuatia upepo mkali uliotokea wilayani humo na kupelekea nyumba tisa kuezuliwa paa zake. 
 MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akiwapa pole Wananchi wa kijiji cha Mnyegera wilayani Buhingwe kufuatia upepo mkali uliotokea na kusababisha nyumba tisa kuezuliwa na kusababisha uharibifu wenye thamani ya Shilingi milioni 13.
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akiwa pamoja na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mnyegera wilayani Buhingwe waliothiriwa na  
upepo mkali uliotokea na kusababisha nyumba tisa kuezuliwa mapaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...