Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika sekta ya utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa barabara na pia kuweka mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii viliovyoko kanda ya Kusini ili vichangie ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi. 

Makamu wa Rais aliyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania uliofanyika Kihesa Kilolo mkoani Iringa.Makamu wa Rais alisema Serikali imeendelea kuandaa na kutekeleza mipango mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za utalii zinasambaa nchi nzima .

Makamu wa Rais amasema katika kuendeleza utalii kanda ya kusini, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye masharti nafuu Dola za kimarekani milioni 150 kutoka benki ya Dunia ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6 kuanzia 2017/2018.

Mradi huo wenye lengo kuu la kukuza utalii na kipato kwa wananchi kwa kuboresha miundo mbinu, kujenga uwezo katika usimamizi wa maliasili na kuwawezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la mradi wa REGROW na Mikataba ya Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...