*RC Makonda aongeza muda wa kupiga muziki
*Asema mwisho iwe saa nane usiku,atoa maagizo

Na Khadija Seif ,Globu ya jamii

NI upendo wa aina yake ambao msanii Nassem Abdull 'Diamond'ameamua kuufanya kwa wananchi wa Kata ya Tandale jijini Dar es Salaam.
Unajua kwanini?Iko hivi msanii huyo leo ameamua kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujumuika na wananchi hao na kubwa zaidi ametumia nafasi hiyo kurejesha ahsante kwa wananchi hao.

Katika sherehe hizo Diamond ameamua kufanya mambo yenye kugusa jamii kutokana na aina ya misaada ambayoa ameitoa kwa wananchi hao ambapo ameamua kugawa bodaboda kwa vijana wa Tandale na kugawa kadi za bima 1000 kwa wananchi wa Tandale.

Pia msanii huyo ameamua kutoa msaada wa bajaji kwa mama mwenye ulemavu baada ya kuona anahitaji msaada kwa kumpatia chombo hicho ambacho kitamsaidia mama huyo.Wakati wa sherehe hiyo ikiendelea Diamond hakusita kueleza changamoto ambazo amezipitia katika maisha yake hadi kufika hapo alikofikia.

Pamoja na yote Diamond ametoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuondoa zuio la kufanya muziki mwisho saa sita usiku."Tunaomba Mkuu wa Mkoa hili zuio la mwisho saa sita usiku uliondoe kwani limetubana sana.

"Watu wa Dar ikifika saa sita ndio wanataka kutoka kwenda kwenye kumbi za sterehe, lakini kwa katazo lililopo inakuwa ngumu.Hivyo tunaomba ulitazame hili ili tuendelee kudamshi,"amesema Diamond.Pia ameomba kwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kuwapatia eneo WCB ili wajenge studio kwa ajili ya wasanii wa muziki wa Tandale.

Kwa upande wa watu waliokuwa eneo hilo wengi wao wameonesha kufurahishwa na kitendo cha Diamond na kumpongeza kwa uamuzi wake wa kusaidia jamii.Hata hivyo Makonda akizungumza kwenye tukio hilo ametoa maagizo ya kuhakikisha linapatikana eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha mpira pamoja na kiwanja ambacho kitajengwa shule ya msingi kwa ajili ya wananchi wa Tandale.

Kuhusu kuongezwa muda kwa ajili ya burudani Makonda amesema suala hilo lipo kisheria na la muda mrefu kidogo na kufafanua zaidi kuwa kuna sheria ya mazingira, ambapo kelele nazo ni sehemu ya uchafuzi wa mazingira.Hata hivyo baada ya maelezo mengi ametangaza kuanzia leo ameongeza muda wa kupiga muziki ambapo sasa watapiga hadi saa nane usiku badala ya saa sita usiku kwa kila wikend.

Hivyo ametoa maagizo kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutowakamata watu wanaopiga muziki hadi saa nane usiku na kwamba Jiji la Dar ndio jiji la starehe na ushauri wake ni vema watu wakajenga kumbi za ndani.

Wasanii mbalimbali nao wamepata nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yao na kubwa zaidi ni namna ambavyo Diamond amethibitisha wananchi wa Tandale ni sehemu ya maisha yake.
 Msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdull a.k.a Diamond Platnumz akizungumza na mashabiki wake wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
 Mkuu ya Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye pia ni Mlezi wa kundi la Wasanii WCB ,akizungumza wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
Msanii Nyota wa Bongofleva Nasseb Abdul a.k.a Diamond akimsikiliza mmoja wa akina Mama Bi Evodia Nchimbi ambaye ni mlemavu wa Miguu,alipokuwa akimshukuru huku akitoa machozi na kutoamini kwa kile kilichotokea,kwa kupewa zawadi ya Bajaji ili aweze  kujikimu kimaisha na kuisaidia familia yake,Mama huyo mkazi wa Tandale amemshukuru Diamond kwa kumpa zawadi hiyo kwani hakutegemea na kwamba agalau sasa ataweza kuwa na ahuweni ya maisha.
Mama mlemavu wa miguu ambae ni dereva wa Bajaji akiwa ndani ya Bajaji aliyopewa zawadi na Msanii Diamond mbele ya umati wa wakazi wa Tandale ukishuhudia sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda.
Daimond akimkabidhi nyaraka za gali aliyomnunulia mpiga picha wake aliyemtaja kwa jina moja la Lukamba,kama zawadi kwa jitihada na kujituma katika kazi ambazo amekuwa akizifanya kila siku 
Aliyewahi kuwa Miss Tanzania Jacqueline Mengi akiwasalimia wananchi wa Tandale  wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
Msemaji wa Simba Haji Manara akizungumza jambo kwenye hafla hiyo iliyofanyika Tandale 
Msanii wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro 'Chid Benz' akitoa burudani kwenye hafla hiyo 
Baadhi ya wananchi wa Tandale wakiwa katika sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...