Na Khadija Seif , Globu ya Jamii
HATIMAYE msanii maarufu nchini katika muziki wa Bongo Fleva Nasseb Abdull a.k.a Diamond  amevunja ukimya kwa kutaja siri iliyomfanya afanikiwe kwenye muziki huo.

Wakati Diamond anataka kutaja siri iliyomfikisha katika kilele cha mafaniko mamia ya wananchi wa Tandale, viongozi wa ngazi wa Mkoa wa Dar es Salaa pamoja na wageni waalikwa walikuwa kimya.

Diamond alianza kueleza hatua hatua sababu ambazo zimemfanya awe na mafanikio katika maisha yake ni siri kubwa ya kufanikiwa kwake anasema hachagui kazi ya kufanya.

"Katika maisha yangu sijawahi kuchagua kazi ya kufanya.Ndio maana kwenye maisha yangu nimefanya kazi nyingi sana.Nimefanya kazi ya kuuza mafuta sheli.nimefanya kazi ya kupiga picha kwenye kumbi za harusi pamoja na nimefanya kazi ya kuuza nguo Tandale.

"Siri nyingine ni kujenga uaminifu kwa watu ambao unafanya nao kazi.Uaminifu umenisaidia sana na ndio maana leo niko hapa,"amesema Diamond.

Amesema siri nyingine ni ubunifu na kufafanua baada ya kufanya kazi kwa bidii aliamua kuwa mbunifu kwa kila alichokuwa akikifanya.

Pia amesema kuomba Mungu ni jambo la msingi sana na katika maisha yake moja ya jambo ambalo lazima alifanye ni kumuomba Mungu na amemsadia kumfikisha hapo alipofika.

"Nimekuwa nikimuomba Mungu anisaidie katika shughuli zangu za muziki .Napoomba nataja kaabisa kile ambacho nahitaji ili kumrahisisha Mungu kile ambacho nahitaji kwake.Sitaki kumchanga kwa kuomba mambo mengi.

"Leo hii nimefanikiwa kwasababu namshikirisha Mungu,"amesema Diamond na kuongeza kuwa kwa anayetaka kufanikiwa lazima ajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya.
Bongo Fleva Naseeb Abdull a.k.a Diamond Plutnumz akizungumza na
mashabiki wake wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...