Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaonya askari wa kitengo cha Upelelezi ndani ya Jeshi hilo kuhakikisha hawajiingizi kwenye vitendo vya rushwa sambana na kufanyakazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya Jeshi.
IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na askari wanaopatiwa Mafunzo ya Upelelezi yanayofanyika katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kurasini Dar es salaam, ambapo amewataka kuhakikisha wanapunguza mlundikano wa majalada mbalimbali ya kesi, sambamba na kupata ushahidi wa kutosha utakaowatia hatiani watuhumiwa wa makosa mbalimbali mara wanapofikishwa mbele ya mahakama.
Naye Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCP Charles Kenyera, amesema kuwa, ni vyema askari wa upelelezi kujikita katika kufanyakazi kwa uaminifu ili kutenda haki kwa wananchi na kwamba Jeshi la Polisi halitosita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa askari wasiofuata taratibu na sheria za nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...