Bondia Floyd Mayweather amemchapa mpinzania wake Conor McGregor kwa TKO ya raundi ya 10 kwenye mpambano wao alfajiri ya leo huko Las Vegas, Marekani, ukiwa ni ushindi wake wa 50 bila kushindwa na mara tu baada ya mpambano huo akatangaza kujiuzuru masumbwi.

McGregor, ambaye wengi walimbeza kabla ya pambano, alishangaza wengi kwa kucheza kiweledi na hata vituko ulingoni ambako kuna wakati aliweka mikono nyuma wakati wa mchezo.

Kwenye raundi za awali McGregor alitawala mchezo kwa kumshambulia Mayweather aliyejikuta anajikinga zaidi ya kurudisha makombora. Hata hivyo baadaye hiyo ikaja kugundulika kuwa ni mbinu mbadala kwani mpinzania wake ambaye hakuwahi kucheza masumbwi bali kickboxing alionekana kuchoka na raundi ya 10 refa akasitisha mpambano baada ya kumuona kazidiwa.
BondiaMayweather kajishindia dola za Kimarekani 100 wakati McGregor kaondoka na dola milioni 30. Si haba kwa kazi ya usiku mmoja.
Hata hivyo jedwali hapa chini linaonesha jinsi McGregor ambaye ni rais wa Ireland na bingwa wa Mixed Martial Arts (MMA) ama sanaa mchanganyiko za mapambano, alikuwa nyuma kwa pointi moja tu wakati refa anasimamisha pambano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...