Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam limepitisha makadirio ya mapato kwa mwaka 2018/2019

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa Mwaka 2018/2019 imekadiria kutumia fedha Sh. 98,238,193,600 ambapo katika fedha hizo Sh. 76,607,163,700 ni matumizi ya kawaida na mishahara ambayo sawa na asilimia 78 ya Bajeti yote .Wakati Sh 21,631,029,900 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo sawa na asilimia 22 ya bajeti yote.

Akizungumzia makadirio hayo Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob amesena wamekidhi kigezo cha kutenga asilimia 60 ya fedha za mapato ya ndani katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ambayo ni Sh.12,600,760,400.00 na Sh. 8,498,717,600 sawa na asilimia 40 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na nishahara.

Akifafanu zaidi wakati anasoma bajeti hiyo Jacob amesoma vipaumbele 17 vya Halmashauri kwa mwaka 2018/2019.Ametaja vipaumbele hivyo ni ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Sh bilioni 3, uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji mapato ya ndani,kukusanya Sh.bilioni 25.7

Pia miradi ya maendeleo imetengewa fedha kiasi cha Sh.billioni 21.6 wakati kipaumbele cha nne kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kununua dawa na vifaa tiba Sh.bilioni 8.2.Jacob ametaja kipaumbele cha tano ni kupandisha maslahi ya wajumbe Serikali za Mitaa kutoka sh. 5000 kwa mwezi mpaka sh 20,000 kwa mwezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...